Uchaguzi 2020 Pongezi kwa CCM nyie mna macho na hekima kweli kweli

Uchaguzi 2020 Pongezi kwa CCM nyie mna macho na hekima kweli kweli

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na Mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Ama kwa hakika wale chama mboga mboga wana hekima na uwezo mkubwa wa kuona mbali zaidi labda kuliko kina sisi.

Mabwana hawa kwa hakika ndiyo maana mabingwa wao wanavuna buku 7, 7 kila siku ili wadumu!

Hawa mabwana wamesisitiza mgombea wao haji kwenye mdahalo kwa maana ana nondo za hatari mno dhidi yetu. Kutokuja kwake kumbe ni katika kutuhurumia tu. Anakuwa anasita kuja kumgaragaza mgombea wetu bwana Lissu bila huruma hali inayoweza kutufanya tupoteane kabisa.

Hongera JPM kwa kuwa na moyo mkuu hivi. Kwa hakika ni wachache sana wenye huruma kama wewe.

Jamani tusiwaudhi hawa ndugu zetu kiasi mwisho wakabatilisha mawazo yao na kumruhusu huyu mgombea akaja kutusambaratisha kikweli kweli.

Hali yetu ni tete mno kwani hata ushauri wao wa maana sana kwetu kuwa mgombea awe Membe, bwana Membe mwenyewe naye kawatolea nje. Na kwa kutosikia kwetu tunakomaa na jembe letu bwana Lissu.

Kwa hakika walikuwa na mapenzi makubwa na Membe kwa niaba yetu. Hatukuwaelewa tu.

Bahati mbaya mno kwetu, tumeshachelewa hatuendi na Membe. Basi angalau tuwasikilize sikilize ili kuchota busara zao katika maeneo yaliyosalia.

Tusiendelee kabisa kuomba midahalo. Eboo! Watatusulubu bure! Si mnajua wamejenga ma sgr, wakanunua madege, wakajenga madaraja hadi ziwani nk?

Ikiwezekana tufikirie tena kumshawishi zaidi Membe ikibid ili angalau mgombea wao akubali kuja kwenye mdahalo akiwa na ka huruma huruma tena kwa kiswahili tunachokijua vyema sisi.

Ole wetu sisi akituchenjia.

Kuna maonyo kuwa akituchenjia na akatubadilikia anaweza kuteremka bila huruma tena sasa kwa kiingereza kikali ili kutusambaratisha kabisa tusionekane tena hata humu JF. Yeye si ni mzamivu wa Kemia.

Hiiiii Bagosha!

Chonde chonde mzee baba sisi tu wamoja!

Nawasilisha.
 
😂😂😂 Magufuli ni mzuri sana kujenga hoja, Ni msomi wa kiwango kisichotia Shaka kabisa, Anajua kureason na anaongea Kama Rais sio yule anayemtukana kila siku. Nyie chadema Cha kufanya huyo asiye na sera nzuri Wala mvuto kwa watanzania mshaurini ajitoe tu tumuunge mkono Rais wetu kipenzi Cha watanzania.😂😂😂😂😂🏃 Yani naandika kusifia nafsi inanisuta vibaya Sana. Lumumba mnawezaje kudanganya nafsi? Mbona haiji?
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 magufuli ni mzuri Sana kujenga hoja, Ni msomi wa kiwango kisichotia Shaka kabisa, Anajua kureason na anaongea Kama Rais sio yule anayemtukana kila siku. Nyie chadema Cha kufanya huyo asiye na sera nzuri Wala mvuto kwa watanzania mshaurini ajitoe tu tumuunge mkono Rais wetu kipenzi Cha watanzania.😂😂😂😂😂🏃 Yani naandika kusifia nafsi inanisuta vibaya Sana. Lumumba mnawezaje kudanganya nafsi? Mbona haiji?

Mkuu nashangaa si yehodaya, binti Lowassa, magonjwa matambuka wala mzee bukililo waliotokea hata kutupia ka like jamani?

Maendeleo hayana chama na sisi tu wamoja - in mzee baba's words.
 
Back
Top Bottom