Pongezi za dhati kwa Yanga na Simba, mmetuheshimisha!

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Posts
5,089
Reaction score
9,664
Wawakilishi Wa Tanzania katika Michuano Mikubwa Kabisa kuliko Yote inayoandaliwa na CAF ya Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga na SIMBA zimeweza Kufanya vyema na Kuheshimisha Taifa.

Simba Wakiwa kwenye Kiwanja Cha Levy Mwanawasa Mjini Ndola imeweza Kuituliza Timu ya Power Dynamo ya Zambia Katika Kiwanja Chao Cha 'NYUMBANI' na kutoka nayo Sare ya Bao 2 kwa 2.

Nayo Yanga iliyosafiri nchini Rwanda,nchi ambayo inatumiwa kama 'Home ground' na Timu ambayo Kwao asilia Sudan Kuna Machafuko hivyo kuLAZIMIKA kucheza nchi nyingine kama Wakimbizi imeweza Kushinda na kujiweka kwenye mazingira Rafiki ya Kufuzu..!

Ukiwasikiliza Wachambuzi Wengi Wa Soka wanakiri kuwa Timu Ya Yanga iwapo Wangekuwa Makini basi wangeondoka na Ushindi Mnono Zaidi Ya hapo na Wametolea mfano Simba ilivyoweza Kumfunga Horoya 7 bila Msimu ulioisha.

Yote Kwa Yote Pongezi kwa Timu zote... !
 
Kwahiyo Simba na yanga watakavyo Rudi home shangwe sawasawa tukiwapokea?
 
Hili Swali Jibu Lake niseme tu ... Wale ambao Malengo Yao Makubwa ni Kujiona Wamedumbukia 'Grupu Steji' ya CL ya CAF ni Wazi Tunaweza kushuhudia parade la Mapokezi ya Siku nzima barabara zote za Katikati Ya Jiji zimefungwa...!

Ila Wale Wenye Malengo ya Kufika Semi au Final za CL hawatakuwa na 'hype' ya
Kiviiiile ..! Kwanini Malengo ya Timu kubwa always sio Kuingia Makundi....!

Hata hivyo Inaeleweka ...iwapo hujaingia Makundi CL CAF for 26 years Lzm Upagawe.!
 
Mimi naona ungefumba tu macho na kuwapa pongezi Yanga! Simba kwa mpira ule wa leo, wana mlima mrefu wa kupanda siku za usoni.

Wakubali tu kucheza mpira mtamu kama ule wa Yanga! Mpira wa papatu papatu, nawaapia hautawapeleka kokote.
 
Kwaiyo, Maoni Yako ni Yepi Kwa hawa Wachambuzi Wanaodai Ilitakiwa Yanga iwabugize Tano Zingine hawa Merekkh kama Yanga ilivyofanya Kwa ASAS kwa kuwa hii timu ya Sudani hata Ligi tu kule Sudani hakuna.?

Eti, Wachambuzi hao Wameenda mbali Kuwaita Merrekh ni Kama Wakimbizi Wanatanga Tanga.. hivyo kuja Kujistiri Rwanda ndio kuwe uwanja wa Nyumbani.?
 
Hao unaowaita wachambuzi i don't know wachaa mbuzi ni akina nani? Tuanzie hapa kwanza. Isije ikawa napoteza muda wangu hapa, kumbe wahusika wenyewe ni akina Jemedari Said na Geof Lea.
 
Ukiwasikiliza Wachambuzi Wengi Wa Soka wanakiri kuwa Timu Ya Yanga iwapo Wangekuwa Makini basi wangeondoka na Ushindi Mnono Zaidi Ya hapo na Wametolea mfano Simba ilivyoweza Kumfunga Horoya 7 bila Msimu ulioisha.
Hao wachambuzi wanajua tu kuizungumzia matatizo ya Yanga pekee ya Simba na Beleke wake kushindwa kuzitumia nafasi hawazioni. Simba mechi ilikuwa nyepesi ila ubutu wa safu ya umaliziaji + ubovu wa safu ya ulinzi ndio ukawamaliza. Chama kaendelea kuonesha umuhimu wake ndani ya kikosi cha Simba
 
Kwaiyo, Maoni Yako ni Yepi Kwa hawa Wachambuzi Wanaodai Ilitakiwa Yanga iwabugize Tano Zingine hawa Merekkh kama Yanga ilivyofanya Kwa ASAS kwa kuwa hii timu ya Sudani hata Ligi tu kule Sudani hakuna.?

Eti, Wachambuzi hao Wameenda mbali Kuwaita Merrekh ni Kama Wakimbizi Wanatanga Tanga.. hivyo kuja Kujistiri Rwanda ndio kuwe uwanja wa Nyumbani.?
Kumbukumbu zenu mziweke sawa, Asas alipigwa goli mbili kavu first leg ila second leg akala chuma tano, hivyo kama unataka kulinganisha matokeo ya Asas na Al Merrikh basi jibu unalo nini kitatokea second leg. Kingine tu nikukumbushe kuwa achana na hawa Al Merrikh ni wakimbizi twende kwa bingwa wa CAF super cup alifanywa nini na Yanga kule kwao Algeria?
 
Mimi naona ungefumba tu macho na kuwapa pongezi Yanga! Simba kwa mpira ule wa leo, wana mlima mrefu wa kupanda siku za usoni.

Wakubali tu kucheza mpira mtamu kama ule wa Yanga! Mpira wa papatu papatu, nawaapia hautawapeleka kokote.
Yanga mwaka jana hawakufikia hata hiki kiwango "kibovu" walichokionyesha Simba jana

Hawakuweza kufunga goli la ugenini hata moja kwenye hatua hii, kule Sudan, Simba imetoa sare ya 2-2 ambayo nyie mngeitoa mwaka jana mngeshangilia kama mmetwaa kombe la dunia
 
Kumbukumbu zenu mziweke sawa, Asas alipigwa goli mbili kavu first leg ila second leg akala chuma tano, hivyo kama unataka kulinganisha matokeo ya Asas na Al Merrikh basi jibu unalo nini kitatokea second leg. Kingine tu nikukumbushe kuwa achana na hawa Al Merrikh ni wakimbizi twende kwa bingwa wa CAF super cup alifanywa nini na Yanga kule kwao Algeria?
Mimi nashindwa kuelewa hii mantiki ya kujivuna eti mlimfunga USM kwao, wakati naye aliwafunga hapa kwa goli nyingi zaidi na ndio maana akachukua kombe, timu bora ndio ilichukua kombe
 
  • Thanks
Reactions: BRN

"Timu bora ndio imechukua kombe"
Yanga ilicheza na timu bora na mechi kuisha kwa aggregate 2-2 dhidi ya USMA.
USMA amekuwa ndio timu bora kuliko timu zote za klabu bingwa na za shirikisho. Kama timu imeweza kutoka 2-2 na timu bora ambaye ndiye bingwa wa mashindano yote ya CAF je hao wasudan hata ingekuwa sio vita wangeweza kipi dhidi ya Yanga?

Mziki wa USMA hata Al Ahly mwenyewe kasanda
 
Kwa hiyo hata Simba ilivyotoa sare na Wydad basi tuseme Simba ni sawa na Wydad, kisa walitoa aggregate ya 1-1?

Hii ni mantiki ya ajabu sana kwenye mpira, timu mbovu huwa zinatoa draw ama kufunga timu bora lakini haikuwa kuwa bora imezidiwa...
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Back
Top Bottom