Kama mtanzania, kama binadamu, ni lazima nihitaji huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Ili kuyapata haya lazima nizifuate mahala huduma hizi zilipo iwe ofisi za serikali na zisizo za serikali, ofisi za huduma, mahotelini, mahospitalini, bank, nk. Katika watoa huduma kumi wa kitanzania, zaidi ya 75% hutarithika jinsi ambavyo wana toa huduma kwako kama mteja. Wengine huongea kama umewalazimisha vile, wengine huwa wako busy na mambo mengine wakati ukiwaeleza shida zako, wengine lugha za ukali, nk. Mbaya zaidi utekelezaji wa kile unachokihitaji hata kama unakilipia huwa ni wa kusukuma sana na pengine usifanyike kabisa. Waweza ambiwa uje baada ya siku kadhaa, lakini ukirudi hakuna kilichofanyika. Mbaya zaidi mzaha huu unafanyiwa bila kujali umetoka mamia ya kilometer kwa ajili ya jambo hilo.
Nini chanzo? Mishahara mdogo? Uvivu? Ubabe na dharau?
Je hali hii inaathiri vipi uchumi wetu?
Watanzania tubadilike! It begins with me!
Nini chanzo? Mishahara mdogo? Uvivu? Ubabe na dharau?
Je hali hii inaathiri vipi uchumi wetu?
Watanzania tubadilike! It begins with me!