Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

naingiwa na hofu ya kufikiri kuwa bunge karibu litakuwa above sheria ndani ya tanzania.
Wabunge kwa pamoja wanawawakilisha watanzania wote.Watanzania wote kwa pamoja au zaidi ya nusu ni above the law. Ni zaidi ya raisi ambaye alichaguliwa na wachache tu. Ni sahihi kwa sababu wananchi ndo wenye nchi. Wakiwa above the law basi hiyo ndo demokrasia siyo huyo kibaraka mmoja Hoseah awe above the law.Ameshidwa kazi na anangangania tuendelee kumlipa pamoja na huyo bosi wake raisi ambaye hana chochote lakini ataendelea eti "utamaduni"
 
Wabunge waonyesha jeuri
Wachukua nyingine mbili mpya jana
Sitta asema si haramu, ni takrima
Wapuuza vitisho vya Takukuru

Mapambano ya wabunge na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa juu ya upokeaji wa posho mara mbili jana uliingia hatua mpya baada ya kupokea posho hizo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Hatua hiyo si tu inaiweka Takukuru katika mazingira magumu zaidi juu ya hatua zake za kuwahoji wabunge kwa kuchukua posho mara mbili, ile wanayolipwa na Ofisi ya Bunge na za kwenye taasisi nyingine za umma wanakokwenda kufanya kazi, bali inaonyesha wazi kupuuzwa kwa harakati hizo za kuwadhibiti wabunge.
Jana mchana wabunge wakiwa wamekwisha kuhudhuria kikao cha asubuhi cha Bunge na kwa maana hiyo kuhalalisha posho zao kutoka Ofisi ya Bunge, walihudhuria semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo ili kujadili muswada wa sheria ya watoto.
Muswada huo unaoratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni Julai 31, mwaka huu.
Jana semina hiyo ilifunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, na ilihudhuriwa pia na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta, Manaibu Waziri na watumishi wengine wa Bunge.
Semina hiyo ililenga kuwaelimisha wabunge hao kuhusu muswada huo.
Kabla ya semina hiyo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu aliwatangazia wabunge kuwepo kwa semina hiyo na kusema ‘itifaki zote zimezingatiwa.'
Sitta alisema kuwa wabunge wamekuwa wakiandamwa kutokana na kulipwa posho nje ya Bunge, lakini akasema hiyo ni takrima na kwamba makundi mengine wakiwemo waandishi wa habari nao wanaipokea.
Wabunge waliohojiwa na Nipashe kuhusu kauli hiyo walisema ina maana pana, lakini yenye kubeba tafsiri ya huduma zote zinazohitajiwa kwa mwalika wa semina, ikiwemo makabrasha na posho.
Akifungua semina hiyo, Marmo alisema inatoa fursa muhimu kwa wabunge kuujua muswada huo kwa undani, hivyo kurahisisha mjadala pindi utakapofikishwa bungeni.
Marmo alisema kwa muda mrefu Tanzania haijakuwa na Sheria ya Watoto, hivyo muswada huo utasaidia kujenga na kufanikisha upatikanaji wa mazingira bora na haki kwa mtoto.
Alisema baada ya kusomwa kwake, muswada huo ulijadiliwa na wadau mbalimbali waliotoa maoni yao ambayo kwa kiasi kikubwa yatafanikisha azma ya kuwezesha kupatikana kwa haki za mtoto.
Wakati huo huo, habari zimetanda mjini hapa kuwa bado Takukuru wanaendelea kuwawinda baadhi ya wabunge machachari ili kuwahoji kabla ya kuwasilishwa bungeni taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali mjini Dodoma, zinaeleza kuwa baadhi ya wabunge ambao wamesimama kidete kuibana serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Richmond wamepelekewa taarifa za kujiandaa kuhojiwa na taasisi hiyo kuhusiana na kupokea posho nje ya vikao vya Bunge.
Mbunge mmoja ameiambia Nipashe kuwa tangu wiki iliyopita alitaarifiwa na Takukuru kuhusu mpango wa kumuita kumhoji, lakini akasema hadi sasa hajaitwa.
Alisema anashangaa hadi sasa kutoitwa na Takukuru, hatua ambayo alisema inalenga kudhoofisha mjadala wa Richmond baada ya kuwasilishwa bungeni Jumatano ijayo. Mbunge mwingine, ambaye naye ameeleza kuwa ataitwa kuhojiwa na Takukuru, alisema kitendo cha kuwaita na kuwahoji siku chache kabla ya kuwasilishwa na kujadiliwa kwa hoja ya Richmond, lengo lake ni kutaka kuwajengea hofu ili wasiweze kushiriki katika mjadala huo.
Baadhi ya wabunge ambao wamethibitisha kuhojiwa na taasisi hiyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shellukindo.
Shellukindo, ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) na kamati yake wamekuwa mstari wa mbele kuibana serikali itekeleze maazimio ya Bunge kuhusu Richmond hususan azimio linalotaka watendaji waliohusika kuipa zabuni ya kufua umeme wa dharura wa megawati 100 wa kampuni hewa ya Richmond wachukuliwe hatua.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye aliiongoza Kamati Teule ya Bunge kuchunguza uhalali wa zabuni ya Richmond, aliitwa kuhojiwa na Takukuru, lakini alikataa kufanya hivyo. Alipotakiwa kuthibitisha kuwepo kwa mpango huo, Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani, alisema jana jioni kuwa hakuwa katika nafasi ya kulitolea ufafanuzi suala hilo kwa kuwa yuko nje ya ofisi kutokana na ugonjwa.
Mbunge mwingine ambaye amehusishwa na mpango wa kuhojiwa ni Lucas Selelii, Nzega (CCM). Selelii ni mmoja wa wajumbe waliounda Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza zabuni ya Richmond.
Baadhi ya Wabunge na makundi mengine ya jamii wanaichukulia hatua ya Takukuru kuwa ina lengo la kulitisha Bunge ili lisiweze kuibana serikali ili iwachukulie hatua waliohusika na mkataba wa kitapeli ulioligharimu taifa kiasi cha Sh. bilioni 200 kuilipa kampuni ya Richmond na mrithi wake Dowans.
Kutokana na mlolongo wa matukio hayo, baadhi ya watu wanahoji uadilifu wa Takukuru inayoongozwa na Dk. Hoseah kuwahoji wabunge wakati hatma ya utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge haijajulikana.
Kashfa ya Richmond ilimlazimisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu Februari mwaka jana pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na mtangulizi wake, Dk. Ibrahim Msabaha.
Pamoja na mambo mengine maazimio ya Bunge yalitaka kuwajibishwa kwa watendaji wa serikali wakiwemo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah.

CHANZO: NIPASHE
 
Yaani ningekuwa RAISI ningemfuta kazi HOSEA!Kumbe yupo takururu sijui kwa ajili ya maslahi yake na si maslahi ya umma aka ya TAIFA
 
ngoja nishuke bustanini kwangu nikang'oe karoti na pilipili hoho .

huu upuuzi wa kina hosea sitaki kuusikia
 
Kabisa, jamaa anataka kuchanganya issue kupotosha maana halisi.
Tumeshtuka.
 
Siku ukisikia Dk. Kajiuzuru, ujue kalazimishwa. Angekuwa na dhamira hiyo angeondoka mara baada ya madudu ya Richmond kubainika
 


Kwanza, suala la wabunge kulipwa posho nyingine wanapozitembelea kikazi wizara, taasisi, mashirika ya umma na idara za serikali, ni suala ambalo limekuwepo kwa muda mrefu, linajulikana, limezoeleka na kuota mizizi. Hatua ya serikali kujifanya haijui kinachoendelea na hivyo kuamua kuiagiza TAKUKURU kuchunguza kitu kinachojulikana ni hatua ya kinafiki na kisanii.

Pili, kitendo hicho ni ghiliba kubwa dhidi ya Watanzania kwani kinalenga kuwaonyesha wananchi kuwa serikali yao inafanya uchunguzi juu ya wabunge kupewa fedha mara mbili mbili (fedha ya umma), wakati ukweli wa mambo ni kuwa serikali yenyewe ndiyo inayotoa posho hizo kwa wabunge kupitia wizara, idara, taasisi na mashirika ya umma, ambayo yapo chini yake.
Hapa serikali inafanya usanii, inaitumia TAKUKURU kuchunguza posho haramu zinazotolewa kwa wabunge wakati chanzo cha kutolewa kwa posho hizo ni serikali yenyewe na idara zake kuamua kuzitoa.
Ndiyo, wanasema baadhi ya wabunge wamekuwa wakidai posho hizo lakini ni vema ikaeleweka kuwa wabunge wamefikia hatua ya kudai posho hizo baada ya kuzoeshwa kupewa. Kwa upande mwingine, suala la wabunge kudai posho si hoja kwa sababu wizara, taasisi, au shirika husika bado lina uhuru wa kutosha wa kukataa kutoa posho hizo.
Tatu, uchunguzi huo hauna maana kwa sababu badala ya serikali kuitumia TAKUKURU kuendesha uchunguzi kuhusiana na posho hizo huku ikijua fika haina sheria inayokataza wabunge kupewa posho hizo, ilipaswa kwanza kutoa agizo kwa wizara, idara, mashirika ya umma na taasisi zote zinazofanya kazi na Bunge, linalopiga marufuku desturi hiyo ya kutoa posho kwa wabunge.
Nne, hata kama uchunguzi unaofanywa na TAKUKURU ungekuwa na maana basi uchunguzi huo haukupaswa kuanzia kwa wabunge, ulipaswa kuanzia kwa wizara, idara, mashirika ya umma na taasisi zinazotajwa kutoa posho hizo. Ulipaswa kuanzia kwenye chanzo na si kwenye matokeo.
Kwa mantiki hiyo, uchunguzi wote unaofanywa na serikali kupitia TAKUKURU, kwa kuwahoji wabunge, hauonekani kuwa na dhamira njema ya kunusuru fedha za umma zinazopotea kwa posho mbilimbili, bali unaonekana kuwa na malengo ya kisiasa dhidi ya wabunge, ambao baadhi yao tayari wameshakiri kupewa posho hizo.
Kama serikali ina nia ya dhati ya kunusuru pesa za umma zinazofujwa kwa kutoa posho mbilimbili kwa wabunge, basi inapaswa kuionyesha nia hiyo kwa kupiga marufuku na kuweka sheria shinikizi na iliyo dhahiri, inayokataza wabunge kupewa posho hizo mbilimbili, vinginevyo kinachofanywa hivi sasa na TAKUKURU ni kupoteza muda tu wa Watanzania. Ni usanii usio na tija, usanii huu mpaka lini?
Nachukua fursa hii kumtaka, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuzitaka wizara, mashirika ya umma, idara na taasisi zote zinazofanya kazi na Bunge, kuacha mara moja na kutothubutu tena kutoa posho kwa wabunge pindi wanapotembelewa na wabunge kikazi. Akitoa agizo hilo na kuweka mfumo ++++ TANZANIA DAIMA - nadhani wamesummarize vizuri kabisa
 
"there is life after PCCB" anasema Dr Hoseah-

Kazi nzuri kutambua hilo Dr Hosea lakini usicheze karata ya mbele ya life after PCCB.
Cheza karata ya sasa hivi, ya Richmond na uimalize.
Halafu wananchi hatutajali ukicheza karata ya Posho dabali dabali maana bado ni ufisadi.
Usikimbilie kutafakari maisha baada ya PCCB kabla ya kutatua hasa Richmond.
History will not take you kindly about this.
You might have realised now that you are a pawn in the whole chess game.
 
TANZANIA DAIMA .. wameelezea vizuri sanan hii issue ya posho mbili:

Hata hivyo pamoja na kupinga posho hizo mbili mbili wanazolipwa wabunge, pia siungi mkono hatua ya serikali kupitia TAKUKURU kuendesha uchunguzi (kuwahoji wabunge) kuhusiana na suala hilo; siungi mkono hatua hiyo ya serikali, nikitilia maanani yafuatayo: Kwanza, suala la wabunge kulipwa posho nyingine wanapozitembelea kikazi wizara, taasisi, mashirika ya umma na idara za serikali, ni suala ambalo limekuwepo kwa muda mrefu, linajulikana, limezoeleka na kuota mizizi. Hatua ya serikali kujifanya haijui kinachoendelea na hivyo kuamua kuiagiza TAKUKURU kuchunguza kitu kinachojulikana ni hatua ya kinafiki na kisanii.

Pili, kitendo hicho ni ghiliba kubwa dhidi ya Watanzania kwani kinalenga kuwaonyesha wananchi kuwa serikali yao inafanya uchunguzi juu ya wabunge kupewa fedha mara mbili mbili (fedha ya umma), wakati ukweli wa mambo ni kuwa serikali yenyewe ndiyo inayotoa posho hizo kwa wabunge kupitia wizara, idara, taasisi na mashirika ya umma, ambayo yapo chini yake.
Hapa serikali inafanya usanii, inaitumia TAKUKURU kuchunguza posho haramu zinazotolewa kwa wabunge wakati chanzo cha kutolewa kwa posho hizo ni serikali yenyewe na idara zake kuamua kuzitoa.
Ndiyo, wanasema baadhi ya wabunge wamekuwa wakidai posho hizo lakini ni vema ikaeleweka kuwa wabunge wamefikia hatua ya kudai posho hizo baada ya kuzoeshwa kupewa. Kwa upande mwingine, suala la wabunge kudai posho si hoja kwa sababu wizara, taasisi, au shirika husika bado lina uhuru wa kutosha wa kukataa kutoa posho hizo.
Tatu, uchunguzi huo hauna maana kwa sababu badala ya serikali kuitumia TAKUKURU kuendesha uchunguzi kuhusiana na posho hizo huku ikijua fika haina sheria inayokataza wabunge kupewa posho hizo, ilipaswa kwanza kutoa agizo kwa wizara, idara, mashirika ya umma na taasisi zote zinazofanya kazi na Bunge, linalopiga marufuku desturi hiyo ya kutoa posho kwa wabunge.
Nne, hata kama uchunguzi unaofanywa na TAKUKURU ungekuwa na maana basi uchunguzi huo haukupaswa kuanzia kwa wabunge, ulipaswa kuanzia kwa wizara, idara, mashirika ya umma na taasisi zinazotajwa kutoa posho hizo. Ulipaswa kuanzia kwenye chanzo na si kwenye matokeo.
Kwa mantiki hiyo, uchunguzi wote unaofanywa na serikali kupitia TAKUKURU, kwa kuwahoji wabunge, hauonekani kuwa na dhamira njema ya kunusuru fedha za umma zinazopotea kwa posho mbilimbili, bali unaonekana kuwa na malengo ya kisiasa dhidi ya wabunge, ambao baadhi yao tayari wameshakiri kupewa posho hizo.
Kama serikali ina nia ya dhati ya kunusuru pesa za umma zinazofujwa kwa kutoa posho mbilimbili kwa wabunge, basi inapaswa kuionyesha nia hiyo kwa kupiga marufuku na kuweka sheria shinikizi na iliyo dhahiri, inayokataza wabunge kupewa posho hizo mbilimbili, vinginevyo kinachofanywa hivi sasa na TAKUKURU ni kupoteza muda tu wa Watanzania. Ni usanii usio na tija, usanii huu mpaka lini?
Nachukua fursa hii kumtaka, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuzitaka wizara, mashirika ya umma, idara na taasisi zote zinazofanya kazi na Bunge, kuacha mara moja na kutothubutu tena kutoa posho kwa wabunge pindi wanapotembelewa na wabunge kikazi. Akitoa agizo hilo na kuweka mfumo wa ufuatiliaji, atakuwa ametusaidia kupiga hatua moja mbele katika kunusuru mabilioni ya fedha za Watanzania yanayotafunwa na viongozi huku Watanzania maskini tukizidi kuangamia.
 
Oho... ndipo inapokuwa hatari pale tunapomwona technoocrat akigeuka kuwa mwanasiasa... Hoseah anapiga tu porojo hapa, it's a game of CHICKEN... haya tuone who is going to chicken out.... but my feel when someone starts talking about life after PCCB, he knows the end of the game .... maana he has considered very deeply life after PCCB....
 
Kwa maneno aliyotoa Mr Hosea ni ya Kiburi tena yenye maana kubwa sana kwa Watanzania ,tena kiburi kibaya kabisa, Neno SI JIUZULU NGÒ then akaongezea THERE IS LIFE AFTER PCCB .
Kwa wenzangu na mimi walio ingia ndani kisaikologia wanaweza kungundua kwamba ,Hapa si Dr. Hosea aliye ongea,bali ana mwakilisha mtu.
Tunaomtaka Hosea kujiuzuru ni Watanzania na si wabunge kwani wabunge wanatuwakilisha sisi. Kwa maana hiyo hapa anajaribu kutu Kashfu..!!
 
nilisema mapema kwamba hana lolote analokuja kusema ila upupu tu......mpumbafu tu na yeye wala hatafia madarakani.
 
Hakuna kipya alichosema kwenye mkutano wake according to some news sources za hapo nyumbani.Cha kusubiri ni maamuzi ya Bunge hiyo Jumatano.Binafsi nisingependa Bunge liwe juu ya sheria lakini timing ya PCCB siyo nzuri kabisa na pia inaleta maswali mengi kuhusu nia na madhumuni yake.Ukweli ni kuwa Serikali haitakuja na majibu ya kuridhisha kwa mara nyingine tena.Mategemeo ya wengi yalikuwa Dr.Hosea atajiuzulu lakini haijatokea.Kiburi hichi si kidogo kwa sababu anajua anashikilia wapi kwenye serikali ya sasa.Nanukuu alichosema..."...there is life after PCCB..."

Kiburi hiki.....sijui!

Mungu atusaidie Tanzania.
 
Hosea ame-time vibaya, angesubiri kwanza Serikali iwasilishe taarifa yake bungeni. Sasa Luhanjo/Pinda kwa maelekezo ya JK wanaweza kum-suprise Hosea. Nasikia Taarifa hiyo itawasilishwa bungeni kesho. Pole sana Hosea, ubabe hauna maana.
 

Na wewe utakapobainika kuwa lile jumba (bangaloo) lako limejengwa huku ukiwa huna hicho kipato cha kulijenga kwa muda huo ndo utatambua kweli kuwa There's life after PCCB.
 
Daktari Hosea ameshaongea na waandishi leo hii.nimeona kwenye tv,hakuna lolote la maana zaidi ya kuongeza hasira za wadanganyika.
Na anasema kwamwe akosi usingizi kabisa na wala afikirii kujiuzulu.
kweli maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…