inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 20,344
- 21,967
Mi mkulima,navuna gunia mia n ne kwa mwaka za mpunga na mahindi,Sina njaaHawashibi hao kama sio wanashimdia mihogo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi mkulima,navuna gunia mia n ne kwa mwaka za mpunga na mahindi,Sina njaaHawashibi hao kama sio wanashimdia mihogo.
Dini za kizazi cha Abraham ni mbili tu, sijui wewe hiyo ya tatu umeipatia wapiHija ya Waisrael unafahamu ni dini tatu za kizazi cha Abraham hapo hapo sehemu moja, wanapishana milango tu.
Majini mbwenduko yatabisha huu ukweli acha ukweli ubaki ukweli
Waarabu ndiyo wapalestina ambao eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.Watu wengi huzihusisha dini kwenye mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.
Israel ni nchi moja inayokaliwa na watu ambao hawajakubaliana kuishi pamoja, wayahudi na waarabu.
Waarabu ndiyo wapalestina ambao eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.
View attachment 2779426
Kuna sehemu mbili za waarabu.
1. Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako kunatawaliwa na chama cha Fatah.
2. Ukanda wa Gaza ambako kunatawaliwa na kikundi cha Hamas.
Sehemu hizi mbili ndizo zinazounda mamlaka ya Palestina ambayo Rais wake ni Mahmoud Abbas, mwenyekiti wa chama cha Fatah.
Sehemu yenye machafuko yanayoendelea sasa ni ukanda wa Gaza.
Hili ni eneo dogo la kilomita za mraba 365, yaani ni karibu sawa na wilaya ya Ilala yenye kilomita za mraba 364.9.
Lakini licha ya udogo wake, eneo hili la lina watu zaidi ya milioni mbili waliobanana vibaya.
Asilimia kubwa ya watu hawa ni vijana wasio na ajira ambao maisha yao yote wamekuwa wakishuhudia machafuko ya umwagaji damu.
Watu hawa hawaogopi chochote kuhusu vita, huku ndiko inakotoka Hamas, yaani kikundi cha harakati za ukombozi cha kiislamu (Ḥarakah al-Muqāwamah al-ʾIslāmiyyah).
Hamas ni kikundi ambacho kimechagua vita kama njia yao ya kutafuta ukombozi kutoka Israel.
Hii ni tofauti na vikundi vingine kama Fatah, PLO na PLMA ambavyo viko tayari kwa mazungumzo na Israel kupata muafaka wa kudumu.
ASILI YA MGOGORO
Watu wengi huuhusisha na udini mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.
Kujua asili ya mgogoro huu inabidi kurudi nyuma miaka zaidi ya 3000.
Picha inaanzia mwaka 63 kabla ya kuzaliwa Kristu pale dola ya warumi ilipoivamia nchi ya wayahudi na kuitawala kama wakoloni.
Wakamtoa mfalme wa wayahudi, Hasmonean na kumuweka Herod madarakani.
Wayahudi hawakukubali kutawaliwa hivyo wakapigana vita kadhaa za kutafuta uhuru.
Mwaka 165 baada ya kuzaliwa Kristu, vita kali ilizuka lakini wayahudi wakashindwa tena.
Baada ya vita hii warumi wakaamua kuwafukuza wayahudi kutoka nchi yao.
Wakaibadilisha jina nchi hiyo na kuiita Palestina.
Hili ni neno la kigiriki ambalo maana yake ni 'vunja kabisa uhusiano kati ya wayahudi na ardhi yao'.
Wayahudi wakasambaa Ulaya yote ambayo ilikuwa chini ya Warumi, na hawakutakiwa tena kurudi.
Hiki kilikuwa kipindi ambacho ukristu ulikuwa unaanza kushamiri lakini warumi waliupiga vita.
Kuwa mkristu ilikuwa kosa kubwa sana ndani ya himaya ya warumi hadi karne ya nne pale mtawala wa warumi, Constantine alipoupokea.
Akausambaza katika himaya yote aliyoitawala na kuufanya ukristu kuwa dini rasmi ya warumi.
Hii ilimaanisha kwamba sasa wazungu wataanza kujifunza ukristu na katika kujifunza wakagundua kwamba kumbe wayahudi ndiyo walimuua Yesu.
Wakawachukia na kuanza kuwaua kila walipokuwepo.
Karne kadhaa baadaye himaya ya warumi ikaanguka na nchi ya Palestina pamoja na eneo lote la Mashariki ya Kati likaangukia chini ya tawala kadhaa za kiislamu za waarabu. Hapo ndipo Palestina ikakaliwa na waarabu.
Utawala wa mwisho wa kiislamu ukawa wa himaya ya Ottoman, ambayo ilianguka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.
Ottoman ilipigana vita ya dunia upande wa Ujerumani, baada ya kushindwa, ikanyang'anywa makoloni yake yote kama adhabu, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani ambayo ilinyang'anywa hadi nchi yetu.
Hapo ndipo Palestina ikaangukia kwa wakoloni wapya, waingereza.
Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, zilioitwa Zionism.
Harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina.
Hii ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi pale na wayahudi waliokuwa wakirudi.
Vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.
Nchini Ujerumani ikiwa inaongozwa na Hittler, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kinyama (Holocaust), Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.
Kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka.
Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.
Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.
Ramani inahusika.
View attachment 2778309
Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.
Itaendelea...
Marekebisho; Wakati huo Israel haikuwepo isipokuwa wazee wao walijulikana kama Waebrania, wakitokea Uru ya Wakaldayo maeneo ya Irak/Iran jirani na Syria.Kwa wakat huo, Waisraeli walikuwa wanaishi wap
Ongezea Hebrew historyNenda Israel kahiji, wataanza kukutembeza kuanzia Western/Wailing Wall. Kwa msaada zaidi unaweza kumtafuta Job Ndugai akuelekeze. Vitabu vya Historia anza kusoma Israel and the Nations; F.F Bruce, David F Payne.
Amenambia wikipedia:Dini za kizazi cha Abraham ni mbili tu, sijui wewe hiyo ya tatu umeipatia wapi
Wikipedia sio rejea madhubuti kwa watu makini na masuala complex.Amenambia wikipedia:
The Abrahamic religions are a group of religions, most notably Judaism, Christianity and Islam, centered around the worship of the God of Abraham. Abraham, a Hebrew patriarch, is extensively mentioned in the religious scriptures of the Hebrew and Christian Bibles, and the Quran.[1]
![]()
Abrahamic religions - Wikipedia
en.wikipedia.org
Hivi hizo shule mlienda kusoma ujinga?
Just to be clear:
Before Israel, there was a British mandate, not a Palestinian state.
-Before the British Mandate, there was the Ottoman Empire, not a Palestinian state.
-Before the Ottoman Empire, there was the Islamic state of the Mamluks of Egypt, not a Palestinian state.
-Before the Islamic state of the Mamluks of Egypt, there was the Ayubid Empire, not a Palestinian state. Godfrey IV of Boulogne, known as Godfrey de Bouillon, conqueror of Jerusalem in 1099
-Before the Ayubid Empire, there was the Frankish and Christian Kingdom of Jerusalem, not a Palestinian state.
-Before the Kingdom of Jerusalem, there was the Umayyad and Fatimid empires, not a Palestinian state.
-Before the Umayyad and Fatimid empires, there was the Byzantine empire, not a Palestinian state.
-Before the Byzantine Empire, there were the Sassanids, not a Palestinian state.
-Before the Sassanid Empire, there was the Byzantine Empire, not a Palestinian state.
-Before the Byzantine Empire, there was the Roman Empire, not a Palestinian state.
-Before the Roman Empire, there was the Hasmonean state, not a Palestinian state.
-Before the Hasmonean state, there was the Seleucid, not a Palestinian state.
-Before the Seleucid empire, there was the empire of Alexander the Great, not a Palestinian state.
-Before the empire of Alexander the Great, there was the Persian empire, not a Palestinian state.
-Before the Persian Empire, there was the Babylonian Empire, not a Palestinian state.
-Before the Babylonian Empire, there were the Kingdoms of Israel and Judah, not a Palestinian state.
-Before the Kingdoms of Israel and Judah, there was the Kingdom of Israel, not a Palestinian state.
-Before the kingdom of Israel, there was the theocracy of the twelve tribes of Israel, not a Palestinian state.
-Before the theocracy of the twelve tribes of Israel, there was an agglomeration of independent Canaanite city-kingdoms, not a Palestinian statehood.
Actually, in this piece of land there has been everything, EXCEPT A PALESTINIAN STATE!
Mbona kuna mtume mmoja ya ile dini ya waabudu mwezi na nyota alioa binti wa miaka 9. Huyo binti alikuwa amevunja ungo?Acha kukaza hicho kichwa mzee wangu, Yesu aliishi karne ipi na netanyau yupo karne ipi.?
Ww n msukuma kwa sababu baba ako n msukuma lkn mbona ww sio Mmasai kwa sababu mama ako n Mmasai.?
Zamani watoto wakike wanavunja ungo wakiwa na miaka 12 ila sasa hv ht 9 tayari, hy inatokana na life style pamoja na sababu za kimazingira.
Pia kuna kuchangamana na watu tofauti tofauti zinapelekea watu kubadilika.
Mambo hayo n simple sana kuelewa ukiamua kufungua akili ili uelewe
Wakuu mmekazana na hy kuvunja ungo, yn point zingine zote hamzioni zaidi ya hy 😂 au na nyie tayari.?Mbona kuna mtume mmoja ya ile dini ya waabudu mwezi na nyota alioa binti wa miaka 9. Huyo binti alikuwa hajavunja ungo?
Bado haujaongea vizuri. Kipindi hao wapelestina wanavamia waisrael na kuwaua kwenye tamasha hakuongea.Wakristo wanatumia nguvu kubwa mno mno kuongea uongo, why? Ila naamini kabisa mnaujua ukweli ila chuki zimewajaa vifuani mwenu dhidi ya waarabu na waislamu kwa ujumla
Katika hii page ni mkristo mmoja tu ameongea ukweli na kuweka kando unafiki, ubarikiwe sana mkuu Dannion
On that day the Lord made a covenant with Abram and said, "To your descendants I give this land, from the Wadi of Egypt to the great river, the Euphrates – the land of the Kenites, Kenizzites, Kadmonites, Hittites, Perizzites, Rephaites, Amorites, Canaanites, Girgashites and Jebusites."
Karibia Mashariki ya kati yote na Afrika. Ukisoma historia waliwepo ambazo leo zinaiwa "Syria, Jordan, Egypt, Saudi Arabia, Iraq, Iran, Yemen, Ethiopia, Morocco. Wengine mpaka leo wapo Yemen, Iran, Ethiopia, Morocco na nchi zingine nyingi.
Wachaga pia wana asili ya kiyahudi.
na kama walitokea middle east kabla ya kusambaa huko ulaya kwa nini wanaonekana kama hawana haki ya kuwepo hapo middle east kwa sasa?naona unarukaruka tu mama...haiwezekani origin ya hao jamaa iwe nchi zote hizo,,,,huko labda walisambaa tu lakini kimsingi lazima wawe na sehemu yao ya asili, na hapo ndo watu wanashindwa kuwaelewa.
Umeambiwa maana ya wapalestina ni tofauti na wafilisti pia native filistian sio hao waarabu. Hili andiko mbona limeshiba sana na lina jikamilosha kwa kila jambo.Mawazo yako ni kama yangu niliochangia sehemu flan kuhusu chanzo cha mgogoro. Watu wengi hawaanzii mwanzo wa mgogoro. Wao wanaanzia Israeli kashaingia Kanaani na kuvamiwa na warumi kisha wapalestina wakachukua ardhi yao. Sijui ni maksudi au wanasahau.
Kingine ambacho sijui, hawa wapalestina ndo wale wafilisti wa mwanzo au hawa ni wengine? Na kama sio, wafilisti wa kale masalia yao ni akina nani wa sasa?
Vema mkuu.Watu wengi huzihusisha dini kwenye mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.
Israel ni nchi moja inayokaliwa na watu ambao hawajakubaliana kuishi pamoja, wayahudi na waarabu.
Waarabu ndiyo wapalestina ambao eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.
View attachment 2779426
Kuna sehemu mbili za waarabu.
1. Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako kunatawaliwa na chama cha Fatah.
2. Ukanda wa Gaza ambako kunatawaliwa na kikundi cha Hamas.
Sehemu hizi mbili ndizo zinazounda mamlaka ya Palestina ambayo Rais wake ni Mahmoud Abbas, mwenyekiti wa chama cha Fatah.
Sehemu yenye machafuko yanayoendelea sasa ni ukanda wa Gaza.
Hili ni eneo dogo la kilomita za mraba 365, yaani ni karibu sawa na wilaya ya Ilala yenye kilomita za mraba 364.9.
Lakini licha ya udogo wake, eneo hili la lina watu zaidi ya milioni mbili waliobanana vibaya.
Asilimia kubwa ya watu hawa ni vijana wasio na ajira ambao maisha yao yote wamekuwa wakishuhudia machafuko ya umwagaji damu.
Watu hawa hawaogopi chochote kuhusu vita, huku ndiko inakotoka Hamas, yaani kikundi cha harakati za ukombozi cha kiislamu (Ḥarakah al-Muqāwamah al-ʾIslāmiyyah).
Hamas ni kikundi ambacho kimechagua vita kama njia yao ya kutafuta ukombozi kutoka Israel.
Hii ni tofauti na vikundi vingine kama Fatah, PLO na PLMA ambavyo viko tayari kwa mazungumzo na Israel kupata muafaka wa kudumu.
ASILI YA MGOGORO
Watu wengi huuhusisha na udini mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.
Kujua asili ya mgogoro huu inabidi kurudi nyuma miaka zaidi ya 3000.
Picha inaanzia mwaka 63 kabla ya kuzaliwa Kristu pale dola ya warumi ilipoivamia nchi ya wayahudi na kuitawala kama wakoloni.
Wakamtoa mfalme wa wayahudi, Hasmonean na kumuweka Herod madarakani.
Wayahudi hawakukubali kutawaliwa hivyo wakapigana vita kadhaa za kutafuta uhuru.
Mwaka 165 baada ya kuzaliwa Kristu, vita kali ilizuka lakini wayahudi wakashindwa tena.
Baada ya vita hii warumi wakaamua kuwafukuza wayahudi kutoka nchi yao.
Wakaibadilisha jina nchi hiyo na kuiita Palestina.
Hili ni neno la kigiriki ambalo maana yake ni 'vunja kabisa uhusiano kati ya wayahudi na ardhi yao'.
Wayahudi wakasambaa Ulaya yote ambayo ilikuwa chini ya Warumi, na hawakutakiwa tena kurudi.
Hiki kilikuwa kipindi ambacho ukristu ulikuwa unaanza kushamiri lakini warumi waliupiga vita.
Kuwa mkristu ilikuwa kosa kubwa sana ndani ya himaya ya warumi hadi karne ya nne pale mtawala wa warumi, Constantine alipoupokea.
Akausambaza katika himaya yote aliyoitawala na kuufanya ukristu kuwa dini rasmi ya warumi.
Hii ilimaanisha kwamba sasa wazungu wataanza kujifunza ukristu na katika kujifunza wakagundua kwamba kumbe wayahudi ndiyo walimuua Yesu.
Wakawachukia na kuanza kuwaua kila walipokuwepo.
Karne kadhaa baadaye himaya ya warumi ikaanguka na nchi ya Palestina pamoja na eneo lote la Mashariki ya Kati likaangukia chini ya tawala kadhaa za kiislamu za waarabu. Hapo ndipo Palestina ikakaliwa na waarabu.
Utawala wa mwisho wa kiislamu ukawa wa himaya ya Ottoman, ambayo ilianguka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.
Ottoman ilipigana vita ya dunia upande wa Ujerumani, baada ya kushindwa, ikanyang'anywa makoloni yake yote kama adhabu, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani ambayo ilinyang'anywa hadi nchi yetu.
Hapo ndipo Palestina ikaangukia kwa wakoloni wapya, waingereza.
Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, zilioitwa Zionism.
Harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina.
Hii ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi pale na wayahudi waliokuwa wakirudi.
Vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.
Nchini Ujerumani ikiwa inaongozwa na Hittler, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kinyama (Holocaust), Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.
Kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka.
Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.
Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.
"ramani ya pendekezo la umoja wa mataifa mwaka 1947 kuigawa ardhi ili kuwe na mataifa mawili"
View attachment 2779883
Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.
Kabla ya kuendelea kwanza nikupitishe kwenye historia ya kiutawala ya nchi hiyo tangu kuingia kwa warumi, miaka zaidi ya 3000 iliyopita.
1. WARUMI
Wakati wa utawala wa warumi kwenye nchi yao, dini ya wazawa ilikuwa moja tu, uyahudi, baadaye mnamo karne ya kwanza ikazaliwa dini mpya kutoka uyahudi ambayo ilianza kama tawi la uyahudi na baadaye ikaitwa dini kamili, Ukristo.
Warumi walikuwa na dini zao za kipagani na waliwalazimisha wayahudi na wakristo kuzifuata.,waliweka sheria kwamba lazima wayahudi na wakristo watoe sadaka kwa miungu ya kirumi na masanamu, baadaye wayahudi wakaondolewa ulazima huo kwa fidia ya malipo maalumu yaliyoitwa Fiscus Judaicus yaani Kodi ya Wayahudi.
Lakini wakristo hawakupewa hiyo nafasi, badala yake walitakiwa kutekeleza tu sheria ya sadaka kwa miungu ya kirumi, warumi hawakuupenda kabisa ukristo na ilikuwa kosa kisheria kuwa mkristu, ndiyo maana waliwalazimisha kufanya ibada za kipagani.
Ilipofika karne ya pili, ndipo wayahudi wakaanzisha vita kubwa ya kudai uhuru, kwa hasira warumi wakawafukuza kabisa wayahudi katika nchi yao na kuibadili jina na kuwa Palestina, wakaweka marufuku kwa wayahudi kurudi katika nchi ya Palestina.
Mnamo karne ya nne, mtawala wa warumi, Constantine, akaupokea ukristo na kuufanya kuwa dini kuu ya warumi, hii ni baada ya kuona kwamba ukristo ulikuwa unakuwa kwa kasi na hata yeye alibadili dini kuwa mkristo, lakini pia alitaka kuitunza amani ya nchi kwa kuondoa ukandamizaji wa kundi linalokuwa kwa kasi.
Ukristo uliposambaa ulaya kulikuwa na chuki dhidi wa wayahudi (Anti-Semitism), sababu kuu zilikuwa ni kwamba wayahudi walionekana wauaji wa Yesu Kristo na dini yao haimtambui Yesu. Matukio kadhaa yakiwemo mauaji yalifanyika kwa wayahudi, Kusambaa kwa elimu ya dini ndiko kulisaidia kujua kwamba hata alieamuru kusulubiwa kwa Yesu hakuwa Myahudi bali ni Pilato wa warumi ambao waliabudu masanamu kwa muda huo.2. DOLA ZA KIISLAMU
Mnamo karne ya sita dini mpya ilizaliwa kutoka makabila ya kiarabu, yakiongozwa na Mtume Muhammad (SAW). Muhammad hakuwa tu kiongozi wa kidini bali pia kisiasa, alizaliwa mji wa Maka na baadaye kuhamia mji wa Yathrib.
Alipohamia mji huu, wenyeji wakaubadili jina na kuuita Madinat Al Nabii yaani mji wa Nabii, ndipo mji huu ukaitwa Madina. Akiwa hapo Muhammad SAW akaanzisha taifa jipya la kislamu lililorudi na kuuteka mji wa Maka, alipofariki nafasi yake kisiasa ikarithiwa na Abu Bakr halafu akaja Umar au Omar.
Huyu Omar akaitanua nchi hadi kufika Palestina, chini ya tawala za kiislamu, mambo yakabadilika sana Palestina, Ile marufuku ya warumi juu ya wayahudi kurudi ikaondolewa...wayahudi wakaruhusiwa kurudi Palestina.
Waislam, wayahudi na wakristo wakaishi pamoja nchini Palestina chini ya utawala wa Omar.
Mji mkuu wa Jerusalem uliruhusu dini zote tatu, waislamu waliwaita wakristo na wayahudi DHIMMI, ambayo maana yake WATU WA KULINDWA, Waliwaita hivyo kwa sababu walikuwa Ahl Al Kitab yaani watu wa taifa la kitabu, kwenye kitabu cha waislam yaani Koran, wakristo na wayahudi wametajwa kwamba wamepewa kitabu na Mungu cha miongozo ya kumuabudu.3. CRUSADERS
Baada ya karne nyingi za kuwa chini ya tawala za kiislamu, wakristo wa Ulaya wakataka kuurudisha mji wa Jerusalem na nchi ya Palestina mikononi mwao, wakaanzisha harakati zilizoitwa CRUSADE, yaani vita vya msalaba, waliopigana vita hii waliitwa Crusaders, hii ilikuwa vita iliyopiganwa kwa miaka zaidi ya 200 kuanzia 1095 hadi 1291
IIianza mwaka 1095 baada ya kiongozi wa kanisa katoliki, Papa Urban II, kuitisha kongamano kuu la Clermont kuwataka watu wa Ulaya kutumia kila aina ya uwezo walionao kuuchukua mji mtakatifu wa Jerusalem kutoka kwa waislam, ulaya iliitikia wito huu na wafalme wake wakatuma jeshi kubwa lililoenda kuuteka mji huo na nchi yote ya Palestina, na miji mingine ya karibu.
Chini ya utawala wa Crusade, Palestina haikuwa tena mahala salama kwa wengine zaidi ya wakristo, waislam na wayahudi waliteswa na kuuawa, Hii ilipelekea ulazima waungane kupigana dhidi ya Crusaders.
Wakiongozwa na Sultan Saladin, wakafanikiwa kushinda na kuwapindua Crusaders.
Hata baada ya Papa Urban II kufariki, Mapapa wengine waliofuata waliendelea kutuma misafara mingine katika awamu saba zaidi na kufanya jumla kuwa na misafara nane ya Crusade ambazo zote hazikufanikiwa kuirejesha Palestina mikononi mwao, Wafalme kadhaa wa Ulaya waliamua kwenda wenyewe vitani kuongoza mapambano katika misafara tofauti mfano ukiwa ni Mfalme Richard The Lion Heart wa Uingereza aliongoza Crusade ya tatu lakini haikufanikiwa.4. SALADIN
Dola ya kiislam ilikuwa ikiangukia kwa watawala tofauti kulingana na koo zao, nao walihamisha makao makuu kupeleka walipopata au kwenye asili yao.
Kwa mfano, wakati wa Mtume Muhammad SAW, makao makuu yalikuwa Madina, Ali ibn Talib, alihamishia mjini Kufa katika nchi ambayo sasa ni Iraq, Umayyads watu wa Syria wakahamishia huko kwao makao makuu, Hali ilienda hivyo hadi dola ikawa chini ya Sultan Saladin aliyechukua madaraka kutokea Misri.
Chini ya Sultan Saladin,Waislam walijipanga na kuirudisha Palestina mikononi mwao.
Saladin hakulipa kisasi kwa wakristo bali aliwaruhusu waendelee kuishi na kufanya ibada zao bila tatizo lolote, Yeye ndiye aliyekabidhi kwa familia ya kiislamu ufunguo wa kanisa kuu la Holy Sepulchre ambapo wakristu wanaamini ndipo alipozakiwa Yesu, alipokufa na kuzikwa.5. OTTOMAN
Kutoka kwa Saladin, Palestina ikaangukia kwa utawala mwingine wa kiislam wa Ottoman, maisha yaliendelea kuwa ya pamoja kati ya dini zote tatu kubwa za eneo hilo.6. UINGEREZA
Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, himaya ya Ottoman ilianguka na Palestina ikaangukia kwa waingereza,
Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina lakini ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi na kutawala Palestina dhidi wayahudi waliokuwa wakirudi.
Vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.
Muda huo Ujerumani ikiwa inaongozwa na Dikteta Hittler, Kulifanyika mauaji ya kinyama (Holocaust) Wayahudi milioni 6 waliuwawa, wengi walipelekwa kambi za maalum za mauaji, walifungiwa kwenye kumbi kubwa kisha kufukizwa kwa gesi yenye sumu. Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.
Kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka, Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.
Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.
Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.
Kuanzia hapo ndipo machafuko yote ya sasa yanakuja ....
Itaendelea ....
Kwa hiyo Esau uzao wake ni wapalestina na wa Yakobo ndio wayahudiYalikaliwa na Esau na kizazi chake,kulwa wa Yakobo(Israel).Code:Wayahudi walivyokwenda utumwani Misri , nchi Yao ilikaliwa na Nani?
Kama haiwezekani basi ifute historia uandike yako. Utapata PhD kuja na kitu kipya, hayo niliyokufahamisha yapo mtandaoni wala usipate tabu kutafuta. Tumia google tu.na kama walitokea middle east kabla ya kusambaa huko ulaya kwa nini wanaonekana kama hawana haki ya kuwepo hapo middle east kwa sasa?
Unaeleweka sana tu mkuu ila watu wanajitoa ufahamu.Kwanza tujiulize ramani ya dunia ilichorwa mwaka gani.? Kwa vyovyote vile ramani ya Israel hauwezi kuwepo kwenye ramani ya dunia kwa sababu kwa muda huo ramani inachorwa hapakuwa na nchi ya Israel mana walisambaa duniani kote.
Ila kabla ya mchoro wa ramani ya dunia nchi ya Israel ilikuwepo.
Hvy baada ya vita vya pili vya dunia na Israel kupewa eneo bc ni lazima nchi yao ionekane kwenye ramani ya dunia.
Ni sawa na sasa hv Morogoro ikijitawala yenyew bc lazima ramani ya dunia ichorwe upya kuonyesha nchi ya Morogoro.
Umesema kweli kabisa,ilibidi kwa imani zetu tunazoziamini tuwaombee hawa watu amani iwepo.All in all tuweke Udini pembeni hawa ni watu kama sisi wanapaswa kuishi na kupata mahitaji ya msingi
Kwa dunia ilivyo sasa hakuna duru muhimu ya kuleta suluhisho kama kuongea baina ya pande mbili, msipoongea bado hamuwezi kuelewana
Nb; hatuwezi elewana kwa risasi na mabomu