Pongezi kwa Serikali kwa aina hii ya ukusanyaji kodi isiyokwepeka

Pongezi kwa Serikali kwa aina hii ya ukusanyaji kodi isiyokwepeka

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
609
Reaction score
604
Nawasalimu ndugu watantania kwa jila la JMT

Wiki kadhaa zilizopita walijitokeza watu wakimnanga mkuu wa nchi kwamba kwa anayoyafanya ya kulegeza kamba kwenye ukusanyaji kodi kwa kutotumia nguvu ni kujiingiza kwenye anguko la kitaifa kwani hakuna mtu anapenda kulipa kodi hivyo kama hakuna nguvu ya ziada basi serikali itapoteza makusanyo yake kwa kiasi kikubwa.

Watu wale wale nawaona leo hii 15/07/2021 wakilalama baada ya Mkuu wa Nchi kutumia akili badala ya nguvu katika kukusanya kodi ambayo haiwezekani kuikwepa au kufanya hila yeyote ya ujanja. Kodi hii iliyowekwa kwenye miamala ni kodi mujarrab sana kwa wote na sio ya kinyonyaji na wala sio kandamizi. Kodi hii analipa mwananchi wa pato la chini hadi wa pato la juu.

Wanalipa watawala hadi watawaliwa. Na hamna task force inayotumika kukusanya kodi hii kwa maana ni kodi ya kiuchumi (economic). Raisi mwenyewe akifanya mwamala wa simu analipa kodi hii, Waziri Mkuu, Spika, Mawaziri na Wabunge wote wanalipa hii kodi kila wanapofanya muamala wa kifedha kwa njia ya simu.

Naipongeza sana serikali kwa hili, hakika akili kubwa imetumika.

Waliokua wanaombea anguko la serikali ktk ukusanyaji wa kodi sasa wamebaki wameduwaa! Hawaamini yanayotokea! Kazi Iendelee.
 
hii kodi ni nzuri sana yaani haina ukwepaji wala ubabaishaji.

sasa najipa uhalali wa kudai elimu bora, hospitali, barabara n.k

Ahsante Serikali yetu kwa ubunifu.

kamwe asiyumbishwe na wanasiasa wahuni wasio itakia mema nchi yetu.
 
Back
Top Bottom