Porojo za Wana Yanga Kubeza Uwezo Wa Fei Toto na Kumpaisha Aziz K, Mimi Mchambuzi Nguli Nasema Feisal anastahil kuwa MVP

Ubaya Ubwela

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2024
Posts
1,353
Reaction score
3,060
Timu Nyingi za nje zipi zinazomuhitaji Aziz K Zaidi ya Tetesi

Hakuna timu yotote kubwa iliyomuhitaji Aziz k kutoka nje, tunapozungumzia timu kubwa zinajulikana,

Aziz K ni One season Wonder, watu wenye weredi na soka hawawezi kukurupuka kununua kimulimuri kinachowaka usiku tu mchana kinapotea,

Narudia tena Aziz K ni One season Wonder na msimu ulipopita ndo msimu wake bora toka aanze soka, na unaweza kubaki kua msimu wake bora asi shine tena,

Aziz k Na fei toto walicheza timu Moja na msimu Ule Aziz alikua anasubili nje Fei Anaanza, Fei ana muendelezo wa kufanya vizuri kwa zaidi ya misimu mitatu

Aziz k Alifanya vizuri kiasi akiwa Asec akaja yanga akadrop mbele ya Feisal na Fei baada ya kuondoka ndo Aziz aka shine

Timu Kubwa Zilizo muhitaji Feisal ni

Simba
Wydad
Mamelodi

Timu zilizomuhitaji Aziz K

Kaizer Chief
USMA Alger
JS
 
Wewe ni kichaambuzi, ukitaka kujua ni nani bora angalia takwimu za wote wawili huyu kacheza Yanga na huyu kacheza Azam je takwimu zina mbeba yupi? Aziz Ki hajaishia kwenye ligi ya ndani tu bali hadi CAF kafanya vyema vipi kuhusu Feisal?

Mfano tu mdogo tupo maandalizi ya msimu mpya, tayari Yanga imecheza mechi za kirafiki za kimataifa na Azam imecheza mechi za kirafiki za kimataifa lakini mpaka sasa Aziz Ki kaonesha bado atakuwa ni mwiba kuelekea msimu mpya lakini wewe mganga wa kienyeji unatuambia hatotamba tena msimu huu je huo ni uchambuzi au utabiri au wivu?

Azizi Ki kukaa benchi dhidi ya Feisal ilitokana na mfumo wa kocha sio ubora wa Aziz Ki. Unasema Aziz Ki hakutakiwa na timu nyingine wakati tuliona wazi wazi Belouizdad wakitoa dau kubwa la kumtaka na barua yao ilioneshwa mitandaoni, Kaizer Chiefs walimtaka, Mokwena alivutiwa sana na Azizi Ki.
 
Hapo kwenye Wydad na Mamelodi usichokijua ni kuwa kocha wa Mamelodi ndio kocha wa sasa wa Wydad hivyo Mokwena alimtaka akiwa Mamelodi na sasa anamtaka akiwa Wydad ila hizo zote ni tetesi tu kama angekuwa anatakiwa kweli Azam wasingeshindwa kumuuza. Wamemuza Kipre Junior ambaye ni mchezaji hatari, msumbufu na kipaji kwa bei chee ndio washindwe kumuuza Feisali? Ukiona hivyo ni maneno tu ya mtandaoni ila hakuna cha Wydad wala cha Mamelodi walio serious na Feisali labda Simba pekee.
 
Hata Nabi kocha wa Kaizer Chief kasema anamtamani Feitoto. Nabi alikuwa kocha wa yanga na kawafundisha wote wawili kwanini anamuhitaji Feitoto zaidi? Kwa sababu Fri ni Bora kuliko Azizi K.
Hata alikuwa kocha wa Taifa Stars alisema Feitoto anawexa kucheza Barcelona Ina maana wote hawana ajili.
 
Weka clip ya Nabi akiyaongea hayo, halafu la pili je Nabi aliulizwa kwa kuchagua kati ya hao wawili au aliulizwa kwa kutoa maoni yake juu ya Feisal?
Swali la mwisho kama Feisal ana uwezo wa kucheza Barcelona, kwanini kabakia Azam? Nabi huko alipo ana project na Rabat na pia na Kaizer kwanini hana nia ya kumsajili kama kamuona anafaa kufanya nae kazi? Azam ela wanaitaka na hata Feisal nae kwenda nje ya nchi na kulipwa vizuri zaidi anatamani ila hakuna klabu iliyoleta ofa hapo Azam. Azam wamemuuza mchezaji mwenye msaada zaidi kwenye timu Kipre Junior kwa bei ya kawaida tu. Huyo Feisal kama kuna kungekuwa na ofa wasingeiacha
 
ubwela fc ushakunywa kizampa
 
Fungua hiyo link usome
 
Ndiyo hawana akili tena siyo wao tu Hadi na wewe.
 
Kwenye hiyo link uliyotuma, sijaona Nabi akisema Feisal ni bora kuliko Azizi Ki bali amesema anatamani kufanya kazi na watanzania na moja ya wachezaji wa Tanzania anayependa kufanya nae kazi ni Feisal. Sasa sijui hayo ya Feisal ni bora kuliko Aziz Ki Nabi kayaongea wapi?

"Nabi aliema ana kiu ya kufanya kazi na wachezaji wa kitanzania, lakini namba moja ni Feisali."

"Nawapenda watanzania nilitamani mmoja wapo awe kwenye timu yangu ili nisaidie kukuza vipaji nje ya hapo Tanzania"
 

Weka ushahidi ulionyooka kama Mamelodi na waydad zimemuhutaji Fei. Ila fei na azam wakakataa
 

Hao mwanaspoti wanaandika habari wauze magazeti.

Weka link za media za majuu zinaoonesha ofa za fei toto media zipo nyingii nenda ka google tu.

Achana na hizo link za mwanaspoti na dimba zinazoandikwa na wahuni wa kariakoo wanaotaka kuuza magazeti tu.

 
Narudia tena Aziz K ni One season Wonder na msimu ulipopita ndo msimu wake bora toka aanze soka, na unaweza kubaki kua msimu wake bora asi shine tena,
Hujui unachokiongea mkuu, weka ushabiki maandazi pembeni Azizi Ki ni bora na atazidi kulithibitisha hilo.
 
Huyu feisal amezidiwa hata na bacca huko kwao zanzibar, alafu aje huku bara kapapatua papatua awe mvp, labda mvp huko kwenu kwa makolo
 

Attachments

  • 1718025662182.jpg
    46 KB · Views: 6
Ukiwa bora utalinganishwa na watu wa hovyo tena kwa kudogodeshwa ilihali takwimu zinauonyesha uwezo wako hadharani, Wachawi watakuja kumpondea Ki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…