POSSO Yatangaza neema kwa wanariadha Tanzania

POSSO Yatangaza neema kwa wanariadha Tanzania

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
IMG_3463.jpeg

Kutoka kushoto ni Suleiman Nyambui, Luis Posso(Posso International Promotions) , Mao Hando , Zakarie Barie , Yuich Isaka (Asics) na Mwanariadha Gabriel Gerald Geay.


Kampuni ya Posso International Promotions yenye Makao Makuu yake nchini Marekani imetangaza neema kwa wanariadha wa Kitanzania kuanzia Shule za Sekondari, Vyuo na Wanariadha wanaojitegemea.

" Tunatarajia kuanzisha Eneo maalum la kisasa la kufanyia mazoezi kwa wanariadha (International Standards Training Camps) , Tutashirikiana na Kampuni ya Asics kwa ajili ya vifaa vya mchezo wa riadha , tunaleta makocha hapa Tanzania kutoka nchi mbalimbali ikiwemo majirani zetu ili wabadilishane uzoefu na tunatarajia kushirikiana na Shirikisho la Riadha Tanzania kuboresha uwanja wa Sheikh Amri Abeid sehemu ya kukimbilia (tartan Track) ili kupata muda sahihi kwa wanariadha wa uwanjani " alisema rais wa Posso International Promotions Luis Felipe Posso.

Posso na Asics inatarajia kuanzisha mbio za Nyika , mbio za kilomita 21 , mbio za kilomita 10 na michezo ya uwanjani kwa vijana wa Kitanzania kuanzia sekondari hadi wanariadha wakubwa wa kimataifa.

Ikumbukwe kuwa Posso ndo wasimamizi wa Wanariadha wakubwa Tanzania, akiwemo Gabriel Gerald Geay , Alphonce Felix Simbu na Jackline Sakilu.

"Tunashukuru kampuni ya Posso kwa kuendelea kuwasaidia wanariadha wetu kufikia malengo yao, pia tunashukuru kwa mabadiliko chanya wanaotegemea kuja kufanya kwa wanariadha wetu, sisi kama Shirikisho la Riadha Tanzania RT tutawapa ushirikiano wa kufanikisha malengo yao " alisema Mwenyekiti wa chama cha Riadha Mkoa wa Arusha, Gerald Babu.
 

Attachments

  • IMG_3465.jpeg
    IMG_3465.jpeg
    1.5 MB · Views: 2
Back
Top Bottom