Pongezi Yanga kwa usajili wa viwango vya juu

Pongezi Yanga kwa usajili wa viwango vya juu

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Nafikiri mechi ya Yanga dhidi ya Vipers ilikuwa ni moja ya mechi bab kubwa, Vipers walionyesha ni namna gani wako vizuri kiufundi, walikuwa wanacheza objective football, walikuwa very sold kwenye ngome yao baada ya kutangulia kupata bao la mapema, ni moja ya timu ambayo iko vizuri sana kwenye muunganiko kucheza kitimu uwanjani.

Yanga walipotezwa zaidi na goli la mapema liliwafanya wawe na presha kubwa ya kutaka kuonyesha kwamba wanaweza mbele ya mashabiki wao kitu ambacho kiliwafanya waanze kucheza na jukwaa muda mwingine badala ya ku-focus na kile walichoelekezwa na kocha, pia kitendo cha kumsogeza nyuma Bangala na Sure Boy kucheza Kama namba 6 kidogo ilileta shida kwasababu Mwamnyeto akuwa vizuri alikuwa anafanya makosa mengi ya kiufundi, bahati nzuri kocha alimbadilisha kipindi cha pili na kuingia job na timu ikatulia pia baada ya kuingia Bigirimana.

Maingizo yote mapya yaliyocheza mechi iyo yalikuwa bora sana, uyu Bigirimana hauitaji elimu kubwa ya mpira kujua kwamba ni moja ya usajili bora ambao Yanga wameufanya, utulivu wake, pasi zake zenye macho na za hatari, anakaa kwenye nafasi kwa wakati muafaka, kwakweli ni quality prayer, Azizi Ki ameonyesha ni kwanini amekuwa MVP wa ligi ya Ivory Coast, amecheza mechi ya kwanza na klabu yake mpya na mazingira tofauti na wachezaji tofauti lakini ameonyesha ni mchezaji wa aina gani ni fundi hasa vile vile kwa Morrison na Lomarisa, wakipata mechi nyingine 3 au 4 wakazoeana na wenzao uwanjani (combination) yao itakuwa hatari sana.

Kwa nilichokiona kinawasumbua jana ni muunganiko wao bado aujacklick, bado wana-struggle kujua mikimbio ya kila mchezaji uwanjani ikoje, kwamba nikipiga penetration pass pale mayele ataikuta au nikienda upande ule fei toto atakimbia upande huu, ni vitu ambavyo wanaendelea kuvisoma taratibu na baada ya hapo itakuwa balaa tupu kwa timu pinzani, binafsi yangu matokeo sikuyatilia maanani sana nilikuwa naangalia masuala ya kiufundi zaidi hasa hasa maingizo mapya, kwasababu Kama ni matokeo pia yanga walikosa nafasi za kuweka mpira kambani.

Makambo alipata nafasi akashindwa kuzitumia vizuri, cha msingi ni timu imechezaje na maingizo mapya yatafiti vipi kwenye mfumo, nimejiridhisha yanga itakuwa na viungo supa sana na hatari sana wakizoeana ni suala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi.

NB: Pasi za bigirimana ni balaa jingine mjini👏👏👏👏
 
Laiti yanga ingeendelea na kile kikosi cha kwanza wangechomoa na kuongeza goli. But walivoingiza wachezaji wapya ndo mambo yakawa mabaya.

Pass zinapotea, mikimbio hakuna, penetration pass hakuna. Hivi Mauya mkabaji aliingia kufanya nn wakati timu inahitaj attacking.
 
duuh ila mapenzi kweli upofu
Laiti yanga ingeendelea na kile kikosi cha kwanza wangechomoa na kuongeza goli. But walivoingiza wachezaji wapya ndo mambo yakawa mabaya.

Pass zinapotea, mikimbio hakuna, penetration pass hakuna. Hivi Mauya mkabaji aliingia kufanya nn wakati timu inahitaj attacking.
 
Weka link tujue kweli aziz ki alikua mvp kule ivory Coast
 
Weka link tujue kweli aziz ki alikua mvp kule ivory Coast
MVP wa Serbia huyu hapa
JamiiForums-177395527.jpg
 
Back
Top Bottom