Pongezi kwa kubuni mitihani ya mchujo na interview, naiona dalili ya Tanzania yenye weledi (meritocracy)

Pongezi kwa kubuni mitihani ya mchujo na interview, naiona dalili ya Tanzania yenye weledi (meritocracy)

Tatizo la Tanzania ni wanasiasa kuvhezea Elimu yetu. Kinachofanyika sasa kinapaswa kiendano na vigezo vya udahili.
Mtu hapaswi somea udaktari kama alifeli Form Four.

Mwalimu asiwe mtu aliyefeli.
Ikiwezekana walimu walio makazini wafanyiwe tathmini na kustaafishwa kwa ulazima kwa maslahi ya baadaye
 
Wengi wanachoshindwa kuelewa NI kuwa interview siô njia Sahihi ya kupata Watendaji Bora Ila NI mchujo kama ilivyomitihani mingine.

Imelenga zaidi kwèñye Cognitive domain ya wahusika badala ya utendaji wa wahusika.
Huwezi pima utendaji wa wahusika Kwa interview ya Siku Moja.

Kumbuka interview NI sehemu assesment.

MTU anaweza akapata A lakini kwèñye utendaji akashindwa na aliyepata C
Njia gani nzuri ya mchujo ili tuwapate hao hao wenye weledi/uzoefu wa kazi?
 
Unashauri wafanyaje sasa?

Waendelee na mfumo wanaouona unafaa.

Lakini field na internship ndio ilikuwa kipimo Sahihi cha utendaji Kazi.

Makampuni binafsi hata ufaulu interview Kwa kiwango kikubwa Kisi gàni lazima wakupe Muda Wa kukutazama utendaji Kazi(probation period)
Njia gani nzuri ya mchujo ili tuwapate hao hao wenye weledi/uzoefu wa kazi?

Kipindi hichi ndîo muhimu kujua mbivu na mbichi
 
Watu wamemaliza chuo kitambo sana wamesahau sasa mjue kwanini kada zingine walikuwa wanakosa kazi. Wanesahau, wanatoa maswali tofauti, au yale wasiyotegemewa kabisa.
Kuna kitu kinaitwa CPE (Continuous professional Edu) kisomo kinapaswa kuwa endelevu ili kujilinda na usahaulifu au kiachwa nyuma.

Lakini pia ninakubaliana na wewe, wasiulizwe mambo ya elimu ya zamani isiyohusiana na kazi. Bali wataalamu waulizwe yale yanayoendana na kile watakachoenda kufanya kazini
 
Exactly. Mtu ameajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kwa zoa zoa. 8 years later anahamia NIMR kama "technical officer". Hakuna merits wala competence.​
Tutaufikia tu weledi, hatua kwa hatua.
 
Tatizo la Tanzania ni wanasiasa kuvhezea Elimu yetu. Kinachofanyika sasa kinapaswa kiendano na vigezo vya udahili.
Mtu hapaswi somea udaktari kama alifeli Form Four.

Mwalimu asiwe mtu aliyefeli.
Ikiwezekana walimu walio makazini wafanyiwe tathmini na kustaafishwa kwa ulazima kwa maslahi ya baadaye
Umenena, tuweke lengo la kufikia WELEDI katika kila sekta.

Uzuri sasa hivi watu wa kila sekta wasomi kibao wamejaa sio kama zamani ambapo tunajiuliza tukimkataa huyu tutampata nanii?.

Nakubaliana na kuwa tuitengeneze workforce yenye weledi kila idara nchi iinuke. Ili nchi iinuke tunahitaji kila idara iwe na wataalamu wenye weledi
 
Majitu ya afya mengi huwa ni mapumbavu nie mnataka interview mpewe kile mnachokijua mbona course zingine wamekuwa wakipewa hiyo mitihan hawaji humu kulalamika Kama umeshindwa tuliza makalio subir awamu nyingine
 
Makampuni binafsi hata ufaulu interview Kwa kiwango kikubwa Kisi gàni lazima wakupe Muda Wa kukutazama utendaji Kazi(probation period)
Hii wanaweza kuiongeza, sema kabla ya kuiongeza wahakikishe kwanza kuna mifumo ya haki ya kufanya hiyo mitazamio.

Ila kama haipo mifumo hili tuliache kwanza
 
Yan daktari nakosa kazi eti kisa sijajibu vizuri nilipoulizwa tell us about yourself au sijajibu vzr mtihani wenye topic za physics za olevel duh
 
Hapo vigezo itakuwa bado havijatosha mfano hawana diploma/digrii husika.
Vigezo vya kupata kazi sasahivi ni kufaulu mtihani wa utumishi na sio kuwa na degree/ diploma Wala cheti mkuu.
Issue mtihani TU hata kwa mfano ukiwa wa hesabu za kuchagua ukifeli aijalishi wewe umesoma miaka 6 udaktari sijui una leseni ya Nini
 
Sisi tena atuzitaki wapeni watoto wa form 1 B hizo kazi za kuwapima tezi dume mana kipimo Cha utendaji kazi wao watakifikia watabutua vibaya mnoo hizo Pepa zenu
Usaili wa oral ndio unaamua mshindi baba.Cha muhimu wote walioingia oral wana sifa za msingi za kada husika so wataweza kazi hivyo dua la kuku halitampata mwewe
 
Vigezo vya kupata kazi sasahivi ni kufaulu mtihani wa utumishi na sio kuwa na degree/ diploma Wala cheti mkuu.
Issue mtihani TU hata kwa mfano ukiwa wa hesabu za kuchagua ukifeli aijalishi wewe umesoma miaka 6 udaktari sijui una leseni ya Nini
kama sio hizo digrii na diploma mbona wanakagua kabla hawajaingia katika mtihani wenyewe!??

Tena mtihani hata sio kigezo cha pili ni kama cha saba huko maana kuna vigezo kama;
1. Awe mtanzania -NIDA/Mkazi etc
2. Alozaliwa bongo - Cheti cha kuzaliwa
345xxx Amesoma sekondari, Advance, Chuo Ameidhinishwa na bodi/baraza lao etc yoooooote hayo.

...... halafu ndio inakuja amefaulu mchujo, halafu ndio amejieleza vema kwenye mahojiano. Bado tu.

Jameni hata kama tunakubaliana kuwa mtihani sio njia pekee ya kupima utoshaji wa mtu, ni lazima tukubaliane kuwa hiyo nayo ni njia mojawapo yaani ni HATUA KATIKA UELEKEO SAHIHI
 
Yan daktari nakosa kazi eti kisa sijajibu vizuri nilipoulizwa tell us about yourself au sijajibu vzr mtihani wenye topic za physics za olevel duh
Kwahy unalalamikia utumishi au?
Hilo n kosa lako mwnyw huna wa kumpa lawama zako
 
Back
Top Bottom