KJ07
JF-Expert Member
- Dec 17, 2021
- 2,370
- 5,381
Salaam Wakuu,
Katika pitapita zangu za hapa na palehuko mjini instagram nimekutana na mdada mmoja ambaye ameni inspire sana kutokana na kitu alichoamua kufanya kwa jamii ya watanzania. Jina lake halisi sijalifahamu bado ika la instagram ni Mentor_Cherry.
Sasa kwa harakaharaka nimegundua kuwa ni muathirika wa VVU na ameamua kuliweka wazi hilo mbele ya jamii na nadhani ni kwa ajili ya kuongeza uelewa kwa jamii hasa juu ya masuala yanayohusu VVU.
Miongoni mwa post zake kuna ambayo anatoa taarifa juu ya uwepo wa tabia ya manesi (CTC) ya kuwanyanyapaa waathirika wa VVU wanapoenda kuchukua madawa ya kupunguza makali ya VVU. Video zake nyingi zina contents hizo na shuhuda mbalimbali za watu wakimtaja kama mtu aliyewabadilisha kimtazamo hasa waathirika wa VVU.
Pia nimeona post moja akiwashauri wadada wa vyuoni kuacha kujirahisisha kwa wababa kisa pesa na mwisho wa siku wanaingiliwa kinyume na maumbile jambo ambalo linachangia maambikizi ya VVU kwa kiasi kikubwa.
Natamani tuwe na watu wengi kama yeye ambao wanachukulia changamoto za kiafya in a positive way ili kupunguza athari zitokanazo na hofu ya magonjwa.
Ni hayo tu wakuu wa JF.
Hii ni moja ya post zake ambayo imeniinspire sana.