Kuna kitu watu wengi tunakosea pale tunapoamua kununua magari. Ni vigumu saana kupata gari lenye kila kitu unachohitaji in the same package. Ukitaka performance kwenye gari, jua utasacrifice fuel economy. Ukitaka fuel economy, performance ni tatizo. Ukitaka comfort, jua handling unapoteza. Na vingine kama hivyo. Na from experience, gari ambazo ni comfortable na luxurious mara nyingi zinakua na engine kubwa, sababu kuna vitu vingi saana vinavyoongeza uzito. eg power seat, seat heater, leather seats na vingine vingi. Pia gari luxurious zimetengenezwa kwa watu ambao kwao mahitaji sio pesa, so hawawazi saana mafuta.
Brevis ilitengenezwa kwa mtazamo huo. Kujaribu kuwapata Wajapan gari lenye comfort na performance ya compact executive salon za Ulaya kama 3 series, C class na A4. Ingawa haikufanya vizuri kwenye mauzo, na hiyo kazi ya kupambana na kina 3 series na C class ikaachiwa Lexus Is ambayo mwanzo (before 2005) ilikua haiuzi Japan kama lexus, bali Altezza. Pia kama jina lake Brevis linavyomaanisha, ni brief. So ilizalishwa kwa muda mfupi.
Sasa sisi hatufuatilii hayo yote. 1JZ na 2JZ engine zina matumizi makubwa kidogo ya mafuta kulinganisha na engine tulizozoea za kina Corolla na salon cars ndogo ndogo. Ndio maana tunalalamika. Vile demand kubwa ya used car ipo Africa, hizi gari zenye matumizi makubwa ya mafuta zinashuka bei saana sababu hatuziwezi. Wengi wetu kipato chetu ni kidogo.