Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Kwanza nianze kwa kusema kwamba mimi ni mdau mkubwa sana wa maendeleo ya jiji la Dar na binafsi ninatamni sana Dar es Salaam liwe jiji la kisasa kabisa.
Leo naandika waraka huu kumpa pongezi zangu za dhati kabisa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Ndugu Kunenge kwa namna ulivohakikisha kwamba hauwabugudhi Watanzania walipokuwa wanampokea Jemadari Lissu. Sitaki kufikiri kwamba MSIBA wa MZEE MKAPA umechangia hili hapana,Nataka kuamni kabisa kwamba wewe unazo hekima na busara za kiutawala na kwamba yaliyotokea jana ni udhihirisho wa kuzaliwa kwa Dar es Salaam Mpya.
Nakukaribisha sana Kigamboni uje kusimamia Miradi maana huyu Boss wako wa Zamani huku sis hatumtaki tunataka wewe uje maana wewe sasa ndo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.Ile kasi mnayoonesha ya kukamilisha hiki kipande cha Barabara hapa Mnadani ni nzuri sana,Wahimize wakandarasi wafanye kazi usiku na mchana ila uje utuzindulie hii rounda about hapa ambayo Boss wako wa zamani alishindwa kuitengeneza kwa miaka mitano.
Vile vile uje huku Kigamboni uangalie namna ya kufanya kwenye hii barabara ya Kutoka Tungi-Mnadani kupitia Kisota mpaka Mjimwema ambayo naona inawekewa lami lakini wakandarasi wanafanya kazi kivivu sana Ili uwachangamshe wafanye kazi kwa bidii.
Hapa kwenye Bonde la maji wote walipojenga na ambapo hapapitiki wakati wa mvua naamini kabisa unaweza kupafanyia jambo ili pawe bora zaidi.
Vile nikukumbueshe tu kwamba Lile eneo la Manispaa liliko karibu na barabara njia ya kwenda ofisi ya mkuu wa wilya na mkurugenzi litolewe kwa wananchi kwa mkataba wajenge Majengo ya Biashara kwa mkataba na Manispaa ili Wana Kigamboni tuwe na Shopping centere ya Kisasa Pale.Kama Pesa Ipo Mnaweza kujenga Stand Kubwa ya Kisasa Kabisa Pale pamoja na Masoko na Ofisi space.ili kusogeza huduma huku kati.Cha muhimu ni kuhakikisha kwamba kunakuwa na huduma za muhimu kama umeme maji na internet yenye kasi.Mkifanya hivyo Na hakika Geza Ulole itakuwa Centre ya Kigamboni
Pia Hili Daraja la Kwenda Mbutu naona Kazi inaenda vizuri ila spidi ya Kazi ni ndogo sana,Wekeni Mipango ya Kuiwekea hii barabara ya Dege Mbutu Lami kabisa ili sisi wana kigambini tuendelee kufurahia maendeleo.Huku Kimbiji nako Msitusahau bwana,hata sisi ni watanzania Pia
Kwa kuwa ulikuwa katibu tawala najua mengi tayari ulikuwa unayafahamu ili nitaurahi sana ukija Kigamboni kutusalimia wanakigamboni maana hapa ndipo JIJI jipya la Dar-Satelite city litakapojengwa na Tunataka wewe uje uongozi njia.
Hongera sana Kunenge kwa kuonesha hekima ya kiuongozi.
Kizito S.
Kimbiji-Kigamboni