Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Kuna mambo yako wazi sana wala hayahitaji rocket science kujua kwamba hawa wanasiasa wamejifavor wao, ukitumia hesabu za kawaida kabisa unaona lengo lilikuwa kujilipa vizuri wao na sio watumishi wa umma.
Watumishi ambao wanalipwa kima cha chini nchi hii ni wachache sana, hata wale wa daraja la kati pia ni wachache.
Asilimia kubwa ya watumishi wa umma wapo kwenye UALIMU na AFYA. Sasa ukiangalia haya makundi, wengi mishahara yao inaanzia kwenye 720,000/=. Hawa wa kwenye hili kundi wameongezewa 55,000/= ambayo ni ghafi, ukishatoa makato take home inakuwa kama 20,000/= hivi.
Watumishi hawa wanaoitwa wa kima cha chini ni wachache sana, yani walioongezewa 70,000/= ni wachache sana unaweza kukuta hawafiki hata 10% ya watumishi wote na ndio maana kilio cha nyongeza ndogo kilikuwa na mshindo mkubwa sana. Siyo kama WM alivyotuambia eti kelele zilikuwa zinatoka kwa wanaolipwa vizuri. Kelele zilikuwa nyingi sababu kundi kubwa limeongezewa ongezeko ghafi lisilozidi 50,000/= ambalo baada ya makato unaondoka na kiasi kiduchu sana.
Wakati huohuo wakaongeza viwango vya posho mara 2. Hii yote ni kwa sababu wanajua itawahusu wao zaidi. Ni wao ndiyo wenye safari nyingi, ni wao ndiyo wenye vikao vingi nk. Mtumishi wa kawaida mpaka aje apate nafasi ya safari siyo mchezo, labda kipindi cha mei mosi.
Hili ndiyo kundi lililoongezewa 20,000/=, lakini wanajua watacompesate kwenye posho. Halafu eti WM anasema hili kundi ndilo walilokuwa wanapiga kelele? Wapige kelele kwa kipi wakati posho zao tuu zinawafanya wasiiguse mishahara yao?