Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Hawa watu mbona wanafiki sana. Hivi wanataka kutuambia ni wabunge ndio wamekuwa wakidai wapewe posho hizo au ni taasisi zenyewe zinaamua kutoa? Kama mbunge kupokea posho hiyo ni kosa (rushwa?), kwa nini serikali kupitia taasisi hizi haziwajibishwi pia kwa kutoa rushwa hiyo? (Tunaambiwa hata takukuru pia imewahi kutoa posho hizo!).

Nadhani takukuru wangeanzia kwenye hizi taasisi (hususani takukuru yenyewe) ili kujua ni kwa nini wanatoa posho hizi huku wakijua fika kwamba wabunge tayari wanapewa posho na bunge.
 
ngoja ninywe chai kwanza, nchi hii bana!
 
Solution ni kuwafilisi sio kuwahoji kama ushahidi wa hizo posho za mara mbili mbili dhidi ya wabunge upo. Hao TAKUKURU nao wasijifanye miungu watu nao pia lazima wawajibishwe. Habari ya Richmond inachosha. Na Don Rostam anajua mwakani watamtafuta tena kwa hiyo lazima alindwe na asafishwe.

By the way kuna taarifa zisizokuwa rasmi/tetesi kwamba jamaa wa ikulu wamefukua pesa zilizokuwa zimefukiwa chini kwenye Ma -Sim tank huko Monduli na kuzirudisha serikalini.(sina uhakika nazo ila nazileta jamvini najua wapo wanaojua humu kuhusu hiyo ishu)
 
Mwakyembe Mwakyembe - Duh!
Hivi huyu jamaa anadhani yeye ni mkubwa sana kiasi cha kuwaona vijana wa TAKUKURU kuwa hawana uwezo wa kumhoji? How do you know someone is just a junior?

Kwani alitaka ahojiwe na Dr. Hosea mwenyewe au?? Mi naona inafika wakati hadi naona vitu vyote vinavyoendelea nchi hii ni maigizo tu!

Mungu Ibariki Tanzania
 


If true, that interview smacks of outright arrogance, snobbishness, insensitivity and conceit. For crying out loud, what "hadhi" does the Rt.Hon Speaker thinks he has? One to belittle a claim, regardless of its validity, of a misappropriation of public funds to the tune of TSh. 70 mil?

That's a lot of money and some respect of public finances will be appreciated.
 
Naendelea kujiuliza uwezo wa kufikiria wa watu walioko kwenye ofisi nyeti za nchi yetu ukoje. Hii ni mbinu nyingine ya kulizima bunge lisijadili hoja za rushwa serikalini. Kama kweli ikulu ina nia njema na nchi yetu, iache kuagiza vyombo vyake kufanya mambo yanayoonekana ni kinyume na interest za utawala bora.Hii ni mbinu nyingine ya kuzima wabunge midomo ila ni strategy ambayo kwenye zama zetu hizi haiwezi kufanya kazi maana ni kujitafutia aibu.People are well informed
 
Demusa!

Hold on kinachogomba hapa sio swala la nani ni mkubwa! Watz bwana? Akili za kupepea. Mh. Mwakyembe anasema kuna taratibu za kumhoji mtu anayetuhumiwa kudai/kupokea au kutoa rushwa. Kumpigia mtu simu na kumwita is one of the dragonian tactics za kutishia watu.

Hao vijana wa TAKUKURU walitakiwa kufuata utaratibu wa kumpelekea mtuhumiwa wito. Na kama hilo lingefanyika Dr. Mwakyembe akiwa ni mtaalam wa sheria asingeweza kuwakatalia. KWA KUMPIGIA SIMU ni kujaribu kumtisha and at this juncture left or right Dr. Mwakyembe remains right mpaka wampelekee summon ya kisheria.

Sasa kama sio danganya toto ya Dr. HOSEA kwa nini wasichukue hatua na kwenda kupiga porojo kwenye magazeti ambayo wamiliki wake ni watumwa wa ROSTAM & COMPANY. Kustaafu kwa Mwanyika kunatuachia mwanya wa kushughulikia mafisadi lakini bado yuko Feleshi ambaye ni Mtumwa wao. Ithink we need a change tupate DPP ambaye hana uhusiano na Don Andy Chenge the kin pin Mafioso. Akina Mwakyembe mkomae hao akina Mwanyika na Arthur lazima wafuate nyayo za Mramba na Mgonja pia ua vinginevyo patachimbika!!! Kama mtawasahau Karamagi na ile kashfa ya Buzwagi ,TICTS na Tanga Cement!!! sijui. Itabidi CCM watumie another 200bn mwakani kununua ushindi as in 2005.
 
we will know it all huyu Mwakyembe ni another generation ya mafisadi hana lolote makelele tu ..anapayuka kuhusu Richmond kumbe na yeye alikuwa na kampuni yake kwenye dili hizo hizo za umeme wa dharura..aaaahgggggg .asihojiwe yeye nani kwani?

Sikujua kama JF kuna watoto wa mafisadi kama wewe, naona mmeguswa mwaka huu inakula kwenu na baba zenu, kama Dr.mwakyembe ni fisadi wa umeme mbona hujamwambia baba yako fisadi ampeleke mahakamani, mwaka huu inakula kwenu.Watanzania wengine sijui mmezaliwa mwaka gani na siku gani, bado hamjaona wabunge wetu machachali wanafanya nini mpaka sasa hivi.Tuwasamee bure nyinyi watoto wa mafisadi lakini mwaka huu ni wa mwisho kwenu.
 
Mkuu hapo sijakupata kisawasawa,sijaisoma katiba kisawasawa,lakini mimi kama mwanajeshi nachojua mbunge anapigiwa saluti akiwa bungeni tu,na hii ni baada ya wenyewe kuidai sana.Pili nachojua Rais ni amiri jeshi mkuu,so ana mamlaka hata ya kumtuma askari mdogo akamkamate(sembuse kumhoji) mtu anayempigia saluti.Na nachoelewa pccb wako chini ya ofisi ya rais,so anaweza kuwaagiza wakamhoji mtu.Mwisho mkuu wangu kasome kwenye katiba madaraka ya huyu rais wa tz ndo utachoka alivyo na power.
 
Jamani, kilicho MUHIMILI ni BUNGE sio WABUNGE. Posho(rushwa) hizi wamezipokea nje ya BUNGE kinyume na taratibu. Sasa wanataka ziitwe TAKRIMA/UKARIMU ni mambo ya kijinga kwa kweli. BUNGE letu litaisimamiaje SERIKALI na TAASISI zake endapo kila wanakoenda wanahongwa kwa staili na mitindo tofauti?
 
Hapa ni suala la mipaka na kufanya kazi ovyo ovyo tu. Tangu lini suala la kupokea posho mara mbili mbili limekuwa rushwa? Kama lipo na likathibitika kuna taratibu za kufuata na si hii ya kuburuzana kwenda kuhojiana. Posho zote zinatolewa kwa kusainiana. Kuna tatizo gani kukusanya ushahidi huu bila kumhusisha mtuhumiwa maana nakala za malipo zitakuwepo katika ofisi husika? Kama ushahidi wanao wa mtu amesaini mara mbili kwa kazi hiyo hiyo basi ataarifiwe muajiri wake kwa hatua zaidi. Muajiri wake ndiye atakayemhoji mtuhumiwa na si Takukuru. Huku ni kupotezeana muda na kutafuta cheap popularity. Kwa kufanya walivyofanya wanaonekana vindictive badala ya wapigania haki.

Amandla.........
 
Uongozi wa nchi umekosa credibility. Dr. Hosea hana budi kuachishwa kazi kama kamati ya bunge ilivyobainisha ili kazi zifanyike. Sio kwamba wabunge hawataki kuhojiwa au kuchunguzwa. Issue ni kwamba anayewachunguza yuko madarakani kinyume cha sheria. Takukuru inatakiwa iwe nyeupe kama theluji ili iweze kupenya popote bila ya kisingizio chochote. Hata mimi wakija kwangu kujifanya wananichunguza nitawatoa bomba na mshale.

PCCB iko pale ku-serve interest za mafisadi au? Ni kwa nini order ya kuwahoji wabunge imetokea Ikulu? Hawajui kazi zao mpaka wapewe orders? Tunayeyushana tu, wabunge kataeni ujinga ujinga kama huu. Hosea aondolewe, PCCB isafishwe, mafisadi wote washtakiwe - then PCCB safi iendelee na kazi yake ya kuchunguza na kuhoji bila kinyongo, kisasi wala hofu.
 
Hii nchi hata sijui inaelekea wapi

2010 hiyoooooooooo mengi tutasikia na kuona
 
Hosea hawezi kubanwa wazee hapa midanganyika tunachezewa shere, kama order imetoka ikulu that means kuna watu wanjilinda na richmond jamani,hili linaonekana, sawa posho hizi ukufuatilia ni serikali yoote inafanya the same thing, nakumbuka nilishafanya kazi ya ukaguzi kipind flani, ukifika tu unapewa chakula, hotel, mapokezi 100% na mkiondoka kuna bahasha mbele ya safari utaifungua, hii ikawa ni mazoea yamekuwa tabia sasa!Wizarani mnakaa kikao the same office mnalipana sitting allowance!?one hr meeting?mh? so hapo IKULU wana jambo, kuna vigogo wanafunika kombe mjinga akatize.Nchi hii bado bado ssaaana tuu! long way to go! so tuwatoe tu madarakani ndo deal
 
Kwa kasi hii ya jamaa kukabana koo basi lazima nyumba iungue kwa maji ya moto .Sina comments ila naangalia sarakasi hizi .Ikulu imeamuru kama alivyosema Pinda kuhusu posho ila imeshindwa kuamuru kwenye mambo mengine ?
Hizi sarakasi zinatia Kinyaa maana wananch wasojua vizuri wanaweza kupotoshwa sana na baadae tukaendelea kuumia hii nchi.
Hivi ni mambo mangapi ya watu wasio katika madaraka yanafichwa na kukumbatiwa, halafu Mengine yanaibuliwa Ghafla na kufanyiwa Kazi. Ila hizi sarakasi zinatupeleka pabaya sana. Sijui hiyo mwakani itakuwaje, maana hadi sasa Maafisa kilimo hwaendi tena mashambani eti mafuta hamna, mishahara inachelewa huku pesa zingine zimefungiwa DECI maamuzi hayapo. Maamuzi ya kuwafunika midomo wabaya wa Ikulu yanafanyika haraka sana, TUTAFIKA?
 
Hivi mwajua kuwa Akina Mwakyembe wana hali mbaya sana, maana Lowasa Bado ni mtu mkubwa nchi hii,- wao wamemtibua adi akajiuzulu, Hosea naye yupo katikati ya JK ndo maana hamtoi- wao wameng'ang'ana kutaka awajibishwe- Pinda naye yupo katika kiti kilekile na hao jamaa, na hawezi kuchmoka.
JE, hAWA AKINA SPIKA NA MWAKYEMBE WATAKUWA WAPI MSIMU UJAO????
 

kWAKWELI MKUU HAPA SINA LA KUONGEZA HII IKULU Imekosa kazi na takukuru ni walewale wala si chombo kama kinavyotajwa. Ni uozo mtupu. HOSEA Kalindwa sana hivyo hajui hata kazi ya mwezi ujao ni ipi adi aambiwe. Docta mzima! Namsifu Mwakyembe ni Critical thinker. Watu inabidi tuwe tunahoji kabla ya kukubalitu eti hili latoka IKULU.
 

wananchi tutawachagua, acha woga wewe,huo ni mpambano mazee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…