kuna moja nilikuwa na date na alikuwa na 2 childs bac kila cku pesa nikawa nampiga calenda mpka kuna cku akanambia hiv ww kwa ubayili wako huu unapata Apple kweli nikacheka sanaaaa!!!hatari sana hao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka kula bila kuliwa hilo haliwezekani ndugu.


Heshima Kwa "Single Mother" Wote Amani iwe Juu yenu.

Niliwahi kutoka na "Single Mother" Mmoja, Mwanzoni alikuwa mgumu sana,huku akisema Wanaume wote hamfai,Waongo sana.

Hivyo ni kama nilikuwa namfaata tembo alijeruhiwa,Nilijaribu kumuweka sawa Palikuwa na taabu,Muda mwingi anazungumzia Jamaa yake aliyemkacha na lawama kibao utadhani Mahakamani.

Mimi moja ya falsafa yangu siwekezi muda Mwingi na nguvu nyingi kuongelea historia ya nyuma,Tunagusa kidogo tena kwa idhini yako au udadisi wako na sio wangu,kisha tunasonga mbele kwa kasi.

Pesa ndogo ndogo wataiatia.

Penzi bila pesa karne hii usawa huu,Penzi litakwenda Mwendo wa Kobe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji15][emoji15][emoji15] ngoja waje pm mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very true
 
GREAT ARTICLE INDEED. BUT LET ME PUT IT CLEAR THAT HAVING CHILDREN WHILE THE PARENTS ARE NOT IN A MARRIAGE IS A CURSE. ANYONE CAN DO THEIR ON RESEARCH ON THIS, IN FACT THOSE CHILDREN ARE KNOWN AS "BASTARDS". IT'S A DISGRACE EVEN TO OUR SOCIETIES. PERSONALLY I SUPPORT SINGLE MOTHERS WHO ARE OR WHERE BEFORE ALREADY IN A MARRIAGE.
 
Hivi pacha wangu huyuhuyu ndo alianzisha hili lisiredi?
 
Fundichupi uko wapi aisee nataka unishonee chupi
 
Huo ndio u selfish ambao akina mzabzab wanausema....unajali matakwa yako tu, vipi haki ya mtoto kulelewa na baba na mama?
Sasa inafikaga wakati umri unaenda na haupo na mwanaume wa kueleweka..ndo tuseme ubaki bila mtoto eti kisa ukizaa atakosa malezi ya baba?

Mm mwenye apa bado naangalia upepo tuu ela ikisimama vzuri na nikianza nusa 30 basi ntazaa tuu yann kusubiri ndoa na 30+ imekufika. all in all hakuna mwanamke anaependa kulea mtoto peke ake.
 
Habarini wana jamvi.

Juzi kati ( kabla ya Eid) nilikuwa natoka zangu sokoni kutafuta zaga za Eid el Hajj nakaribia kwangu kuna mdada wa hapa kitaa ninapoishi akanisimamisha na mm nikasimama kumsikiliza kunani, dada kaumbika masha Allah yaani ana mkia wa maana japo sura ya baba. Basi yule mdada kwa upole wa hali ya juu akanisalimia na kunitaka radhi kwa kunisimamisha nikamwambia uwe na Amani.

Chakushangaza yule dada bila kupindisha maneno akaniambia najuwa hali imekuwa ngumu sana kwa kila mtu lakini amini kaka hali yangu ni mbaya zaidi. Mimi ni mjane na nina watoto watatu najitahidi kutafuta rizki ya halali ila kwa hii siku kuu hali imekuwa mbaya zaidi. Nakuomba kaka yangu nisaidie chochote watoto wangu wafurahi hata kwa hii siku moja. Kilichoniuma aliniambia nipo tayari kwa lolote kaka ilimradi watoto wangu wafurahi kama watoto wengine. Nilijikaza kiume lakini bado kidogo tu nitokwe na machozi mbele ya yule mdada.

Niliamua kurudi tena sokoni na yule dada nikamwambia chagua unachotaka dada, alikua muoga wa kuagiza nikaamua niseme mm nilimnunulia mchele wa basmat kilo tano, vitunguu, mbatata, nyanya, kiufupi zaga zote za jikoni na baadae nikampa laki na hamsini imsaidie. Alinishukuru huyo mdada yaani hadi nilihisi kama anakufuru na akaamua kunipa number ya sim ila nilikataa. Maneno yake yalinifanya niwaze siku nikifa ghafla mke wangu ataishi vipi?

Na nimejifunza kitu si kila mwanamke anaetowa papuchi kuwa anapenda wengine huwa mambo yamewafika kooni hawana option. Tujitahidi wanaume kuwa na mioyo ya huruma kwa wajane na single mothers.
 
Dini ya kweli ni kuwasaidia wajane na yatima..! Hakika hiyo pesa hujaitumia amini usiamini...!

Kunyanyasa yatima au mjane unaitafuta hasira ya Mungu aisei barikiwa sana.

Kitu kingine ungemsaidia cha kuifanyia hiyo 150k, Ili imfae kwa muda mrefu. BARIKIWA SANA MKUU, sijaoa ila huwa nasali sana Mungu akinipa mke na watoto anivumilie wakue ndiyo anihitaji aise.
 
Ni vyema kuwasaidia sio mtu kuona amepata zari la mental .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…