Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Mkuu bambumbile bandiko lako linachosha kusoma huwezi weka paras?? mwe!!
 
Hapa ni suala la mipaka na kufanya kazi ovyo ovyo tu. Tangu lini suala la kupokea posho mara mbili mbili limekuwa rushwa? Kama lipo na likathibitika kuna taratibu za kufuata na si hii ya kuburuzana kwenda kuhojiana. Posho zote zinatolewa kwa kusainiana. Kuna tatizo gani kukusanya ushahidi huu bila kumhusisha mtuhumiwa maana nakala za malipo zitakuwepo katika ofisi husika? Kama ushahidi wanao wa mtu amesaini mara mbili kwa kazi hiyo hiyo basi ataarifiwe muajiri wake kwa hatua zaidi. Muajiri wake ndiye atakayemhoji mtuhumiwa na si Takukuru. Huku ni kupotezeana muda na kutafuta cheap popularity. Kwa kufanya walivyofanya wanaonekana vindictive badala ya wapigania haki.

Amandla.........

Ni kweli mkuu. Hilo suala ni dogo sana, ila kama alivyosema Mwakyembe, bila shaka lengo ni kuwadhalilisha wabunge wapiganaji ili waonekane hawana 'moral authority' ya kuzungumzia kashfa ya Richmond. Kwa nini mtu anayedaiwa kuchukua posho mara mbili ahojiwe na Takukuru? Mie nadhani Takukuru ina majukumu mazito zaidi, ikiwa ni pamoja na kuchunguza kashfa kubwa kama za KAGODA. Au Takukuru wanafanya kazi kwa maelekezo ya mafisadi?? Inashangaza sana!
 
Waheshimiwa Mramba na Yona walihojiwa na hatimaye wamefikishwa Mahakamani, hakukuwa na vikao vya kuwatetea maskini! Hawa "wapambanaji" wameguswa eti wanadai ni vitu vidogo na vimeanza siku nyingi! Wakumbuke kuwa 'two wrongs can not make a right!' Hivi kama ujambazi umeanza siku nyingi kwa hiyo sio tatizo kama ukifanywa sasa hivi? Kwani kosa la jinai lina expiry date jamani? Huyo Mwakyembe anahofia nini kuhojiwa kama anaheshimu sheria? Amesahau kwamba kinga haimhusu mhalifu? Hongera sana Pinda, wahojiwe hawa "wapambanaji!"
Mkuu Buchanan, Mramba na Yona hawakuhojiwa na TAKUKURU kwa tuhuma zozote wakiwa kama Wabunge. Bali walihojiwa kwa tuhuma zilizotokana nautendaji wao wakiwa viongozi wa serikali. Kuna utaratibu wa kufuata kuhoji waBunge.

Mkuu, ndani ya CCM ni dhahiri kuwa kuna mpasuko mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea katika historia ya chama hicho. Nadhani kuna wanasiasa wanaodhani kuwa kwa kuwakomoa wenzao, wao watapata nafuu ya kisiasa. Vinginevyo, nadhani wanadhani kuwa kama wao wataanguka kisiasa, basi waanguke na wengine wote. Ni siasa za hivyo hizo.

TAKUKURU wanatakiwa kuanza kuchunguza mambo hayo kwa kuanzia na mashirika ya serikali na kutoa mapendekezo ya kuzuia utaratibu huo badala ya kurukia wanaopokea (ambao sidhani kuwa huomba posho hizo).

Visasi vitaimaliza nchi, tuwe makini na wanasiasa wanaodhani kuwa kulipiziana visasi ndio njia ya kuonyesha uwezo wao kama viongozi.
 
Inaonyesha kuwa Wabunge hao huomba/hudai posho hizo. Angalia taarifa hizi za onyo amabzo zilitolewa mapema tu na Bunge lenyewe na Waziri Mkuu:

1. Toka kwa Katibu wa Bunge

"Wakati Sitta akitoa kauli tatanishi kuhusu barua iliyoandikwa na Kashillila kwenda kwa Hosea huku akisisitiza kutoifahamu, Tanzania Daima Jumatano imefanikiwa kuiona barua hiyo yenye kumbukumbu namba CEB.50/155/05/81 ikiwa na kichwa cha habari kinachosomeka "Baadhi ya Kamati za Bunge kuomba takrima serikalini na katika mashirika ya umma".

Sehemu ya barua hiyo inasomeka hivi" Tafadhali rejea mazungumzo kati ya Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Bunge kuhusu suala tajwa hapo juu.

"Nimepokea malalamiko kuhusu mwenendo usioridhisha wa Kamati za Bunge kuomba takrima kutoka kwa watendaji wakuu serikalini na mashirika yake wanapohojiwa na kamati za Bunge.

Hivyo ili kuepuka athari zaidi ilionekana kuwa ni busara jambo hili likatazamwa kwa kina ili kuainisha chimbuko lake linaanzia wapi, nani wahusika wakuu, hatua gani zichukuliwe na kwa utaratibu upi. (Rejea nyongeza ya nane ya kanuni za Bunge za toleo la 2007 kuhusu mgawanyo wa kazi wa kila kamati.)

Ni tegemeo langu kuwa suala hili utalipatia kipaumbele na kulitazama kwa unagalifumkubwa, kwa kuzingatia aina ya makundi yanayohusika na nafasi yake katika jamii na uongozi wa nchi, ili pamoja na kulitafutia ufumbuzi, bali pia kuwa makini katika kulishughulikia."

Barua hiyo pia imenakiliwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi na mkurugenzi wa Usalama wa Taifa.

2. Toka kwa Waziri Mkuu
Wakati Spika Sitta akikana kuiona barua hiyo (toka kwa PM), Tanzania Daima Jumatano imefanikiwa kuiona barua hiyo yenye kumbukumbu namba PM/P/2/567/33 yenye kichwa kinachosomeka "Malipo ya posho kwa wabunge wanapotembelea kikazi ofisi za serikali, taasisi na mashirika ya umma."

Sehemu ya barua hiyo inasomeka " Kwa muda mrefu sasa zimekuwepo taarifa mbalimbali kwamba baadhi ya kamati za Bunge zinapotembelea wizara, mikoa, taasisi za serikali na mashirika ya umma zinaomba au zinadai kulipwa posho mbalimbali. Posho hizo ni pamoja na posho za kujikimu, posho za kikao na takrima.

"Nimepewa taarifa kuwa wizara ambazo maofisa wahasibu walitakiwa kufanya malipo hayo ni pamoja na wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maji na Umwagiliaji, Afya na Ustawi wa Jamii, Maliasili na Utalii, Nishati na Madini, Kilimo, Chakula na Ushirika na Viwanda, Biashara na Masoko.

Nimeona ni busara nitoe taarifa hii kwako ili uweze kutumia njia zako za kiofisi kuwaasa waheshimiwa wabunge wachache wanaofanya hivyo waache, kwani mambo kama haya yanaweza kulipuka siku yeyote na yakalifedhehesha Bunge letu tukufu."

Barua hiyo ambayo imesainiwa na Waziri Mkuu mwenyewe, imenakiliwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo.

Barua hizo mbili zinaonyesha wazi kuwa Spika alionywa juu ya tatizo hili mapema lakini hakufanya lolote kutokana na uchu wa fedha.
 
hivi nyinyi mbona fikra zenu zinakua mgando hivi!!!?? hamjui kwamba ni lazima usafi wa nyumba uanzie chumbani ndo ufike hadi sebuleni!! kwa hiyo mlitaka rais atoe amri ya kuchunguza mambo ya nje kama RICHMOND na KAGODA wakati yanayomzunguka ya kamati za BUNGE bado! msimchoshe RAIS wetu, kazi kumlaumu tu, toeni solution ya lawama zenu, na si kukosoa tuuuuuuuu...
 
Huu ni ule ule upuuzi wa kutaka kutupoteza maboya. Wanadhani wakileta hiyo ya posho tutasahau Kagoda, Richmond, Meremeta, Deep Green nk.?
Kwanza hao hao wanaoidhinisha hizo posho bila kuwa zimepangwa kwenye bajeti na kupitishwa na Bunge lenyewe wanatakiwa wawajibishwe halafu waliozipokea wazirudishe na kupata onyo kali. Upuuzi wa kuanza kuandikiana barua za kusitisha mara moja ni kutowajibika kwa Ikulu kwa wananchi wake kama kawaida yake. Huu ni ulegevu ambao ndiyo umesababisha kushindwa kueleza umma ni nani mmiliki wa Kagoda. Ujinga mtupu upuuzi wa wazi kabisaaaa! Tumekaribisha viganga vya kienyeji Ikulu. Balaa kubwa kwa nchi.
 
Date::10/28/2009

Serikali yaibua hoja ya 'posho mbili' kuua kashfa ya

RichmondOfisi ya Rais Kikwete inadaiwa kushinikiza kuibuliwa hoja ya 'posho mbili' kufifisha kashfa ya Richmond kuendelea kuhojiwa bungeni.

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

SERIKALI imeshutumiwa kwa kuibua hoja ya 'posho mbili' kwa wabunge ili kuzima kashfa ya Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development (LLC) iliyobuni mkataba wa kifisadi kati yake na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Shutuma hizo zinakuja baada ya vyombo vya habari mbalimbali kutangaza jana msuguano uliojitokeza kati ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliyetoa hoja kusitishwa kwa wabunge kuhojiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusisitiza kuwa zoezi hilo litaendelea kwa sababu ni agizo kutoka katika Ofisi ya Rais, Ikulu.

Takukuru imekuwa ikiwahoji baadhi ya wabunge, wengi wao wakitajwa kuwa ni miongoni mwa wanaojipambanua katika kupiga vita ufisadi, kwa madai ya kupokea posho mara mbili, kufuatia malalamiko ya baadhi ya idara na taasisi kuwa kamati za Bunge zinadai posho mara mbili.

Sambamba na hoja ya 'posho mbili' za wabunge kwa kazi moja, kuendelea kujadiliwa katika nyanja mbalimbali za kijamii, pia mjadala mkali umekuwa ukiendelea katika mtandao maarufu wa 'wanajamii'.

Mchangiaji mmoja, Richard Mabala alisema anashangaa kuona serikali imeamua kuchagua kupambana na baadhi ya wabunge wakati suala la 'posho mbili' ni utamaduni wa miaka mingi bungeni.

"Mwaka juzi nilipotumwa kazi na wafadhili kuonana na kamati moja ya Bunge, vivyo hivyo walitengewa vijisenti vyao, wakiwemo mawaziri na mawaziri wastaafu ndani ya Bunge, mashirika ya jamii na wafadhili," ameandika.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa hiyo ya Richmond, juzi alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kusema kuwa kitendo hicho cha Takukuru ni cha kisasi na kuwa kamwe hatokubali kuhojiwa.

Jana Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Haji Duni alisema serikali inaogopa matokeo ya sakata la Richmond na inataka kutumia suala la wabunge kupokea posho mara mbili kama njia ya kutokea, baada ya kukwama kutekeleza maazimio ya Bunge kwa zaidi ya miezi sita sasa.

"Waziri Mkuu Mizengo Pinda na serikali yake anaogopa Richmond, anakazania wabunge wahojiwe kwa kuwa anaona hapo ndio mahali pa kutokea, wanajaribu kukwepa hoja ya msingi," alisema.

Alisema ikiwa serikali ina sura mbili moja ikiwa ya ufisadi na ndio sababu inachelea kuchukua hatua za wazi zilizopendekezwa na kamati ya Bunge kuhusu watendaji wake.

"Kama serikali ina sura mbili, moja ya kifisadi; ingekuwa makini ingewachukulia hatua wote kama ilivyopendekezwa na Bunge. Sasa inashangaza kwa kushupalia posho za wabunge na kuwahoji ikitafuta pa kutokea," alisema Duni na kuongeza:

"Kama serikali ipo makini kwa nini haijasema wazi ni nani waliorejesha fedha za EPA? Si kweli kama posho za wabunge ndiyo suala kubwa kwa sasa. Serikali iache unafiki kwani, kama posho si wabunge pekee hata watendaji wa serikali wanakula mara mbili."

Alisema, Pinda anajipapatua, huo ni unafiki wa serikali kutaka kufunika hoja ya Richmond na kwamba, kama wana umakini mbona waliorejesha fedha za EPA hawatajwi mpaka leo. Kama Takukuru wapo 'serious' (makini) kwa nini hawakulisemea hilo mwanzo wanasubiri wakati huu wa mkutano wa Bunge."

Aliongeza kuwa lililo mbele ni Bunge kuachiwa lifanye kazi yake na wabunge wafanye kazi yao na iwapo serikali kupitia Takukuru inahitaji kuwahoji basi isubiri kumalizika kwa mkutano wa Bunge.

Kauli hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF iliungwa mkono na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF) aliyesema kuwa ingawa hana tatizo na Takukuru kutekeleza wajibu wake, lakini hofu yake ni wakati gani inatekeleza wajibu huo na kama Bunge ambalo pia lina kanuni zinazoweza kufanyia kazi madai hayo limeshindwa kufanya hivyo.

"Ingawa sheria za nchi hazikatazi mtu kuhojiwa wakati wowote, lakini kila jambo lina wakati wake. Kama Takukuru imefanya hivyo ili kudhoofisha nguvu za wabunge kutetea maslahi ya taifa, basi wajue hakuna mtu yeyote anayeweza kulizuia Bunge kufanya kazi yake," alisema Hamad na kuongeza:

"Bunge lisizuiwe kufanya kazi yake. Hata kama litawavuruga wachache bado tutasimamia haki kwani waliobaki pia ni nguvu ya umma, kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi na wana nguvu na uwezo ule ule".

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewasihi wabunge wenzake kukubali kuhojiwa na Takukuru kama njia pekee ya kujisafisha mbele ya umma kuhusu tuhuma za kulipwa posho mara mbili kwa kazi moja.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake bungeni mjini Dodoma jana, alihadharisha kuwa endapo umakini na busara haitatumika katika suala hilo, kashfa hiyo inaweza kuliondolea Bunge heshima ambayo chombo hicho kimejijengea kwa wananchi.

“Sisi wabunge tunapopinga kuhojiwa na chombo cha dola tunatoa taswira mbaya kwa jamii…tunaweza kuharibu hii sifa tuonekane kuna mambo tunayafanya halafu tunajificha na kinga ya Bunge…kinga inatulinda kutoa maoni na michango yetu ndani ya Bunge tusishtakiwe,”alisema Zitto.

Katika mtazamo tofauti Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema anayachukulia mabishano hayo sawa na ya vibaka wawili wanaogombana kila mmoja akitaka kumuwahi mwenzake.

“Takukuru ni questionable (wanatuhumiwa) na wabunge nao pia ni ‘questionable’. Sasa imekuwa ni sawa na vibaka wawili ambao wanapambana na sasa inategemea ni kibaka yupi atamuwahi mwenzake.” alisema Mbatia.

Alifafanua kuwa katika mazingira ya sasa wabunge, wanatuhuma na wanapaswa kuchunguzwa na suala la Richmond nalo linapaswa kuchukua nafasi yake, hivyo Takukuru wasizuiwe kufanya kazi zao kama Bunge nalo lisivyotakiwa kuingiliwa.

Naye Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambaye pia ni kijana aliyeinukia kwa kasi kisiasa nchini katika miaka ya karibuni, Nape Nnauye, alisema anatilia shaka uhalali wa Takukuru kutekeleza kazi yao wakati huu wa Mkutano wa Bunge, hasa ikizingatiwa hoja nzito zinazotarajiwa kujadiliwa.

"Mazingira ya sasa tuna sakata la Richmond na bado halijaisha na mmoja wa wanaotuhumiwa ni Mkurugenzi wa Takukuru. Hata kama operesheni yao ni 'genuine' (halali) tunaweza tukafikiri ni kuzuia wabunge wasitekeleze wajibu wao," alisema Nnauye.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Malya alielezea kitendo hicho cha Takukuru kuwa ni cha kuwadhalilisha wabunge na kuongeza kama ni suala la kutolewa posho mara mbili kwa wabunge, Bunge kupitia kamati yake ya maadili lingeweza kujadili na kutoa ripoti.

"Tunaamini wabunge wetu wamekuwa wakijadili kwa uwazi mambo yote kwa maslahi ya umma. Suala hilo pia wangeweza kulifanyia kazi. Kitendo cha Takukuru kwenda kuwafuatilia mimi naona ni cha kuwashushia hadhi," alionya Usu.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dk Edward Hosea, ametia ngumu akitaka uchunguzi dhidi ya wabunge uendelee akisema : "Hakuna mtu aliye juu ya sheria."

Kauli hiyo ya kwanza ya Dk Hosea tangu kuanza uchunguzi huo ambao sasa umefikia hatua ya juu zaidi, inakuja kipindi ambacho tayari kumeibuka msuguano kati ya mihimili miwili ya dola, ambayo ni Bunge na Serikali.

"No one is above the Law..., no matter who are you (Hakuna aliye juu ya sheria, bila kujali wewe ni nani)," alisema Hosea na kuongeza: (What about Mafisadi?)

"Sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba, kwa hiyo hatuangalii nani ni nani zaidi ya sheria na katiba".

Mapema mwaka huu Dk Hosea alionya wabunge kwamba, wakianza mchezo wa kuumbuana hawatasalimika, kwani kumekuwa na taarifa na ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi wao wa kuchukua posho mara mbili.

Akionyesha kutimiza azma hiyo, Hosea alisema hapendi malumbano na wanasiasa kwani yeye si mwanasiasa mwenye jukwaa kama Bunge, ila atasimamia sheria.

"Wanaweza kusema mambo mengi, mimi si mwanasiasa sipendi malumbano na wanasiasa, wao wana audience (hadhara) mimi sina, wana Bunge na wanaweza kukaa bungeni na kuzungumza chochote," alifafanua Hosea na kusisitiza:

"Lakini kwa kifupi ni kwamba, msimamo wa Takukuru uko wazi, ni kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba basi, hakuna jambo jingine".

Alipoulizwa endapo uchunguzi huo una msukumo na nguvu za aina yoyote nje ya sheria na utendaji kazi wa kawaida wa Takukuru, alijibu: "Nasisitiza, sipendi malumbano na wanasiasa, wanaweza kusema mengi, lakini tunasimamia sheria tu".

Msuguano huo unaondelea kati ya mihimili hiyo miwili ya dola, pamoja na mambo mengine unaweza kuliingiza Bunge la Tanzania katika kashfa mbaya ya matumizi mabaya ya fedha za umma kama ilivyokuwa kwa Bunge la Uingereza.

Tayari hadi sasa, wabunge wengi wakiwa ni kutoka Kamati ya Nishati na Madini wakiongozwa na Shellukindo mwenyewe, wamekwishahojiwa kutokana na tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata, karibu wajumbe wote 21 kutoka Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma wamekwishaitwa kuhojiwa huku mwenyekiti wao Zitto akiwa njiani.

Baadhi ya wabunge kama James Lembeli wa Kahama na Dk Mwakyembe, walikwishaitwa kuhojiwa lakini hadi sasa hawajafanyiwa hivyo, huku mbunge huyo wa Kyela akiweka bayana kwamba, hayuko tayari kuhojiwa na Takukuru vinginevyo apelekwe mahakamani.

Baadhi ya wananchi waliliambia gazeti hili kwamba, hawaoni sababu ya wabunge kulalamikia kitendo cha Takukuru.

"Mjadala wa bunge hauwezi kuzuia mambo mengine yasifanyike... kama wabunge watashindwa kwa sababu tu ya kuhojiwa basi kazi yao watakuwa hawaijui. Na pengine hili litakuwa ni changamoto kwao," alisema Hamis Athuman. Imeandaliwa na Exuper Kachenje, Leon Bahati na Ramadhan Semtawa
 
Mwaka huu tutamjua tu fisadhi ni nani, ni mpaka kieleweke, hakuna mchezo!
 
Nilimwamini, nikamkubali, nikasema tumepata jasiri wa kusema kwa ajili ya wanyonge. Akaanza kwa mbwembwe za Speed and Standard,akatetea nyongeza ya Mishahara ya wabunge,akasemwa,akatulia!

Lakini kwa namna anavyoshughulikia swala la Richmond, halafu hashughulikii mengine kwa kasi hiyo, napoteza imani nae. Kama vile ana kisasi flani. Mbona kagoda haiundiwi tume? Meremeta? Tangold?

Mbona anatetea sana wabunge hata kwenye mambo ambayo yanaonekana wazi yanahitaji kuguswa?

Mbona ikiguswa ofisi yake anageuka mbogo? au milioni sabini ni hela za chai kwake? Haoni kama zingewaletea maji wamasai wa ngorongoro? Mbona ofisi yake ikiguswa anawaka wakati ye ndo kinara wa ufisadi?

kwa haya na mengine mengi, napoteza imani na huyu Bwana, nadhani ndo maana wakina EL na RA kila siku wanawaza kumpindua
 
Kuna makala moja imeandika kuwa RA alifadhili kampeni za huyu Bwana Jimboni na Katika kuutafuta uspika. . Hili linanifanya nijiulize mara mbili, ndio sababu Haishikii kagoda bango? au Kwa vile EL 'alimpiku' kwenye uwaziri mkuu 2005? Sipendi iwe hivi, bado namkubali Spika wangu, lakini napoteza Imani kabisa!
 
Serikali yaibua hoja ya 'posho mbili' kuua kashfa ya Richmond

kikwetecapaign.jpg

Ofisi ya Rais Kikwete inadaiwa
kushinikiza kuibuliwa hoja ya
'posho mbili' kufifisha kashfa
ya Richmond kuendelea
kuhojiwa bungeni.

SERIKALI imeshutumiwa kwa kuibua hoja ya 'posho mbili' kwa wabunge ili kuzima kashfa ya Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development (LLC) iliyobuni mkataba wa kifisadi kati yake na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Shutuma hizo zinakuja baada ya vyombo vya habari mbalimbali kutangaza jana msuguano uliojitokeza kati ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliyetoa hoja kusitishwa kwa wabunge kuhojiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusisitiza kuwa zoezi hilo litaendelea kwa sababu ni agizo kutoka katika Ofisi ya Rais, Ikulu.

Takukuru imekuwa ikiwahoji baadhi ya wabunge, wengi wao wakitajwa kuwa ni miongoni mwa wanaojipambanua katika kupiga vita ufisadi, kwa madai ya kupokea posho mara mbili, kufuatia malalamiko ya baadhi ya idara na taasisi kuwa kamati za Bunge zinadai posho mara mbili.

Sambamba na hoja ya 'posho mbili' za wabunge kwa kazi moja, kuendelea kujadiliwa katika nyanja mbalimbali za kijamii, pia mjadala mkali umekuwa ukiendelea katika mtandao maarufu wa 'wanajamii'.

Mchangiaji mmoja, Richard Mabala alisema anashangaa kuona serikali imeamua kuchagua kupambana na baadhi ya wabunge wakati suala la 'posho mbili' ni utamaduni wa miaka mingi bungeni.

"Mwaka juzi nilipotumwa kazi na wafadhili kuonana na kamati moja ya Bunge, vivyo hivyo walitengewa vijisenti vyao, wakiwemo mawaziri na mawaziri wastaafu ndani ya Bunge, mashirika ya jamii na wafadhili," ameandika.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa hiyo ya Richmond, juzi alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kusema kuwa kitendo hicho cha Takukuru ni cha kisasi na kuwa kamwe hatokubali kuhojiwa.

Jana Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Haji Duni alisema serikali inaogopa matokeo ya sakata la Richmond na inataka kutumia suala la wabunge kupokea posho mara mbili kama njia ya kutokea, baada ya kukwama kutekeleza maazimio ya Bunge kwa zaidi ya miezi sita sasa.

"Waziri Mkuu Mizengo Pinda na serikali yake anaogopa Richmond, anakazania wabunge wahojiwe kwa kuwa anaona hapo ndio mahali pa kutokea, wanajaribu kukwepa hoja ya msingi," alisema.

Alisema ikiwa serikali ina sura mbili moja ikiwa ya ufisadi na ndio sababu inachelea kuchukua hatua za wazi zilizopendekezwa na kamati ya Bunge kuhusu watendaji wake.

"Kama serikali ina sura mbili, moja ya kifisadi; ingekuwa makini ingewachukulia hatua wote kama ilivyopendekezwa na Bunge. Sasa inashangaza kwa kushupalia posho za wabunge na kuwahoji ikitafuta pa kutokea," alisema Duni na kuongeza:

"Kama serikali ipo makini kwa nini haijasema wazi ni nani waliorejesha fedha za EPA? Si kweli kama posho za wabunge ndiyo suala kubwa kwa sasa. Serikali iache unafiki kwani, kama posho si wabunge pekee hata watendaji wa serikali wanakula mara mbili."

Alisema, Pinda anajipapatua, huo ni unafiki wa serikali kutaka kufunika hoja ya Richmond na kwamba, kama wana umakini mbona waliorejesha fedha za EPA hawatajwi mpaka leo. Kama Takukuru wapo 'serious' (makini) kwa nini hawakulisemea hilo mwanzo wanasubiri wakati huu wa mkutano wa Bunge."

Aliongeza kuwa lililo mbele ni Bunge kuachiwa lifanye kazi yake na wabunge wafanye kazi yao na iwapo serikali kupitia Takukuru inahitaji kuwahoji basi isubiri kumalizika kwa mkutano wa Bunge.

Kauli hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF iliungwa mkono na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF) aliyesema kuwa ingawa hana tatizo na Takukuru kutekeleza wajibu wake, lakini hofu yake ni wakati gani inatekeleza wajibu huo na kama Bunge ambalo pia lina kanuni zinazoweza kufanyia kazi madai hayo limeshindwa kufanya hivyo.

"Ingawa sheria za nchi hazikatazi mtu kuhojiwa wakati wowote, lakini kila jambo lina wakati wake. Kama Takukuru imefanya hivyo ili kudhoofisha nguvu za wabunge kutetea maslahi ya taifa, basi wajue hakuna mtu yeyote anayeweza kulizuia Bunge kufanya kazi yake," alisema Hamad na kuongeza:

"Bunge lisizuiwe kufanya kazi yake. Hata kama litawavuruga wachache bado tutasimamia haki kwani waliobaki pia ni nguvu ya umma, kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi na wana nguvu na uwezo ule ule".

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewasihi wabunge wenzake kukubali kuhojiwa na Takukuru kama njia pekee ya kujisafisha mbele ya umma kuhusu tuhuma za kulipwa posho mara mbili kwa kazi moja.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake bungeni mjini Dodoma jana, alihadharisha kuwa endapo umakini na busara haitatumika katika suala hilo, kashfa hiyo inaweza kuliondolea Bunge heshima ambayo chombo hicho kimejijengea kwa wananchi.

"Sisi wabunge tunapopinga kuhojiwa na chombo cha dola tunatoa taswira mbaya kwa jamii tunaweza kuharibu hii sifa tuonekane kuna mambo tunayafanya halafu tunajificha na kinga ya Bunge kinga inatulinda kutoa maoni na michango yetu ndani ya Bunge tusishtakiwe,"alisema Zitto.

Katika mtazamo tofauti Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema anayachukulia mabishano hayo sawa na ya vibaka wawili wanaogombana kila mmoja akitaka kumuwahi mwenzake.

“Takukuru ni questionable (wanatuhumiwa) na wabunge nao pia ni ‘questionable’. Sasa imekuwa ni sawa na vibaka wawili ambao wanapambana na sasa inategemea ni kibaka yupi atamuwahi mwenzake.” alisema Mbatia.

Alifafanua kuwa katika mazingira ya sasa wabunge, wanatuhuma na wanapaswa kuchunguzwa na suala la Richmond nalo linapaswa kuchukua nafasi yake, hivyo Takukuru wasizuiwe kufanya kazi zao kama Bunge nalo lisivyotakiwa kuingiliwa.

Naye Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambaye pia ni kijana aliyeinukia kwa kasi kisiasa nchini katika miaka ya karibuni, Nape Nnauye, alisema anatilia shaka uhalali wa Takukuru kutekeleza kazi yao wakati huu wa Mkutano wa Bunge, hasa ikizingatiwa hoja nzito zinazotarajiwa kujadiliwa.

"Mazingira ya sasa tuna sakata la Richmond na bado halijaisha na mmoja wa wanaotuhumiwa ni Mkurugenzi wa Takukuru. Hata kama operesheni yao ni 'genuine' (halali) tunaweza tukafikiri ni kuzuia wabunge wasitekeleze wajibu wao," alisema Nnauye.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Malya alielezea kitendo hicho cha Takukuru kuwa ni cha kuwadhalilisha wabunge na kuongeza kama ni suala la kutolewa posho mara mbili kwa wabunge, Bunge kupitia kamati yake ya maadili lingeweza kujadili na kutoa ripoti.

"Tunaamini wabunge wetu wamekuwa wakijadili kwa uwazi mambo yote kwa maslahi ya umma. Suala hilo pia wangeweza kulifanyia kazi. Kitendo cha Takukuru kwenda kuwafuatilia mimi naona ni cha kuwashushia hadhi," alionya Usu.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dk Edward Hosea, ametia ngumu akitaka uchunguzi dhidi ya wabunge uendelee akisema : "Hakuna mtu aliye juu ya sheria."

Kauli hiyo ya kwanza ya Dk Hosea tangu kuanza uchunguzi huo ambao sasa umefikia hatua ya juu zaidi, inakuja kipindi ambacho tayari kumeibuka msuguano kati ya mihimili miwili ya dola, ambayo ni Bunge na Serikali.

"No one is above the Law..., no matter who are you (Hakuna aliye juu ya sheria, bila kujali wewe ni nani)," alisema Hosea na kuongeza:

"Sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba, kwa hiyo hatuangalii nani ni nani zaidi ya sheria na katiba".

Mapema mwaka huu Dk Hosea alionya wabunge kwamba, wakianza mchezo wa kuumbuana hawatasalimika, kwani kumekuwa na taarifa na ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi wao wa kuchukua posho mara mbili.

Akionyesha kutimiza azma hiyo, Hosea alisema hapendi malumbano na wanasiasa kwani yeye si mwanasiasa mwenye jukwaa kama Bunge, ila atasimamia sheria.

"Wanaweza kusema mambo mengi, mimi si mwanasiasa sipendi malumbano na wanasiasa, wao wana audience (hadhara) mimi sina, wana Bunge na wanaweza kukaa bungeni na kuzungumza chochote," alifafanua Hosea na kusisitiza:

"Lakini kwa kifupi ni kwamba, msimamo wa Takukuru uko wazi, ni kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba basi, hakuna jambo jingine".

Alipoulizwa endapo uchunguzi huo una msukumo na nguvu za aina yoyote nje ya sheria na utendaji kazi wa kawaida wa Takukuru, alijibu: "Nasisitiza, sipendi malumbano na wanasiasa, wanaweza kusema mengi, lakini tunasimamia sheria tu".

Msuguano huo unaondelea kati ya mihimili hiyo miwili ya dola, pamoja na mambo mengine unaweza kuliingiza Bunge la Tanzania katika kashfa mbaya ya matumizi mabaya ya fedha za umma kama ilivyokuwa kwa Bunge la Uingereza.

Tayari hadi sasa, wabunge wengi wakiwa ni kutoka Kamati ya Nishati na Madini wakiongozwa na Shellukindo mwenyewe, wamekwishahojiwa kutokana na tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata, karibu wajumbe wote 21 kutoka Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma wamekwishaitwa kuhojiwa huku mwenyekiti wao Zitto akiwa njiani.

Baadhi ya wabunge kama James Lembeli wa Kahama na Dk Mwakyembe, walikwishaitwa kuhojiwa lakini hadi sasa hawajafanyiwa hivyo, huku mbunge huyo wa Kyela akiweka bayana kwamba, hayuko tayari kuhojiwa na Takukuru vinginevyo apelekwe mahakamani.

Baadhi ya wananchi waliliambia gazeti hili kwamba, hawaoni sababu ya wabunge kulalamikia kitendo cha Takukuru. "Mjadala wa bunge hauwezi kuzuia mambo mengine yasifanyike... kama wabunge watashindwa kwa sababu tu ya kuhojiwa basi kazi yao watakuwa hawaijui. Na pengine hili litakuwa ni changamoto kwao," alisema Hamis Athuman.

Source: Mwananchi 10/29/2009
 
  1. Kama TAKUKURU wakiw wanafanya kazi ya kufuatilia wanaolipwa kimakosa au kugushi risiti wangapi watapona huko serikalini, including waajiriwa wa hapo TAKUKURU?
  2. Kama posho mara mbili ni rushwa ya kufuatiliwa na TAKUKURU, kwa nini TAKUKURU wasiombe kuongezewa watumishi kwa maelfu na kupangishiwa jengo kubwa kama la Kitega Uchumi, ili waweze kufuatilia viji-posho vya watumishi serikalini na local gov zake?
Kwa kifupi ni kuwa TAKUKURU sasa ni kiboko cha Ikulu cha kuadhibu wale wasioafikiana nao.

Waheshimiwa wabunge ningewaomba mtengue sheria inayounda TAKUKURU ili ife.
 
Ndugu zangu lazima kila kitu kiwe na mwanzo wake. Kama kuna udanganyifu unafanywa na wabunge uanikwe na ukemewe. Kama wabunge is mafisadi kwanini wagushi risiti? Kwanini walipwe mara mbili kwa kazi moja? Wanaosema kwamba ni kwa sababu ya wao kuibana serikali kuhusu Richmond haina mantiki yoyote. Wote wanaohisiwa wahojiwe na wale watakaokua na hatia warudishe hizo hela zetu na wengine ikibidi waburuzwe mahakamani. Baadhi ya wabunge wanaficha maovu yao kwenye kivuli cha kupambana na ufisadi.
 
Kuna makala moja imeandika kuwa RA alifadhili kampeni za huyu Bwana Jimboni na Katika kuutafuta uspika. . Hili linanifanya nijiulize mara mbili, ndio sababu Haishikii kagoda bango? au Kwa vile EL 'alimpiku' kwenye uwaziri mkuu 2005? Sipendi iwe hivi, bado namkubali Spika wangu, lakini napoteza Imani kabisa!

Swala la Kagoda lipo kwa DPP pamoja na lile la Malegesy Lawa Chambers. Bunge haliwezi kuingilia swala ambalo linashugulikiwa na taasisi nyingine ya serikali. Kama Sitta angekuwa amefadhiliwa kwenye kampeni na RA unavyodai basi watu hawa wawili wasingekwa maasimu wakubwa kisiasa wakati huu.

Unajua unaweza kumla tembo lakini kwa kumla vipande vipande. Ukitaka kulazimisha kumla mzima mzima hutaweza. Ukisema kwa nini Bunge lisichunguze Tangold na Meremeta wakati hili la Richmond halijaisha ni sawa na kumla 'tembo" mzima mzima na hilo haliwezekani. Mambo yote makubwa na mazuri uchukua muda na hivyo huna haja ya kukata tamaa na kukosa imani na Spika wako.
 
Asiyejua jambo haambiwi jambo, jaribu pale unapopata nafasi kuwa unasoma vitabu vya sheria.

La kagoda kamuulize JK na ile Task Force yake.

Labda ikiwa una agenda ya siri na Bwana spika uiweke bayana
 
Ni unafiki wa pande mbili hila napenda unapoelekea ktk haya yanayoendelea itawaamsaha na wazembe wengine wanaojitia wao wapo kati.

Sawa sawa kwa sisi watanzania ambao atuna side ya kisiasa bali maendeleo ya jamii na uwajibika wa viongozi hili ndilo linalo hitajika. Na wenye makosa wafungweu tu including Mwakyembe.

Hawa jamaa wa kambi nyingine ni wadhaifu Lowassa sasa ana waonesha talk is cheap, kama yeye(6) alikua anaichukulia issue ya Richmond personal na Lowassa anaelewa kuna issue zingine ambazo anazi ignore.

Ni bora nichukue upande wa mtendaji (Lowassa) seriously, sasa along the way amilizi maadui tu bali na wabunge wajinga wajinga. Sawa sawa cowards kama hawa si wapiganaji vinginevyo wangesha muambatanisha na hiyo Richmond.

We actually huyu sitta ulimuona hero.
 
agenda kubwa kwa spika sita ni kuwapendeza wabunge kwa maslahi. mishahara, posho, fungu la la majimbo nk. sasa pia anapigia debe posho mbili mbili na kuziita ukarimu wa kiafrika. masikini kukarimu matajiri kwa posho za kimtindo ambazo nazo kwa kawaida ni zaidi ya posho za bunge.

kwa kuwapendelea wabunge kwa maslahi yao binafsi anadhani hawezi kung'olewa ubunge.

macinkus
 
Back
Top Bottom