Posta Tanzania kushirikiana na Posta za Afrika

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Arusha
🗓️ 12 Juni, 2024

Shirika la Posta Tanzania limejidhatiti kushirikiana na Posta nyingine Barani Afrika hususani katika huduma za Biashara Mtandao “E-Commerce” pamoja na huduma za Usafirishaji.

Hayo yamebainishwa na Postamasta Mkuu Maharage Chande wakati akizungumza na Postamasta wakuu wa nchi za Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo pamoja na Mdau wa Sekta ya Posta ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ship2MyID ya Marekani.

Aidha, Bw. Maharage ameelezea maendeleo ya kiteknolojia yaliyofanywa na Shirika la Posta Tanzania likiwemo Duka Mtandao linalowezesha wananchi Duniani kote kuuza, kutangaza na kununua bidhaa pia kufikishiwa popote pale walipo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…