Pongezi kwa kamati ya utendaji kwa kumsimamisha uanachama Mzee Kilomoni

kimarabucha

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
791
Reaction score
621
Nachukua nafasi hii kuipongeza KAMATI ya utendaji kuamua KUMSIMAMISHA UANACHAMA MZEE Kilomoni kutokana na kufungua kesi mahakamani.Pia kumwondoa katika BARAZA la wadhamini la klabu.Mzee Kilomoni unatakiwa ujue mpira Wa Karne hii ni tofauti na mpira Wa MIAKA yenu.Mpira Wa sasa ni biashara ndio Maana bila FEDHA huwezi kufanya usajili wakati Wa MIAKA ya nyuma ilikuwa ni mapenzi ya mchezaji.Mzee Kilomoni Mchezaji Neimar Wa PSG ndio mchezaji ghali duniani ni sababu ya FEDHA.Kwa hiyo Simba inatakiwa kubadilika na kuwa ya kibiashara zaidi ili iweze kuwa na FEDHA za kununua kina Neimar.Pongezi sana Kwa maamuzi kwani huyo mzee ni Mpinga maendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wa ajabu sana kazi yao kubwabwaja tu hawajui wachezaji wanakula nini, wanahitaji nn wao wanaleta yale yale ya mwaka 1923 haya HATAKI mkutano mkuu ufanyike wakati viongozi wakuu wako mahabusu na kesi yao yaweza chukua miaka 3 so simba tukae tukisubiri hadi akina Aveva watoke jela? Watafute timu yao na shoga yake safi sana simba kwa maamuzi hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo Mzee alikuwa na hoja mkutano unatayarishwa halafu wanachama wanazuiwa kujadili taarifa ya fedha yaani uhuni mtupu
 
Mze alikuwa na uchungu kwa kile alichokisema
"timu yake"

Simba eti ni timu yake.

Badala ya kugumza mapendekezo yake katika mkutano mkuu, ana enda kusemea mahakamani.

Nadhani alikuwa anatumika na wabaya wa Simba sc.
Wakimpa pesa ili aidhohofishe Simba sc.
Hasa wale wa upande wa pili.
 
Hivi hawa wazee wa nini kwenye vilabu hivi? ???akalee wajukuu huko, zama hizi hatutaki cha wazee sisi, tunataka academies za soka na Ubingwa baasii, uzee kwenu na Ndugu zako huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi MO keshapewa timu au bado blah blah tu. ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…