Posho za wabunge zapanda kimyakimya!

Tumepata tulicholipia! Si mliwachagua wenyewe sasa mwalalama nini?
Anyway...na zile nyumba walizokuwa wanajengewa zimefikia wapi?
UBUNGE NI BONGE LA DILI!

Sasa wewe ulitaka watu wasichague wabunge? Kumbuka hii siyo ishu ya CCM au Chadema, kila mbunge anakula posho sawa ya bunge.
 

Wana JF,
Nikitizama kwa makini nakuja kugundua hali ya umaskini na hali ya ugumu wa maisha katika taifa hili inasikitisha sana na halii hii inavyo endelea ni kuwafanya watanzania kuwazia kuwa ukiwa kiongozi serikalini kwenye siasa kama mbunge diwani mayor ni ulaji mzuri na wananchi wanawazia hilo kumbe wana sahau kuwa uongozi huo au nyadhifa hizo ni kuwajibika kwa jamii iliyo kuteuwa kuwa hapo na unapewa dhamana ya kusimamia shughuri zote na utekelezaji wake wote kwa wananchi na kuleta maendeleo katika jamii hiyo.

Kuwepo na mfumo mbaya au usimamiaji mbovu au uongozi potofu na duni wa viongozi walio pewa dhamana ya wananchi kumeleta ugonjwa mbaya sana wa kila mtanzania kufikilia kuwa ukiwa kiongozi katika nyadhifa nilizo zitaja ni kuukimbia umaskini hii inatujengea nini watanzania. ??? wananchi wote tumekodolea hiyo mishahara kwanini hakuna chochote bunge linacho kifanya linasimami nini kuhusu serikali??? Maisha ya wananchi bunge linalo simamia hiyo serikali ni magumu kupita maelezo serikali imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei ya vyakula nchini wananchi hawajui wale nini kesho?

Nchi zingine mkate ukipanda bei tu watu wako barabarani kupinga ongezo la bei nchi hii mkiingia barabarani police waja na mabomu alafu JK anasema nchi hii sio ya ki dectetor ???? wapi na wapi jamani


 
Kwa hiyo hadi Dr Lusinde Livingstone na Profesa Majimarefu watakuwa wanalamba hiyo pesa?! Duu 'ITS NOT FAIR'
 
Tanzania hatuwezi kuondokana na huu umaskini, kama tukiendelea kuongozwa na hawa viongozi walafi.
 
Sasa! pesa zote hizo mbona bado wapo wanaosinzia? ni aibu!!
Na mkumbuke wabunge hawazalishi chochote zaidi ya maneno ambayo nayo vilevile hawaelewani.Du! Mungu tunusuru!!!!
 
Halafu bado wanawalipa wenzao 100,000 kwa mwezi,pia na walimu wanaambiwa wasubiri kwanza serikali haina pesa.............ipo siku tutapigana risasi for greater good of the nation.
 
Wabunge hawana uchungu na watanzania, kweli nimekubali "mwenye nacho huongezewa".

Ok! Tanzania ni nchi maskini, sawa. Kwanini hiki kidogo tulicho nacho tusigawane kwa uwiano sawa. Kwanini wao wanajimegea kipande kikubwa ilihali wanajua kuwa tupo wengi tunaotegemea hicho kipande?.

Wanafunzi wangapi wa vyuo vikuu wamekosa kuripoti chuo kwa kukosa mikopo. Kwanini bunge lisingewafikiria hawa nao, japo nao wapate mgao kidogo. Je gharama za maisha zimepanda kwa wabunge tu au watanzania kwa ujumla?. Ugumu wa maisha unawahusu wabunge tu?.

Shule ngapi za kata hazna madawati, wanafunzi wanakaa chini. Je wabunge hili hawajaliona?.

Inasikitisha kuwa ubunge tena si kwa ajili ya kumwakilisha mtanzania bali kwa sasa imekuwa ni biashara.

Hebu we mbunge jifikirie, utajisikia faraja kupata posho ya 330,000/=@ sikuwa wakati kuna kundi kubwa la wapiga kura wako wanaishi chini ya dola moja.
Kipi kilicho washawishi kupandisha posho 154%?. Kama mnaona sifa tuongezeeni basi na sisi mishahara walau kwa 100% kwani hata hukvu kwetu gharama za maisha zimepanda.


Mungu awalaani nyote na familia zenu.
 
Hili ongezeko watalifidia vipi wakati bajeti imeshapita?. Huu ni uhuni.
 
duh, na mimi naanza kampeni kabla ya wakati niingie mjengoni 2015 muhula mmoja tu unanitosha.
 
 
Hili ongezeko watalifidia vipi wakati bajeti imeshapita?. Huu ni uhuni.


Mhhhh! Sikutegemea kusoma bandiko kama hili toka kwako hasa ukitilia maanani ulivyo mtetezi mkubwa wa magamba hapa jamvini. Mimi nimeguswa na msimamo wa huyu Makamba.

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Makamba ashtushwa
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, alieleza kushangazwa na ongezeko hilo la ghafla akisema kamwe wabunge wasifikiri kuwa wanaweza kumaliza matatizo yao au ya wapigakura wao kwa fedha ya posho.
Alisema kitendo cha wabunge kuongezewa posho za vikao kwa asilimia 185.7, kinaleta jazba kwa wananchi ambao wanahangaika kila kukicha kwa ugumu wa maisha.

"Kwenye jamii lazima kuwe na usawa, kama watu tupo kwenye hali mbaya (ugumu wa maisha) lazima wote tuenende sawa. Wabunge kuongezewa posho kwa asilimia 185 siyo sawa kabisa, tunajiweka mbali na wananchi na wanatuona tunafaidika sana wakati wao wanateseka kwa ugumu wa maisha," alisema Makamba.

Alisema kuwa, kutokana na msimamo wake huo, Juni mwaka huu alikataa posho iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini baada ya kuhudhuria semina iliyoandaliwa na wizara hiyo.

"Tulikaa kwenye semina kwa saa mbili, tunamaliza naletewa karatasi nisaini posho ya Sh280,000. Nilikataa. Nilikataa kwa sababu nilitambua kuwa ile ni kazi yangu kama mbunge, sasa unanilipa hela ya kazi gani?" alihoji Makamba.

SOURCE: Mwananchi


 
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema walivyokuwa wakipinga posho hizo wakati zilivyokuwa Sh70,000 waandishi wa habari walichukua suala hilo kama ajenda ya Chadema, hivyo kupandishwa kwa posho hizo ni matokeo ya watu kuwapuuza walivyokuwa wakizipinga.
 
naomba kujua hivi wabunge wakikataa hizi posho (eg ZITTO & MAKAMBA) pesa zinapelekwa wapi

maana kwenye halmashauri zetu mtu asipo chukua haki yake kuna uwezekano mkubwa sana watu kuzichuka na ku"sign''
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Posho za wabunge zazua mjadala
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 28 November 2011 21:26
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe

Waandishi Wetu
NYONGEZA ya posho za wabunge imewakera wasomi, wanasiasa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(Tucta) ambao kwa nyakati tofauti jana, walieleza kutoridhishwa na hatua hiyo.Posho za vikao vya wabunge imeongezeka kutoka Sh70,000 kwa siku walizokuwa wakilipwa awali, mpaka Sh200,000 fedha ambayo ilianza kulipwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita.

Kutokana na ongezeko hilo, kwa sasa kila mbunge atakuwa akilipwa Sh80,000 kama posho ya kujikimu anapokuwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao (sitting allowance) Sh200,000 na mafuta ya gari Sh50,000 kila siku sawa na Sh 330,000 kwa siku.

Nyongeza hiyo ya posho za vikao imefanya bajeti ya Bunge kwa ajili ya posho za vikao kufikia Sh28 bilioni kwa mwaka.

Zitto adai ni usaliti
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alisema kuwa ameshtushwa na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa wabunge huku wananchi wakiugulia ugumu wa maisha na kusema kuwa ipo siku Watanzania watawapiga mawe kwa usaliti huo.

"Nimeshtushwa zaidi kwamba posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua, maana maslahi yote ya wabunge huamuliwa na Rais baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge," alisema Zitto.

Aliwataka wabunge wote kutambua kwamba, kuamua kujipandishia posho bila kuzingatia hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano.

"Mbunge yeyote ambaye anabariki jambo hili labda anaishi hewani, haoni taabu za wananchi au ni mwizi tu na anaona ubunge ni kama nafasi ya kujitajirisha binafsi," alisema Zitto.

Aliwataka pia wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni wa chama na ni wa kisera.
"Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi," alisema Zitto.

Alisema kuwa amemwomba Katibu Mkuu wa chama chake kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hilo.
Alisema kuwa tangu Juni 8 mwaka huu, alikataa kupokea posho za vikao na kuwa, popote anapohudhuria vikao huwa anaomba risiti za posho anazokataa.

"Baadhi ya wabunge kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho," alisema Zitto.
Alieleza kwamba anampongeza Makamba kwa uzalendo wake na kuwataka wabunge wengine wenye moyo wa dhati kukataa siyo tu ongezeko la posho bali posho yote ya vikao.
" Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa? Tazama nchi hii, juzi Serikali ilipokea msaada wa Sh20 bilioni kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa Sh28 bilioni kama posho ya kukaa tu kwa mwaka," alisema Zitto.
Tucta wawaka

Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema kitendo cha wabunge hao kujiongezea posho ni ishara ya kushindwa kutetea maslahi ya wananchi wao waliowapeleka bungeni.

"Tucta inalaani kitendo cha wabunge kujiongezea posho kubwa kama hizo huku wakijua kuwa wananchi waliowachagua wanawategemea wao, hasa katika kipindi hiki kigumu cha maisha. Jambo hilo linaonyesha wazi kuwa hawako kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi, bali kujinufaisha wenyewe," alisema Mgaya.

Alisema wabunge hao wameshindwa kujali hali ya wananchi wao hasa katika kipindi hiki cha mfumuko wa bei, hali ngumu ya maisha na migongano ya hapa na pale, badala yake wameamua kujipigia debe ili waweze kunufaika wenyewe. "Nasema hawafai, huu ni unyonyaji,"alisema.

AlisemaTucta inapinga kitendo hicho na imeitaka Serikali kuangalia upya suala la posho ili kusiwe na matabaka kati ya wabunge na wafanyakazi wengine ambao ndio msingi wa uchumi wa taifa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema uamuzi wa kuongeza posho kwa wabunge unatakiwa kuchukuliwa kwa umakini kwa kuwa suala hilo limepigiwa kelele kwa muda mrefu.

"Tanzania ni nchi masikini, vipaumbele vya kulikomboa taifa letu vipo vingi na bado havijatekelezwa. Ubunge ni utumishi na kama ni hivyo wabunge wanatakiwa kuishi kama wanavyoishi wananchi wengine," alisema Dk Bana.

Mhadhiri mwingine wa Chuo hicho, Bashiru Ally alisema suala hilo litatengeneza matabaka kati ya aliye nacho na asiye nacho.
"Tunapaswa tujenge taifa la kujitegemea kulingana na hali ya uchumi wetu na sio kuiga mambo ya watu, watawala kupenda kuwa katika nafasi za juu kwa misingi ya kupata fedha ni tatizo," alisema Bashiru.

Shibuda adai posho muhimu
Mbunge wa Maswa Mashariki (Chadema), John Shibuda alisema suala la wabunge kuongezewa posho halina ubaya wowote kwa kuwa litawafanya wasiwe ombaomba.

Shibuda ambaye katika mkutano wa Bunge la Bajeti alipingana na sera ya chama chake iliyokuwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 kuhusu posho za vikao, alisema ili mbunge atekeleze majukumu yake vizuri ni lazima alipwe fedha ya kutosha.
"Umefikia wakati Waafrika tulinde fedheha kwa viongozi wetu ili wasiwe ombaomba. Viongozi wakilipwa vizuri wataweza kuitumikia nchi na jamii inayowazunguka, ipasavyo. Kutokulipwa vizuri ndio mwanzo wa viongozi kusaini mikataba mibovu," alisema Shibuda.

Makamba ashtushwa
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, alieleza kushangazwa na ongezeko hilo la ghafla akisema kamwe wabunge wasifikiri kuwa wanaweza kumaliza matatizo yao au ya wapigakura wao kwa fedha ya posho.
Alisema kitendo cha wabunge kuongezewa posho za vikao kwa asilimia 185.7, kinaleta jazba kwa wananchi ambao wanahangaika kila kukicha kwa ugumu wa maisha.

"Kwenye jamii lazima kuwe na usawa, kama watu tupo kwenye hali mbaya (ugumu wa maisha) lazima wote tuenende sawa. Wabunge kuongezewa posho kwa asilimia 185 siyo sawa kabisa, tunajiweka mbali na wananchi na wanatuona tunafaidika sana wakati wao wanateseka kwa ugumu wa maisha," alisema Makamba.

Alisema kuwa, kutokana na msimamo wake huo, Juni mwaka huu alikataa posho iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini baada ya kuhudhuria semina iliyoandaliwa na wizara hiyo.

"Tulikaa kwenye semina kwa saa mbili, tunamaliza naletewa karatasi nisaini posho ya Sh280,000. Nilikataa. Nilikataa kwa sababu nilitambua kuwa ile ni kazi yangu kama mbunge, sasa unanilipa hela ya kazi gani?" alihoji Makamba.

Habari hii imeandaliwa na Fredy Azzah, Frederick Katulanda, Mwanza, Patricia Kimelemeta, Fidelis Butahe na Ellen Manyangu
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 
Kuna taarifa kwamba wabunge wamejiongezea malipo ya vikao vya bunge kutoka sh 70,000 kwa siku hadi 200,000 kwa siku.Nataka kujua hivi wabunge wa CHADEMA nao wamejua hali hii na kukubali kweli kuchukua viwango vipya ?

Nataka jibu moja ,(Kati ya NDIYO Na HAPANA) kutoka kwa wanaojua ,sitaki maelezo !

nitarejea baada ya majibu
 
Miswaada bungeni huwa inapitishwa na Magamba wakitumia wingi wao na hili wamelipitisha kwa mtindo huo sasa wewe ulifikiri Chadema wafanyeje????
Usitake tu Ndiyo & Habana taka ufafanuzi Ila Kama Umetumwa gangamala na swali lako lakini cha msingi ungewauliza wabunge Wa Magamba wao wangekujibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…