Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Huyu jamaa hajatembea mikoani aangalie watoto wakiokota ukoko majalalan ili nafsi imsute aje kufuta uzi wake huu kuna watanzania wenzetu wanaishi maisha ambayo hayaelezeki jamani acheni kusifia kila jambo jamani Daaah

Sent using Jamii Forums mobile app
Miezi kadhaa nilipita mkoa fulani daaah.....ukiambiwa hali ngumu ni ngumu kweli
 
Kaka P. Ni sawa date of publication ni 2019 na ni sawa pia data ni ya 2000-2011. Tatizo linakuja pale unaposema au unapojaribu kusema huo ndio ukweli kwa mwaka huu wa 2019. Ili iwe kweli basi lazima kuwe na njia ya kufanya prediction kutumia hiyo data kutoka data collection time to the current time. Wewe kama mleta uzi ulitakiwa ujiridhishe kwamba kitu kama hicho kimefanyika vinginevyo ulitakiwa uwatahadharishe wasomaji wako kuhusu ukweli huo. Sasa wewe ulivyoiweka inaonyesha kama mambo hayo ni kweli kwa 2019 na bahati mbaya hata kama ni kweli hiyo haikuwa awamu ya Magufuli. Hapo ndio umejipalia mkaa.

Ningekuwa wewe badala ya kuwalaumu watanzania nige reflect, na kama wako sawa basi hakuna ubaya kujisahihisha au kukubali umekosea. Ukishupaza shingo hii itakula kwako kama mtu mwenye heshima zake hapa JF. Wish you all the best in this.
Mkuu Masiya, katika mashindano ya kuondoa umasikini uliotopea iliyochapishwa mwaka huu, inaonyesha Tanzania ndio inaongoza duniani!. Hata kama data ni za zamani, data hizo ndizo ime Tanzania uongozi mwa mwaka huu!.
P.
 
Wanabodi,
Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.

Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.

Ripoti hiyo ni hii
View attachment 1304778

Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.

Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.

Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.

Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.

Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakatakiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.

Nawatakia maandalizi mema ya kuingia 2020!.
Paskali
Anayekerwa na ukabila aanzie kulaani hapa
 
Viva awamu ya tano, Viva JPM.
Uchumi unakua kwa kasi zaidi ya 7% na umasikini umepungua sana sana Tanzania na hali ikiendelea hivi soon Tanzania itakuwa zaidi ya dubai..
 
Watanzania tujifunze kusoma ni ripoti ya lini!. Ripoti hii ni Ripoti ya mwaka 2019 regardless data zilikuwa collected lini, validity ya ripoti yoyote ni the date of publication of the report na sio dates of data collection, hivyo as of now, Tanzania ndio inaongoza kwa kupunguza umasikini uliotopea kwa mwaka huu 2019!.
P
Kwahiyo ikitolewa ripoti ya Tanganyika na harakati za kusaka Uhuru (mwaka huu) utampongeza Magufuli?!?

Alichokufanya Ndugayi Job Mungu anamwona.
 
Kwahiyo ikitolewa ripoti ya Tanganyika na harakati za kusaka Uhuru (mwaka huu) utampongeza Magufuli?!?
Alichokufanya Ndugayi Job Mungu anamwona.
Mkuu Roboti la Matope, ikitokea ripoti ya nchi zinazoongozwa vizuri toka zipate uhuru na hazijawahi kupinduliwa, Tanzania itakuwepo na pongezi zitakwenda kwa Magufuli.
By the way nimemkumbuka Katope, na kuna dalili ya mvua, usije kusema sikukutahadharisha,
P
 
1577459151222.jpeg
Pongezi kwa serikali ya awamu ya tano.
 
Kiukweli kunahitajika elimu kwa Watanzania kusoma ripoti. Mwaka 2000-2011 was the data collection period, unaweza kukuta kwa data hizo, kwa mwaka huo, wala Tanzania haikuongoza. Date of publication ndio hii ya Dec, 2019. Hii maana yake Tanzania ndio inayoongoza sasa kwa ripoti ya mwaka huu.

Mimi nina watoto 10!. Tukifanya research ya members wa jf wenye watoto wengi kwa mwaka huu wa 2019, naweza kuongoza. Ikichapishwa Ripoti ya "Wana JF Wenye Watoto Wengi 2019", jina langu likaongoza. Ukiangalia niliwapa lini, huwezi kuja na hoja kuwa tangu 2015 tayari nilikuwa na watoto 10, hivyo hiyo rekodi ni 2015!. Ripoti ikitoka mwaka huu, mimi nikaongoza kuwa na watoto wengi, haijalishi walizaliwa lini, bingwa wenu nitakuwa ni mimi, unless aje mwenye watoto 11!.

Sasa katika ripoti ya mwaka huu ya WB kuhusu kiwango cha kupungua umasikini duniani, Tanzania ndio tumeongoza sio kwa nchi za East Africa, Sio kwa nchi za Bara la Africa, bali tumeongoza kwa dunia nzima!. Haijalisi data zilikuwa collected lini, bali ripoti ndio imechapishwa sasa na ni ripoti ya mwaka huu!.
P
Paskali Njaaa, hapa sio Facebook!!! Hii ni JF!

Hii mifano yako ya kitoto usituletee hapa. Yaani mwisho wa data collection ni 2011 then report itolewe leo bado uendelee kuwa kinara?!? Je kama kuna watoto wamekufa?!? Au kuna memba kama Aspron kapata mapacha mfururizo na kakuzidi watoto?!? Anyway mfono wako ni irrelevant.

Pole, usikaze shingo, litavunjika!!! Tafuta msaada
 
Paskali Njaaa, hapa sio Facebook!!! Hii ni JF!
Hii mifano yako ya kitoto usituletee hapa. Yaani mwisho wa data collection ni 2011 then report itolewe leo bado uendelee kuwa kinara?!? Je kama kuna watoto wamekufa?!? Au kuna memba kama Aspron kapata mapacha mfururizo na kakuzidi watoto?!? Anyway mfano wako ni irrelevant.
Pole, usikaze shingo, litavunjika!!! Tafuta msaada
Ripoti ni ya World Bank na sio ripoti ya Wasukuma fulani kuonyeshea uchapakazi wa Msukuma!.
Usiniulize mimi kuhusu contents za ripoti hiyo na wametumia vigezo gani, ndio maana ripoti yenyewe yote nimekuwekea, kama una maswali yoyote, waulize wao sio mimi, mimi kazi yangu ni just to share with you kuwa Tanzania tunaongoza dunia kwa kupunguza umasikini!.
P
 
Magufuli alishiriki vyema katika kujenga miundombinu iliyofungua mawasiliano baina ya mikoa....upende usipende Magufuli na CCM ni moto wa kuotea mbali
 
Unatukana watu hata usiowajua kisa kaandika tu usivyopenda wewe? Unahitaji therapy wewe, ukiendelea hivyo bila ya therapy utakuja kujiuwa tu siku.
Mayalla ni verified user!! Pia ni mwandishi mtangazaji so ni maarufu!!! Tunamjua. Mlichomfanya msukuma wa watu, Mungu anawaona
 
Ripoti ni ya World Bank na sio ripoti ya Wasukuma fulani kuonyeshea uchapakazi wa Msukuma!.
Usiniulize mimi kuhusu contents za ripoti hiyo na wametumia vigezo gani, ndio maana ripoti yenyewe yote nimekuwekea, kama una maswali yoyote, waulize wao sio mimi, mimi kazi yangu ni just to share with you kuwa Tanzania tunaongoza dunia kwa kupunguza umasikini!.
P
Hakuna anayepinga Tanzania kuongoza, tunapinga unaavyotaka kuaminisha Umma lwamba JPM ndo kafanya Tanzania iongoze wakati data zilikua collected 2000 to 2011.


Pongezi zielekeze kwa wahusika.


NB; Kuna jamaa anaandaa report ya kuzaama kwa MV Bukoba na MV Spice obvious utatoa lawama zako kwa Magufuli maana report itatolewa mwaka kesho mwanzoni
 
Back
Top Bottom