macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Kimsingi taasisi, mashirika ya umma, wizara na idara zake kila kitu kinaendeshwa kijima. Bado wapo miaka ya 1970 na mbaya zaidi wana urasimu wa hali ya juu. Kuibadilisha Tanzania inahitaji operation kali sana. Watu hawajali na wanaenda kazini ili kuhesabiwa tu na siyo kufanya kazi.Posta ya Tz ni taasisi fulani hivi ya kijima, genge la vibaka na upuuzi mwingine mwingi.
Ni siasa tu, hamjui kwamba wanapenda mpate shida na mateso ila wao washibe na kunenepeana na mimafutamafutaRangi nyeusi siyo binadamu mkuu!
Mkuu acha kufananisha DHL na ushuzi wa mbuzi tafadhaliShirika limejaa wajanja wajanja wapigaji na hakuna hatua zinachukuliwa. Shida ya kuajiri kwa kujuana. Unakuta wafanyakazi wana undugu na mabosi wakubwa.
Huu uhuni huwezi upata kamwe huko DHL.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi naishi mtwara,
Vitu kutoka China to Dar=two weeks
Dar to Mtwara=two months
Kweli, nikiingia kule kwa Posta Tz naambiwa haupo kwny system[emoji26] inaboa sana, niliwaagizia watoto zawadi matata sana na nikawaahidi by Christmass watakuwa nazo saaasaaaa nimejieleza mpaka bas. Wanataka zawadi zao, inaboa sanaTatizo hata uki-track kwenye ukurasa wa posta hakuna majibu yanayopatikana, ni kama haifanyi kazi kabisa. Unabakia kushangaashangaa tu na hamu ya kupokea kipaseli chako[emoji3][emoji3][emoji3] mzigo kutoka posta kuu kuja kwa sisi tuliopo mikoani inachukua muda mrefu sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu, kama una link itakayonisaidia we nipe hata DM. Tracking number ndio Password yenyeweKama hutojali nitumie tracking number ila kwa sasa ni sikukuu so mambo mengi yamesimama
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu una bahati sana.... Mimi nilituma simu... Parcel ikafunguliwa simu ikaibiwa parcel ikafungwa tena.. Nawasiliana na posta Cape Town parcel imerudishwa lakini haina kitu ndani... Nikapewa documents nijaze kwa ajili ya investigation.... Mpaka leo mwaka wa Tano huu....Kweli kabisa,niliagiza tv Amazon ilichukua siku sita tu kuletwa Tanzania na wala sikutumia DHL au njia za haraka ni posta tu. Lakini kutoka Dsm mpaka Mtwara wiki tatu na ushee na hapo nimeenda posta na kuwauliza sana ndipo wakajibu mzigo upo[emoji23][emoji23][emoji23] tabu sana hii rangi nyeusi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni password vipi ibandikwe juu ya mzigo.Nijuavyo tracking no hutolewa kwaajili ya kukujulisha mzigo ulipofikia.Anyway kila la kherHapana mkuu, kama una link itakayonisaidia we nipe hata DM. Tracking number ndio Password yenyewe
Sent using Jamii Forums mobile app
Bro msaada wa kupeana mpaka Tracking number haupo... kuandikwa juu haimaanishi ndio nikupe namba.Kama ni password vipi ibandikwe juu ya mzigo.Nijuavyo tracking no hutolewa kwaajili ya kukujulisha mzigo ulipofikia.Anyway kila la kher
Sent using Jamii Forums mobile app
Ee yamekuwa hayo...naona fikra zimepishana na uelewa pia.Bro msaada wa kupeana mpaka Tracking number haupo... kuandikwa juu haimaanishi ndio nikupe namba.
Kuchukua mzigo unahtaji Tracking namba na ID yako.
Kwanza we nikupe hyo namba we nani??? Meneja wa Posta????
Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa jamaa wa posta ni wezi sana. Mwezi uliopita nilipokea vimzigo v2 kiearphone na card reader. Upumbavu unaanzia wapi?
wananitumia meseji ndugu mteja fika ofisi ya posta dirisha namba c pia kumbuka kuja na 18800. Nikajiuliza kama vimzigo hivi havifiki hata kilo1 nalipishwa hivyo inakuwaje nikiagiza mikubwa kidogo?