Ultimate
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 739
- 1,888
Hellow bosess
Kwa wazoefu naomba kujua kama Shirika la Posta ni salama kiasi gani kupokea bidhaa nilizonunua mtandaoni (Amazon, eBay na Ali Baba), pia kama kuna gharama za ziada.
==============================
Kwa wazoefu naomba kujua kama Shirika la Posta ni salama kiasi gani kupokea bidhaa nilizonunua mtandaoni (Amazon, eBay na Ali Baba), pia kama kuna gharama za ziada.
==============================
Naomba nikutoe wasiwasi kuwa, kwa siku za hivi Karibuni (tukiacha historia)
SHIRIKA LA POSA wamebadilika sana
Labda nianze kwa kusema kuwa, mimi nilikuwa Muhanga wa historia isiyokuwa nzuri ya shirika hili kwani nilikuwa nalitumia sana miaka kama 4 iliyopita japo niilishia kupokea kama 70% ya vitu nilivyo tumiwa/agiza hivyo kukata tamaa na kuacha kulitumia
Ni mwaka huu 2019 (mwanzoni), nilienda kuwa tembelea tawi moja la mjini kati (Meru Posta) na kukutana na mama wa makamo (45yrs hivi) alikuwa na uso wa bashasha na pale nilipo jaribu kumuuliza vipi kuhusu upoteaji wa Vifurushi aliniambia kwa sasa wapo vizuri. Kwanza nilivutiwa na huyo mama alivyokuwa mchangamfu nikaona kweli Posta wamebadilika kwani, sasa wanatoa huduma ya kibiashara na sio kama zamani
USHUHUDA
Nimeanza tena kutumia huduma za POSTA kwa miezi kadhaa sasa, NAKUHAKIKISHIA SIJAPOTEZA HATA PARCEL MOJA kutokea simu, hadi memory card; na kumbia parcel ikifika Posta wanatuma meseji na hata kupiga simu
BIG UP shirika la POSTA; HONGERENI SANA NA MWENDELEE HIVYO HIVYO, Mtapata Biashara na hata kuyafuta mashirika kadhaa yanayo jikongoja.
USHAURI:
Sijui kikokotoo cha ushuru huko posta (TRA) ila ningeshauri kama inafaa, hizo bidhaa zinazotozwa kodi, mtu akisha lipia gharama za posta; kinacho ongezeka kwa TRA kiwe VAT pekee na sio tozo kadhaa ......