Pongezi kwa uongozi wa wafanyabiashara wa kariakoo,

Pongezi kwa uongozi wa wafanyabiashara wa kariakoo,

Risk vs Return

Senior Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
106
Reaction score
71

Wakuu wote wa janvi hili salamu zenu, Napenda kuwapa Hongera Hongera Sana kwa wafanyabiashara wote na hasa hao viongozi wao kwa kuweza kuonyesha dhahiri hisia zao kwa TRA jambo ambalo hapo nyuma lilikuwa halijawahi tokea kwa uwelewa wangu, hii ni dalili za kukuwa kwa fikra na uwelewa wa wafanyabiashara wetu sasa pia ni kukua kwa uhuru.
Cha kushangaza badala TRA kulipokea swala hili kwa nia njema kama njia iliobora ya kuwarahisishia upatikanaji wa kodi kwani sasa wamepata wadau wa kushilikiana nao bega kwa bega ilikutatua changamoto zilizopo na kufikia malengo ya kila mdau, hao wanaendelea kama walivyozoea kutisha wafanyabiashara na mabango /matangazo yaliojaa vitisho vingi nawakumbusha hakuna mwenye nguvu Zaidi ya mwananchi mwenyewe akiamua.
Wakati watu wakilalamika kuhusu mfumo wa kulipa kodi unavyowasumbua, unavyowaumiza, ulivyowadharirisha, unavyowanyanyasa, usivyojali maslahi yao na wakati mwingine tatizo sio ukubwa wa kodi wafanyabiashara wengi tu wakiulizwa wanadai kwa kuwa TRA hatuna uhakika na kodi zao zisizoisha inatubidi kukataa au kupinga kila wanachokudai kwa sababu hujui kesho watakuja na lipi tena la sivyo kama kungekuwa na Imani tuko tayari kulipa hata mara mbili Zaidi.
TRA kama walivyo zoea ni kutoa sheria kila kukicha (bila kuwashilikisha wadau husika) kwa wafanyabiashara zikiambatana na VITISHO vingi na watu kulipiswa faini kwa nguvu na RUSHWA kwa wingi sana wakifilisi wajasiriamali wazawa hatimaye wanatangaza wazi kuwa wamavuka malengo kwa Faini na Rushwa bila kujali ni wangapi wamefilisiwa na kufungunga biashara.
WAKATI UMEWADIA: Nadhani wakati umewadia wafanyabiashara wa Tanzania wapate watetezi katika vyombo vyote husika Bungeni, Selikarini, wakiwa wadau wakuu wa maendeleo yeyote ya kiuchumi katika nchi yeyote (ETI NDIO INJINI YA MAENDELEO KIUCHUMI) inabidi wapewe fursa ya kutosha katika kuzitunga hizo sharia husika BUNGENI pia vilevile wahusishwe katika utekerezaji wake bila kuleta madhara kwa wadau wake.
TRA WABADILI FIKRA ZAO: Kila mfanyabiashara kwa TRA anaonekana kama mwizi wa kodi (hata mwizi wa kuku ananafuu sana), afisa wa TRA anapokuja dukani kwako chochote atakachoona hakikukaa vizuri basi kwake yeye lengo ni kuiba kodi tu kinachofuata ni vitu viwili VITISHO VINGI SANA, FAINI ZA MAMILION, NA RUSHWA NYINGI SANA, ikibidi ukipona kiafya yaani wakikuacha unapumua basi biashara lazima utafunga na ukifuatilia chanzo cha tatizo ni kutokuelewa tu au ukosefu wa elimu ya kodi, TRA hakuna kitu onyo usirudie, wala wakuelimishe then waje wathibitishe kama kweli ulikuwa na nia mbaya..
MAPUNGUFU YA MFUMO WA TRA NI GHARAMA ZA MLIPA KODI:
Kwa wale wanaotumia mashine za VAT, ikitokea wakati wa kutoa risiti hakuna mtandao kwa nia nzuri tu ili ulipe kodi ukaandika risiti ya kitabu wanachokijua utapigwa utaambiwa faini sh 8,000,000 hapo utakuwa mhanga wa kuwabembeleza hatimaye faini ya serikali sh 3 mln na yao 3 mln vinginevyo unaambiwa kama hakuna mtandao uandike barua uipeleke ofisi ya TRA wakugongee mhuri ndio umpe mteja wako aondoke nayo kwa maana km ofisi ya TRA iko km 4 kila utakapouza kilo chupi ya motto unakenda TRA na barua mteja akisubiri, na pia huwezi jua ni wakati gani mtandao utakuwepo au la..
Kwa wale VAT wakati wa return kuto taarifa za biashara kila mwezi, zamani ilikuwa unajaza form kwa mkono unawapelekea haikuwa na usumbufu, wakabadili kutumia email wakalazimisha wafanyabiashara kununua makompyuta ili wawapelekee wanaweka program yao kwa siri sana na ndio unayoitumia kutuma email, kwanza HAKUNA MAFUNZO yeyote watu wamehangaika na vitisho vya faini ukichelewa watu hawakulala usiku wakituma haziendi network yao dhaifu,, hakuna feedback kuhakikisha kuwa imepokelewa au la pia baada ya muda miezi kadhaa wanakuja wakidadi hawana report zako na malimbikizo kibao ya penalty, faini kibao, sharia za kupandana zote zikitishia kufa biashara yako pia hata wewe mwenyewe Hatimaye rushwa na faini.
KUTOELEWA , UJINGA WAKO NDIO RUSHWA NA KODI TRA(auditing):
Pana wakati wanajua kabisa wafanyabiashara swala Fulani hawalielewi wao wana kaa kimya inapita muda wa kutosha kama miaka kama 3 hivi, then wana zua kitu wanaita ukaguzi (AUDITING)
Lengo kuu hapa kukusanya pesa wafikie malengo yao binafsi na TRA pia, hakuna kukuelimisha hapa, wala kukuonya hapa fikiria shughuli za biashara za miaka 3, hata kama ulipitiwa jibu rushwa na faini iliyo na malimbikizo, una kuta mtaji wako ni milioni 40 wana piga kodi wao wenyewe na hawataki mtu mwingine wanakuambia UNADAIWA KODI YA SH 320 MILLION. BADO HUJAFA TU.. NI HERI UKUTANE NA JAMBAZI MSITUNI KULIKO TRA.. kumbuka wewe huna elimu ya kupingana nao pia wewe kazi yako ni biashara kumhudumia mteja wako utafanya kazi ya kuwahudumia TRA utakula wapi ? ?

Inaendelea nikipata muda . . . .
 
sawa, lakini napingana na wewe na wafanyabiashara wenzio Kuwa hamtutendei haki wananchi wenzenu ka kutokulipa kodi kwa serikali, japo kuna mapungufu TRA lakini mnapaswa kuliangalia hilo la ulipaji wa kodi.

Hebu jiulize kwanini waajiriwa wote walipe kodi kwanini nanyi msilipe!?

Hebu kuweni na huruma na watanzania wenzenu.....
 
Kodi zenyewe hazifanyi kazi Bali zinaingia kwenye mifuko ya wabi he na raisi
 
sawa, lakini napingana na wewe na wafanyabiashara wenzio Kuwa hamtutendei haki wananchi wenzenu ka kutokulipa kodi kwa serikali, japo kuna mapungufu TRA lakini mnapaswa kuliangalia hilo la ulipaji wa kodi.

Hebu jiulize kwanini waajiriwa wote walipe kodi kwanini nanyi msilipe!?

Hebu kuweni na huruma na watanzania wenzenu.....

Shukrani mkuu kwa maoni yako, kodi zote stahiki tunalipa kila mwezi na kila mwaka bila kukosa pamoja na vitisho vyote hivyo na rushwa nyingi tu, kama umenielewa TATIZO sio kulipa kodi tatizo ni mazingira ya mfanyabiashara ya kulipa kodi, Unyanyasaji, mfumo isiyo na tija hata kidogo iwe kwa mlipa kodi pia kwa serikali, Udhalilishaji wa TRA, Adhabu kubwa sana za faini na rushwa hata kwa kosa la kibinadamu la kukanya tu na kuonya, na pengine ni kosa la TRA wao wenyewe, sisi tunasema mazingira ya mlipa kodi yakiwa rafiki tutalipa hata mara mbili ya hapo.

Ndg yangu ukifuatilia mapato ya TRA kwa wafanyabiashara sehemu kubwa sio kodi halisi itokanayo na mapato ya biashara husika ni kukusanya penalty na faini za adhabu mbalimbali ikiwa chanjo chake kikuu upungufu wa uelewa/elimu, mfumo mbovu, kumbukumbu dhaifu JE SIO KUUWA UJASIRIAMALI NA BIASHARA HASA KWA WAZAWA ?

Mwisho ndg yangu kama kweli sisi tunafaidi kwa kutolipa kodi TUNAKUKARIBISHA SANA UJE na wewe ufaidi kwa kufungua tu biashara yeyote upendayo, huna haja ya kuandika barua kama ya kuomba kazi karibu sana mkuu uionje joto ya jiwe..
 
Poleni sana wafanyabiashara eti wanawaletea mashine za kuhesabu mauzo yenu tu je wao wajuaje gharama zenu na matumizi yenu hadi kupata yao mauzo ? TRA wangekuwa waungwana hizo mashine zao zihesabu vitu vyote hadi kupata faida au hasara halisi, yaani mashine iweze kuhesabu manunuzi, matumizi, gharama za biashara na mwisho mauzo yake ndio sasa kodi halisi itapatikana.
 
Back
Top Bottom