Posta ni salama kutuma na kupokea mizigo kutoka nje ya nchi?

Ultimate

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2016
Posts
739
Reaction score
1,888
Hellow bosess

Kwa wazoefu naomba kujua kama Shirika la Posta ni salama kiasi gani kupokea bidhaa nilizonunua mtandaoni (Amazon, eBay na Ali Baba), pia kama kuna gharama za ziada.


==============================

 
lipo salama tu saivi lipo improved,nenda pale ufungue sanduku la posta uwe nalo mzigo unaenda kuchukulia pale pale bila shaka yoyote,malipo ni ya kawaida tu
 
Hellow bosess

Kwa wazoefu naomba kujua kama Shirika la Posta ni salama kiasi gani kupokea bidhaa nilizonunua mtandaoni (Amazon, eBay na Ali Baba), pia kama kuna gharama za ziada.
Mkuu umeshapata kazi TISS??
 
Naomba nikutoe wasiwasi kuwa, kwa siku za hivi Karibuni (tukiacha historia)
SHIRIKA LA POSA wamebadilika sana
Labda nianze kwa kusema kuwa, mimi nilikuwa Muhanga wa historia isiyokuwa nzuri ya shirika hili kwani nilikuwa nalitumia sana miaka kama 4 iliyopita japo niilishia kupokea kama 70% ya vitu nilivyo tumiwa/agiza hivyo kukata tamaa na kuacha kulitumia
Ni mwaka huu 2019 (mwanzoni), nilienda kuwa tembelea tawi moja la mjini kati (Meru Posta) na kukutana na mama wa makamo (45yrs hivi) alikuwa na uso wa bashasha na pale nilipo jaribu kumuuliza vipi kuhusu upoteaji wa Vifurushi aliniambia kwa sasa wapo vizuri. Kwanza nilivutiwa na huyo mama alivyokuwa mchangamfu nikaona kweli Posta wamebadilika kwani, sasa wanatoa huduma ya kibiashara na sio kama zamani

USHUHUDA
Nimeanza tena kutumia huduma za POSTA kwa miezi kadhaa sasa, NAKUHAKIKISHIA SIJAPOTEZA HATA PARCEL MOJA kutokea simu, hadi memory card; na kumbia parcel ikifika Posta wanatuma meseji na hata kupiga simu
BIG UP shirika la POSTA; HONGERENI SANA NA MWENDELEE HIVYO HIVYO, Mtapata Biashara na hata kuyafuta mashirika kadhaa yanayo jikongoja.

USHAURI:
Sijui kikokotoo cha ushuru huko posta (TRA) ila ningeshauri kama inafaa, hizo bidhaa zinazotozwa kodi, mtu akisha lipia gharama za posta; kinacho ongezeka kwa TRA kiwe VAT pekee na sio tozo kadhaa ......
 
Habari za leo wanajamvi?
Nimekuwa nikiagiza mizigo mara kwa mara kutoka China na Singapore sanasana na Tracking inakwenda vizuri sana ila mzigo ukishafika Destination Country yaani Tz unaweza kukaa wiki 2 mpaka 3 hamna updates zozote kuhusu mzigo.
Kwamfano Nina mzigo umeingia tangu tar 6 Dec 2019 mpaka leo hawajauprocess unifikie nilipo.
Tatizo ni nini?
Au nakosea wapi?
Ushauri tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shirika limejaa wajanja wajanja wapigaji na hakuna hatua zinachukuliwa. Shida ya kuajiri kwa kujuana. Unakuta wafanyakazi wana undugu na mabosi wakubwa.

Huu uhuni huwezi upata kamwe huko DHL.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GreatMkubwa,
Posta bado wanafanya kazi in Primitive way, wanafanya utafikiri tuko enzi zile za POSTA na SIMU. Kuna watu wako pale inafaa tu wapate mafao yao wasepe, zije ideas mpya from watu wapya. Wenzetu wanasema "YOU CAN'T TEACH OLD DOG, A NEW WAY OF HUNTING".
 
Kuna shirika gani la umma nchi hii linalotoa huduma nzuri? Mnachokiona Posta ndicho kinachotokea TTCL, TANESCO, Mamlaka za Maji na kiboko yao TRA. Ukiandika barua TRA leo ukafuatilia kesho unaambiwa "hatuioni, katuletee copy" na unaweza usijibiwe mwaka mzima.
 
Mzigo ukishafika tz tracking inahamia kwenye site ya posta Tanzania so track kwa website yao ya post Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo hata uki-track kwenye ukurasa wa posta hakuna majibu yanayopatikana, ni kama haifanyi kazi kabisa. Unabakia kushangaashangaa tu na hamu ya kupokea kipaseli chako[emoji3][emoji3][emoji3] mzigo kutoka posta kuu kuja kwa sisi tuliopo mikoani inachukua muda mrefu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naishi mtwara,

Vitu kutoka China to Dar=two weeks
Dar to Mtwara=two months
Kweli kabisa,niliagiza tv Amazon ilichukua siku sita tu kuletwa Tanzania na wala sikutumia DHL au njia za haraka ni posta tu. Lakini kutoka Dsm mpaka Mtwara wiki tatu na ushee na hapo nimeenda posta na kuwauliza sana ndipo wakajibu mzigo upo[emoji23][emoji23][emoji23] tabu sana hii rangi nyeusi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…