Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
-
- #121
Sijibu kuhusu takwimu ni za lini, Report ni ya Dec. 2019.Pascal Mayala ukuje hapa kuna maswali hayana majibu kuhusu hizo takwimu zako zinaonyesha mwaka 2000 - 2011.
Para ya mwisho sio mipasho, ni mikolezo tuu ile ya kuwaandaa watu kisaikolojia kuhusu 2020.Soma tena para ya mwisho ya bandiko lako, umeandika mipasho bro.
Sawa .mkuuPara ya mwisho sio mipasho, ni mikolezo tuu ile ya kuwaandaa watu kisaikolojia kuhusu 2020.
Hicho wewe ulichokiona kama mipasho, ndicho kitu kinachokwenda kutokea ile October 2020.
P
Ripoti ni ya Dec, 2019. Hivi wajameni mmesoma ripoti?. Mbona watu ni wavivu sana kusoma ripoti na link nimewawekea?!.Pascal Mayalla una matatizo gani mkuu?
Hii ripoti inawahusu Mkapa na Kikwete, wewe unampongeza Magufuli!
Kuna wakati Magufuli anasoma hizi sifa za uongo ansishia kuwadharau tu.
Haya mabadiliko yamefanyika 2000 to 2011.
Ikifanyika sasa hivi nina uhakika utakuwa umeongeza sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania tujifunze kusoma ni ripoti ya lini!. Ripoti hii ni Ripoti ya mwaka 2019 regardless data zilikuwa collected lini, validity ya ripoti yoyote ni the date of publication of the report na sio dates of data collection, hivyo as of now, Tanzania ndio inaongoza kwa kupunguza umasikini uliotopea kwa mwaka huu 2019!.
P
Haya Mkuu ngoja niendelee kukusoma katikati ya mistari.!Mimi ni Msukuma, Wasukuma ndio tunaongoza kwa heshima na unyenyekevu. Hivyo sina dharau kabisa, tena yangefanywa mashindano humu jf kwa watu wanaoongoza kwa kutoa likes, mimi nimo, hata ukinitukana, nakugongea like.
P
Mkuu Masiya, kwanza nikubali sio tuu makosa hata reports interpretation tuu, bali hataPascal umetumia hiki kipengele kutueleza ulicho tueleza "Where has extreme poverty declined the most?
Average of total extreme poverty percentage points change over the circa year 2000-15 (start year - end year), top 15 countries". Data hiyo inaonyesha wamelinganisha 2015 misho (end of year) na 2000 mwanzo (start year). Hivyo data hiyo inawaruhusu kuzungumzia mabadiliko kwa wakati huo. Kama ni hivyo hata kama report ni ya 2019 ukweli ni kuwa reporting period ni 2000-2015. Na kwa period hiyo Tanzania imepunguza umasikini kwa 3.2 "best" performance kwa kipindi hicho. Itakuwa ni makosa wewe kusema in 2019 Tanzania ilipunguza kwa 3.2. usahihi ni kuwa kwa report ya 2019 katika kipindi cha 2000-2015 Tanzania imepunguza kwa kiwango cha 3.2 ikipita nchi nyingine ilizolinganishwa nazo. Sasa kana kwamba haitoshi wewe uka ATTRIBUTE hiyo reduction na awamu ya Tano-hili ni kosa kitaaluma. Ukimpongeza JPM umpongeze kwa niaba ya awamu husika. Interpretation yako siyo sahihi kitakwimu.
Rais Magufuli anapopewaga Salaam za pongezi kwa Uhuru na Jamhuri, huwa anapongezewa nini?. Kwani Uhuru kaleta yeye?. Hapa hatuzungumzii data collected lini, inazungumziwa ni ripoti ya mwaka huu.Kwa nn usifie utawala huu na wakati data ni za tawala zilizopita?
Tusubiri data 2015 mpaka 2025 ndio ulete uhalisia mbona Unataka kufanya vitu Kama hujasoma vile ,
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanabodi,
Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.
Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.
Ripoti hiyo ni hii
View attachment 1304778Year in Review: 2019 in 14 Charts
These charts highlight some remarkable achievements and the serious challenges that remain as we head into 2020.t.newsletterext.worldbank.org
Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.
Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.
Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.
Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.
Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakatakiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.
Nawatakia maandalizi mema ya kuingia 2020!.
Paskali
Hata wewe zezeta..tena bwegeSio vizuri kumwita mwenzio zezeta ni a heri usingeandika chochote ukapita kimya kimya tuu
Wewe ni Fala tuu... sura mbaya kama kichwa cha treniRais Magufuli anapopewaga Salaam za pongezi kwa Uhuru na Jamhuri, huwa anapongezewa nini?. Kwani Uhuru kaleta yeye?. Hapa hatuzungumzii data collected lini, inazungumziwa ni ripoti ya mwaka huu.
Pongezi ni kwa Magufuli na awamu yake.
P
Mkuu hiyo makala yako naweza iandika kwa mistari 2 na ikaeleweka kwa kingereza au kiswahiliMkuu Mliberali, nimekusikia, nitabadilisha
Ila nisaidie nitumie styles gani ili makala zangu ziwe na mvuto, niandike kama nani?, Mkuu Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Maalim Mohammed Said, St. Ivuga, Mag3, Mliberali au niandike kama nani ziwe na mvuto?
P
Umesoma maelezo yote ukaelewa alichoandika Mayalla au umekirupukia kwenye miaka tu?Mkuu Pascal Mayalla 2000 to 2011 ni utawala wa awamu gani?
Ndugu, tafadhali sana ukaye ukijua kuwa wasukuma ni kabila kubwa sana na linaheshimika, usiwachanganye wasukuma wengi walio wazuri na Binadamu wenye utu, wasio wakablia na genge dogo ulilojiunga nalo.Ripoti ni ya World Bank na sio ripoti ya Wasukuma fulani kuonyeshea uchapakazi wa Msukuma!.
Usiniulize mimi kuhusu contents za ripoti hiyo na wametumia vigezo gani, ndio maana ripoti yenyewe yote nimekuwekea, kama una maswali yoyote, waulize wao sio mimi, mimi kazi yangu ni just to share with you kuwa Tanzania tunaongoza dunia kwa kupunguza umasikini!.
P
Nafikiri tunalingalia hili jambo kwa nia tofauti. Huwezi ukampa credits JPM kwa kitu ambacho hakufanya yeye, likewise huwezi kumlaumu kwa kitu ambacho hakufanya yeye. Kwa miaka yote ambayo nimeona maandiko kama haya (ndani na nje ya vyuo) kwa kweli sijaona interpretation na attribution kama yako. Credits zinatakiwa kwenda kwa yule aliyefanya, kiungwana ungesema namuomba raisi wetu afikishe kongole zetu kwa........ Mfano wako wa kitanda hakizai haramu na Tetemeko la Bukoba siyo sahihi. JPM alilaumiwa sio kwa sababu tetemeko lilitokea wakati wake bali kwa sababu (right or wrong) watu walifikiri response yake haikuwa sawa.Mkuu Masiya, kwanza nikubali sio tuu makosa hata reports interpretation tuu, bali hata
Understanding na vigezo ni tatizo, lakini tunapokuja kwenye credits, Tanzania inahesabiwa kama current entity. Kama period of data collection ni 2000-2015 na report ndio imetoka leo, anayepongezwa ni yule aliyepo ripoti ilipotoka.
Hata ndani ya ndoa zetu nyingi, anayemjua baba halisi wa mtoto ni mama, lakini mtoto yoyote akizaliwa kwa mkeo ni wako regardless ni nani haswa aliyeipachika. Jambo lolote jema kuhusu Tanzania likitangazwa kipindi cha Magufuli, credits ni kwa Magufuli, ila hata likitokea jambo lolote baya, pia shutuma ni kwa Magufuli mfano Tetemeko la Ardhi la Bukoba, tulimlaumu Magufuli as if yeye ndie alisababisha hilo tetemeko.
P
Very talented jokagombee bobungeRais Magufuli anapopewaga Salaam za pongezi kwa Uhuru na Jamhuri, huwa anapongezewa nini?. Kwani Uhuru kaleta yeye?. Hapa hatuzungumzii data collected lini, inazungumziwa ni ripoti ya mwaka huu.
Pongezi ni kwa Magufuli na awamu yake.
P
Olenamasala sanaRais Magufuli anapopewaga Salaam za pongezi kwa Uhuru na Jamhuri, huwa anapongezewa nini?. Kwani Uhuru kaleta yeye?. Hapa hatuzungumzii data collected lini, inazungumziwa ni ripoti ya mwaka huu.
Pongezi ni kwa Magufuli na awamu yake.
P
Mkuu kwani Mimi umeona Kuna mahala nimetaja jina la Magufuli Wala mwaka?Na wewe haujasoma chochote ,ulipoona ni pongezi tu ukajiachia.Mwaka 2000 mpaka 2011 alikuwa anaongoza Mh Magufuli !?.
Ndiyo mkuu kwa majibu zaidi juu ya bandiko langu angalia post yangu hiyo ya juu niliyomujibu mkuu juu ya alichoniuliza.