Porsche wamezindua 4th generation ya Cayenne. Kwa kuanza, wameleta ya umeme tu na unaweza kuichaji Wireless!

Porsche wamezindua 4th generation ya Cayenne. Kwa kuanza, wameleta ya umeme tu na unaweza kuichaji Wireless!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Porche wamezindua generation ya nne ya Porsche Cayenne SUV.
IMG_8458.png

Ila cha kushangaza, wamezindua EV tu kwanza, bila kutoa ya mafuta wala hybrid. Ambayo hadi sasa hatujajua watazitoa baadae au ndio basi tena.
IMG_8457.png

Kwa ndani, mafundi simu na computer mtatajirika sana. Kwasababu jamaa wameleta display mbili kubwa za inch 14, moja kwa dereva (instrumental cluster), pia kuna inch 14 upande wa abiria wa mbele, kwa pamoja wanaziita flow display. Pia katikati kuna inch 12 OLED screen kwaajili ya infotainment na SC control.

Porsche pia wametoa specs, ikiwemo 1000hp, 0-100 km/h kwa sekunde 2.5 na top speed 250 km/h.

Battery lake ni 110 kWh, litakufikisha 600 km ukilijaza. Na utachaji 10-80% kwa dakika 15 tu, kutokana na 400 kW charging system.
IMG_8459.jpeg

Kama wewe chaja za cable sio mambo yako, kuna 11 kW wireless charging pads zimetangazwa pia.
IMG_8460.jpeg

Pad sio bei ndogo, ni karibia Mil 8 na bado kuna gharama za kuunganisha kwenye gereji yako.

Bei kamili ya Cayenne bado haijawa officially.
 
Picha yake bado naona ni camouflage au bado wabasubiri tarehe ramsi ya kuzindua ?
Hawa manufacturer wa ulaya bado wanapiga upepo kwenye EV ndiyo maana hilo toleo la Porsche wameona Bora waangalie Kwanza kwenye UMEME ili kama sokoni watashindwa kulipokea warudi kwenye hybrid na ICE
 
Wapuuzi wametoa za ndani tu. Nje wanabana sijui kwann.

Yeah wajanja hawaleti new model ya EV ila wanatengeza EV kutoka kule kule kwenye normal ICE au hybrid.
 
Back
Top Bottom