Poor phone manners can cost you a fortune.

Ahaaaa ahaaaa ahaaa mtu wa hivi ategemee kupata tusi maana watu wengine huwa hawacheleweshi utasikia mjinga nini
 
Dah, kuna mtu aliwahi kusema Teknologia ya habari inatujia kwa kasi, wakati jamii haija jiandaa kuipokea na kuitumia kwa usahihi. Ndo maana bado kuna changamoto kama hizi. Hushangai mtu yupo kanisani anajiinamia anapokea simu? Kwenye mkutano, darasani, nk nk.
 
Kwa kweli bado tuna njia ndefu ya kwenda kwenye matumizi ya simu, ila ninakubaliana na wengi kwamba angalao ustaarabu uanze na aliyepiga simu. Mimi kuna mtu alishanipigia nikamuuliza wewe ni nani akakasirika eti haiwezekani simfahamu, nikamwambia nilipotezaga simu na namba zilizokuwepo hakukubali akaamua kukata simu nami nikapiga kimya!
 
ila hizi simu zinaboa wakati mwingine jamani!!!

sema tu basi no way out!!
 
Mikasa ya simu ipo mingi, lakini hilo la anayepiga akakuuliza wewe nani linaudhi mwisho. Jengine ni lile la wahudumu kuwacha kuhudumia wakaanza kung'ang'ania simu kama washamba. Lakini kuna tukio moja liliniwacha hoi. Ni hivi:
Jamaa yangu wa karibu alinibeep. Nilipompigia akadai nimrushie 5,000/= simu yake kavu, nikamtumia. Baada ya dakika chache akanibeep tena. Kumwuliza ni cha zaidi, akanijibu "asante sana, pesa nimezipata".
 
Hivi kwa nini watu wanapata ugumu kujitambulisha kwanza? Kwa nini unataka kuficha identity yako? kwani kutaja jina kuna tatizo gani?

Mimi nadhani mtu akikupigia simu (kama ni kutoka katika namba au sauti usiyoweza kuifahamu mara moja), ni ustaarabu zaidi uanze kwa kutaja jina lako na kisha umuombe aliyepiga nae ajitambulishe (eg ..Hello!...mimi ni SMU, nani mwenzangu?, au ...Hello, habari?, mimi ni SMU, ninaongea na nani?). Ukifanya hivi, mara moja kama mpigaji amekosea namba ataomba radhi na kukata simu au atajitambulisha na kusema sababu ya yeye kupiga.
 

hahahahaaaaaaaa nimeipeda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…