Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
Naanza na pole kwa watu wa maabara kwa kupewa mitihani ya watoto wa shule wakati ninyi tayari ni watu wazima wa kazini.
Nimeona niandike thread hii kabla sijafanya mtihani hiyo ili nije niisome tena nijicheke baada ya mtihani🤫😁. Bado hayajanikuta.
Inapendeza, sasa badala ya kuchagua mtu kwa kuanzia na sijui jinsia, mara umri na hali ya afya (uzima na ulemavu) kama sifa ya kwanza sasa sifa ya kwanza kabisa imekuwa ni KUFAULU MTIHANI wa nafasi husika ✅✅.
Halafu baada ya kufaulu tukawa na uhakika kwamba hao wanaoenda kushindana kwenye oral ndio 'one of the best men/women for the job' ndio waangalie vigezo vingine. Naona ni kitu nzuri tu.
Hiyo ndio dhana ya weledi (meritocracy) yaani imelenga kuwapata wataalamu wenye weledi kwa kazi husika. Kabla ya kuangalia mambo mengine tunawachukua watu sahihi kabisa kwa kazi kwa kutumia mbinu inayoweza kuleta matokeo sahihi (pragmatic) na mengineyo.
Natamani sana kujua kama kuna takwimu za waliofaulu, wa kike na wa kiume ni wangapi? Sijui hizi data nani anaweza zichakata ukizingatia namba ya mtu ni siri. Kama vipi waitoe takwimu bila namna ya kumjua muhusika (anonymyty) watuwekee tu tulipata madaktari wa kiume watatu (30%) na wa kike saba sawa na asilimia 70%
Nikifanya mtihani alama zangu au za wenzangu zisipotosha kuitwa viva/oral interview basi ntasema tu kama wazungu "may the best man/woman win" 👊. Nakubaliana na ukweli tu kwamba miaka ya kukaa mtaani imesahaulisha mambo ya shule.
Soma Pia: Kimetulamba kwenye written interview😂
Tujitahidi kuona upande chanya wa jambo kila mara.
Mbarikiwe.