Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Nina wasi wasi na "usomi" wa mtoa mada. Bilashaka ni "postgraduate" ambaye hajajifunza maana na matumizi ya "prospective na retrospective studies".

Nashauri si vizuri kuanzisha mjadala wa somo usilolijua kwasababu unaweza kuishia kupotosha au kujidhalilisha.

Lakini unaposhindwa kuelewa ripoti ya kitaaluma (kisayansi) ni kudhihirisha kuwa "masters" uliyonayo haina msaada kwako kwakuwa mtu wa kiwango hiki anatarajiwa awe amejifunza mbinu za kufanya utafiti (research methods) na kuchambua na kutafsiri takwimu (data analysis and interpretation (statistics)) bila kujali taaluma (profession) uliyosomea.
 
Report inayongelewa ni Miata 2000 Hadith 2011 lakini pongezi ni za rais wa 2015 ha 2019. Hapa rais Magufuli anapongezwa kwa jambo gani Au ni staili ya sasa ya kupongeza kwa kila kitu. Kwa hili la umasikini tusubiri report ijayo tuone kama umeendelea kupungua au umeongezeka. Kupunguza umasikini ni lazima kuekeza raslimali katika kilimo, ufugaji na uvuvi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo wadogo ambako ndiko umasikini uliko. Sasa
swali la msingi ni raslimali kiasi gani imeelekezwa katika sekta ya Kilimo, na tutegemee umasikini utakuwa unapungua au unaongezeka..
 
Hahaha hii nchi huwa tunaongoza kila kitu, Juzi nilisikia tunaongoza Uchumi kupanda East, south and central Africa. Leo Tunaongoza Kupunguza umasikini, kesho tutaongoza nchi tajiri afrika, NA UTASIKIA TUNAONGOZA KUWA NA WAGONJWA WENGI WENYE KWASHIORKOR.
Huwa sishangai siku hizi maana takwimu zetu ni kuongoza tu.
 
Mie amenifurahisha sana! Kawakusanya na kuwakoroga, kisha kawaacha hawaelewi wafurahi, wasikie aibu au wamshambulie Pasco!
Zamani sikuwa ninaelewa neno 'kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa' au hadithi ya joho la mfalme, lakini siku hizi ndio nimeelewa kwa mifano dhahiri.
Ripoti hiyo ni sifa kubwa kwa utawala wa Magufuli. Kweli ni 'jembe'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Masiya, katika bandiko hili, tunsbishania vitu viwili tofauti.
1. Report ya World Bank ya Mwaka 2019 ikionyesha Tanzania ndio inch inayoongoza duniani kwa kupunguza umasikini uliotopea.
2. Date of data collection.

Taarifa yoyote kuhusu jambo lolote inayoihusu Tanzania inahesabiwa kwa siku inapotolewa, the date of release na sio the date of data collection.

Jambo lolote zuri au baya kwa Tanzania, linapotangazwa, credits or blames ni kwa the current regime wakati jambo hilo linapotangazwa na sio data zilikuwa collected lini.

Hii ni World Bank Report ya mwaka huu 2019 imekuwa released December hii 2019, hivyo ni sawa na haki kwa credits kwenda kwa utawala uliopo at the time of publication.

Watu wanaofanya Ph.D by thesis wengine huchukua hata miaka 10 wakifanya research lakini Ph.D zao zinahesabika kuanzia pale wanapo publish kazi zao.

Tanzania tuna tatizo kubwa sana kusoma tafiti za data na kutafsiri. Mfano mzuri ni Ripoti ya CAG ni liripoti limoja likubwa full of data. Media yetu haina uwezo wa uchambuzi wa kutosha kuwatafunia Watanzania kila kilichomo hivyo hufanya cherry picking on few areas of interest ndio wana report.
Wabunge wetu mule wengine ndio hao darasa la 7 unategemea nini kwenye data kama zile.

Mfano kwenye report ya CAG ya 2016, CAG amezungumzia madeni ya nje na the risk associated na kutolipa madeni hayo ni mpaka ndege zetu zilipokamatwa ndipo kuna watu wakajifanya kuanza kushangaa!.

Kwenye bandiko hili, nimeiweka report yenyewe, very few or nobody bothered to read the report and understand it but most are very first to criticise!.
Wajameni someni report.

Tanzania ilipata uhuru wake mwaka 1961. Kila sherehe ya uhuru anayepongezwa ni rais aliye Madarakani kwa mwaka huo. Naamini wengi mnasoma salamu mbalimbali za pongezi kwa rais Magufuli kusheherekea Uhuru na Jamhuri, rais Magufuli anapongezewa nini kwani ndiye yeye aliyeleta uhuru?.

Vivyo hivyo japo utafiti umenywa kwa kipindi kilichopita, Tanzania ndio imeongoza kwa mwaka huu wa ripoti ilipotoka na sio mwaka ule wa utafiti.
Tujifunze kutofautisha Tafiti na Ripoti.

Mfano inawezekana kabisa ukafanyika utafiti wa literacy levels za nchi za Africa Mashariki kutokana na Tanzania kuwa na population kubwa, Tanzania tunaweza kujikuta ndio tunaongoza kwa low literacy levels kwasababu kipindi cha Mkapa na Kikwete elimu ililipiwa. Sasa kipindi cha Magufuli anatoa elimu bure. Ripoti hiyo ikitoka na kuonyesha Tanzania ndio tunaongoza kwa vilaza, nani atazomewa?. Atakayezomewa ni Magufuli!. Na rais Magufuli akizomewa kwa vile yeye anatoa elimu bure, hivyo aibuke na kukanusha ripoti hiyo kwa kusema hao vilaza kwenye ripoti hiyo ni vilaza wa Mkapa na Kikwete, yeye hana vilaza kwasababu anatoa elimu bure?.

Ripoti ya Tanzania kuwa nchi kinara kupinguza umasikini uliotopea ni ripoti ya mwaka huu 2019, pongezi ni kwa Magufuli.
P
 
Sema ww jamaa unajuhudi sana .sijui kwanini hupatagi teuzi .au nyota huna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla Walioko mitaani na wananchi ndo wanajua wenyewe kama umasikini ume wapungukia au umezidi.
Graduates ndio wanajua kama kazi zipo bwerere unachagua.
Na walioko kazini wanajua kama mshahara unakidhi mahitaji.
Na hata Wakuu wa nchi wanajua pia kuwa mazingira waloweka biashara zinakua na kodi itaongezeka . Naamini wanajua ukweli
Mfano mimi nilikua na biashara turnover yangu kabla ya 2015 ilikua 3.5 bilion kwa mwaka
Si haba tulikua tunaenda vizuri sasa 2019 biashara imeshuka by 50% na sababu kubwa ni kufa kwa secta binafsi za ujenzi , real estate na uwekezaji ambazo ndio source ya biashara yetu.
Sasa imebidi kuweka masharti kwa wafanya kazi tuwapunguze au wakubali kubaki ila mishahara tunapunguza kwa 50% tukitegemea mambo yatabadilika baada ya Awamu ya Tano.
Tatizo la awamu hii sio ukosefu wa haki democrasiana utawala bora tu lakini hata sera za uchumi ni mbovu na zitaleta matatizo in future.
Hivo utamu wa chakula aujuaye ni mpishi


Sent from my iPad using JamiiForums
 
ongeza juhudi za kusifu, 2020 ndio hii inakuja lazima jiwe atafanya teuzi baada ya uchaguzi

Lakini kwanini yote haya? unajitoa ufahamu na kujizalilisha hivi, watanzania bado sana kutoka katika absolute poverty!

kuliko kutegemea teuzi pekee, ni vema ukarudi kwenu na ukagombee nafasi mbalimbali za uongozi
 
Validity ya ripoti ni date of publication na sio data zilikuwa collected lini??!!...kweli???!...unachoweza kuipongeza serikali (kama kweli kipo cha kupongeza) ni kwa kuwezesha ripoti kutolewa. Lakini hata hivyo sio wao walioitoa, kwahiyo kwa kifupi hapo hakuna cha kupongeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingawa mfano wako hauendani lakini tuchukue tu huo huo. Hao watoto ni wako na ni kweli utashinda lakini ukweli ni kwamba tokea wamezaliwa wewe ndo baba yao, yaani wewe ndo uliwazaa. Tofauti na hiyo ripoti ni kwamba data zilikusanywa kipindi cha mtu mwingine na zimetolewa kipindi kingine. Mfano wangekusanya data kipindi kile ukakutwa na watoto kumi halafu pengine ukafariki watoto hao wakaishi na mjomba. Je, wakitoa hiyo takwimu watasema mjomba ana watoto kumi au watasema wewe mwaka fulani ulikuwa na watoto kumi??!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli anapopewaga Salaam za pongezi kwa Uhuru na Jamhuri, huwa anapongezewa nini?. Kwani Uhuru kaleta yeye?. Hapa hatuzungumzii data collected lini, inazungumziwa ni ripoti ya mwaka huu.
Pongezi ni kwa Magufuli na awamu yake.
P
Naunga mkono hoja, tunaipongeza serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais Magufuli kwa kupunguza umaskini ktk kipindi cha kuanzia mwaka 2000 hadi 2011.

Hapa kazi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…