njwanjwanjwa
Member
- Jul 28, 2022
- 8
- 11
Mapema wiki hii inayoishia, nimefurahi sana kuona Serikali ikigawa bure kwa walimu wa VETA vishikwambi ( tablette) vilivyokuwa vinatumika ktika zoezi la Sensa la mwezi Agasti.
Baada ya zoezi la Sensa kutamatika, Serikali hii tukufu ya Mama Samia iliahidi kugawa vishikwambi vilivyokuwa vikitumika kwa watumishi wa sekta ya Elimu kuanzia vyuo vikuu, vyuo vya kati na hatimae kwa walimu na maofisa wa Elimu sekonsari na msingi.
Nilipoona wakufunzi wa chuo cha ufundi cha Veta iliyokaribu na mimi wamepatiwa vishikwambi, nikajisemea moyoni kuwa basi…hata yule mwaliku wa shule ya Msingi Namtumbo kule Songea nae anaenda kumilikishwa na Serikali mishikwambi muda si mrefu.
Aidha, binafsi hili ni jambo la kupongezwa sana tena sana kwa Serikali si tu kwa kuwakumbuka walimu na kuwapa bishikwambi vilivyokuwa vikitumika wakati wa Sensa la hasha! Bali kuwawezesha nyenzo ya kufundishia kisasa kwa kuendana na mabadiriko ya kasi ya sayansi na Teknologia.
Mimi kama Mwalimu wa Taifa hili pendwa, nasema Asante sana Serikali yangu kwa hili🙏