POSHO: Kuanzia Bungeni Hadi Kwenye Maandamano.. Watanzania na ulaji..

Nadhani tuna umaskini (wa kipato na usio wa kipato) miongoni mwa watu wetu, ambao unaambatana na aina fulani ya udumavu wa kifikra katika ngazi zote (kuanzia "mashinani" hadi ngazi za juu za uongozi). Wakati fulani nilialikwa kushiriki zoezi la kutafuta njia za kuwamotisha waalimu wa shule za vijijini, na tukafanya utafiti kutafuta mapendekezo kutoka kwa waalimu wenyewe walioko huko vijijini. Wengi walipendekeza kuwa wapatiwe semina mbalimbali, na walitaja hata vitu ambavyo wangependa kujifunza. Cha ajabu ni kuwa mafunzo hayo yalipoletwa, ushiriki wa siku ya kwanza ulikuwa mkubwa sana, lakini kuanzia siku iliyofuata mahudhurio yalidorora sana! Kisa? Hakukuwa na posho ya mafunzo! Kumbe wenzetu waliposema "semina" walimaanisha "posho"! Tulishangaa zaidi tulipofanya kikao na maafisa elimu, waratibu na wakuu wa mashule kuwapa ripoti ya kazi yetu, ulizuka ugomvi wanaulizia "kumbe kikao hiki hakina posho?" Tukawaambia jamani ndio maana tumefanyia ofisini kwenu (ukumbi wa halmashauri mojawapo), saa za kazi, ili pasiwepo ulazima wa malipo, hizi ni jitihada za kusaidia elimu hapa. Kwani kilieleweka kitu? Ajabu zaidi ni kuwa waliokuwa wanaongoza kudai posho kwa nguvu kama hawana akili nzuri ni maafisa wakubwa tu wa serikali waliokuwepo! Sasa hili jinamizi ni baya sana, mtu anataka asaidiwe kazi yake, na bado alipwe posho! Mwingine anataka asomeshwe halafu alipwe kusomeshwa! Katika nchi zilizoendelea watu hulipa hela nyingi tu ili wasome (continuing professional development), lakini kwetu wanataka "wahongwe" ndipo wasome! Na wakuu wa serikalini wanataka walipwe posho za ziada kufanya kazi zao za kawaida tena saa za kawaida za kazi!

Je tutafika? (naazima swali la Mzee Makwaia wa Kuhenga, sioni likijibika).
 

Mmhhh....haya bana...mi sio mutu wa mineno mingi...
 
Kithuku... nadhani hili linaanzia Bungeni.. kama Wabunge ambao wanafanya kazi ya kujadili mkutano ambao walichaguliwa kufanya katika muda uliopangwa kufanywa.. wanalipwa Posho ya kikao.. kwanini wafanyakazi wengine na wenyewe wasitake posho ya kufanya unacholipwa kufanya tayari?

Posho ya kikao kwa kweli ni posho ya wizi. Posho ambazo kwangu zinaingia akilini ni:

a. Posho ya Safari (kutoka mji na mji) au mtu anaposafiri. Hata hivyo anapoenda mahali ambapo gharama ya chakula, chumba, na usafiri vinagarimiwa na shirika hahitaji posho nyingine yoyote isipokuwa ya kujikimu kwa muda wa siku anazokuwa safari.
b. Posho ya Magari (kama mtu anatumia gari lake binafsi kwa ajili ya shughuli za kazi)
c. Posho ya Mazingira magumu (hii ni muhimu kwa wale wanaofanya kazi kwenye maeneo ambayo kwa kweli yana mazingira magumu) it is debatable.
 

Mzee Mwanakijiji,

Hoja nzuri lakini kwa hili la ATC na mashirika mengine yoyote yanayojishughulisha na biashara natofautiana na wewe!!! hio ni njia nyingine kwao kujitangaza... pole mzee naona mambo ya biashara kidogo sio upande wako.
 
hapana.. you missed the point.. yaani kujitangaza kwa kupeana posho ya maandamano?
 
Mbona Rais umemwacha? kwani hata yeye ni Fisadi na yeye ndio kiongozi mkuu wa Ufisadi nchi mwetu jamani

tena kaanzia chini kisha kaishia kwa waziri mkuu kama vile bongo ni UK ambako hakuna rais.
hongera babaH kwa kumkumbusha, tena ikiwezekana msisitize siku nyingine asijisahaulishe tena.
 
Mzee Mwanakijiji,

Hoja nzuri lakini kwa hili la ATC na mashirika mengine yoyote yanayojishughulisha na biashara natofautiana na wewe!!! hio ni njia nyingine kwao kujitangaza... pole mzee naona mambo ya biashara kidogo sio upande wako.

Kasheshe, rejea nilichoandika hapo juu our mind has been corrupted and our souls! sasa posho na biashara na kujitangaza yaani marketing inaingiaje hapa?! Naona biashara inkupiga chenga kweli! Hakuna kujitangaza wala nini, hii ni takrima.
 
Wakubwa washajua ukila na kipofu usimguse mkono, halafu mtupie vinyama virapurapu vidogo vile na yeye ajisikie anakula.

Ndiyo haya ya posho za maandamano.
 
Wakubwa washajua ukila na kipofu usimguse mkono, halafu mtupie vinyama virapurapu vidogo vile na yeye ajisikie anakula.

Ndiyo haya ya posho za maandamano.


that is a very good way of putting it..
 
hata mie nimependa hiyo methari yako pundit...ni ukweli mtupu hapo ndugu no comment
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…