Poor Ali Kiba, kama hujui kiingereza ni vema kuongea lugha yako tu

Poor Ali Kiba, kama hujui kiingereza ni vema kuongea lugha yako tu

Stupid him....kwanini asiongee kiswahili tu.
Nimejikuta naona aibu mm hapa.
Mkuu IGWE sio peke yako iliyokugusa; mimi nimeshindwa kuimalizia yote hiyo video clip. Mda mwingine tunajiabisha sisi wenyewe. Naimani kama angeongea kiswahili angekuwa na mengi ya kuhamasisha vijana kuliko hayo aliyojibabaisha nayo. Poor Ali
 
Mkuu IGWE sio peke yako iliyokugusa; mimi nimeshindwa kuimalizia yote hiyo video clip. Mda mwingine tunajiabisha sisi wenyewe. Naimani kama angeongea kiswahili angekuwa na mengi ya kuhamasisha vijana kuliko hayo aliyojibabaisha nayo. Poor Ali
HUYU MTU SIMPENDI ANAVYOJISHEBEDUA SHEBEDUA HALAFU HAPENDI APITWE NA DIAMOND JAPO HAMKARIBII
 
Yuko sawa na anaweza sana coz hii lugha ilikuja na jahazi tu!!! hivyo itabaki kuwa ya Kuja!!!
 
Wengi tuna ujuzi wa kuponda ilimradi tu. Ebu kila alie changia hapa arudi kuchangia kwa kingereza baada ya hapo ndo tuanze kumkosoa huyo Kiba
Na ndio maana hatuchangii kwa kingereza kwani kiba alizuiwa kuongea kiswahili?? angeafunguka tu kw alugha mama na angejielezea vizuri tu na kwa nafasi kama mwenzake baraka the prince na mkalimani wake
 
Watu hujifunza kutokana na makosa so next time ata jitahidi.
 
Nimeiona clip hiyo, jamaa kaniudhi sana aisee na mbaya zaidi yuko front . kwanini asingeongea kiswahili tu? Yaani kwa jinsi alivyokuwa anajikanyaga,kila mtu ilimpa shida aisee. Kuliko kuonekana ju.ha na ch.iz.i kama vile,ni bora uongee kiswahili safi ukabaki na heshima na utu wako badala ya kukomalia mambo ambayo si lazima na wala hukulazimishwa kuyaweza.
You know, underground children sijui musicians wanti to be laiki mi, it makes me feel laiki a king, dah! Nimeudhika sana.
 
Watu hujifunza kutokana na makosa so next time ata jitahidi.
Siyo mara yake ya kwanza kuongea broken,huyo jamaa hajifunzi. Pitia youtube ndio utachoka. Na sijui kwanini hawa baadhi ya wasanii wanakomalia English wakati hawaiwezi? Nani aliwaambia ndio lugha pekee inayopaswa kutumika? Mbona wasanii wanaoongea French hawajishughulishi nayo kama hawaiwezi?
Kama unaona una hamu sana na Kiingereza, mwambie mtu wako wa PR akuombee naswali utakayoulizwa ili uyaandalie majibu muruwa,siyo kosa. Ukiwa nayo mkononi unayafanyia mazoezi majibu yote na ukifika pale unakuwa na confidence. Hata wenye lugha yao sometimes huwa wanababaika wanapoulizwa baadhi ya maswali kwa ghafla kwenye matukio kama hayo,sembuse wewe?
 
Mshikaji kajitahidi tena sana.... Nilijua ametema udambwi kama wa MRISHO KHALFAN NGASSA
 
Back
Top Bottom