Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Shirika la Posta Tanzania leo limepokea ugeni wa wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Gilman Rutihinda iliyopo Wilaya ya Kinondoni, Kata ya Kigogo, walipotembelea banda la Posta katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (SABASABA).
Wanafunzi hao 89 waliongozwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Mwl. Juliana Shine, ambapo walipata fursa ya kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika la Posta Tanzania.
Katika ziara hiyo, wanafunzi walielezwa kuhusu huduma za kisasa za usafirishaji wa mizigo na barua, matumizi ya masanduku ya barua, huduma ya SwiftPack, pamoja na huduma ya kidijitali ya duka la mtandaoni la Posta (KIPEPEO SHOP).
Aidha, walipata elimu kuhusu mashindano ya kimataifa ya uandishi wa barua kwa wanafunzi wa shule za msingi yanayoandaliwa kila mwaka, ambapo wanafunzi walihimizwa kushiriki kwa wingi ili kukuza vipaji vyao na kujiamini katika mawasiliano ya maandishi na ujenzi wa hoja zenye mantiki.
Posta Tanzania inaamini kuwa kuwafikia watoto na vijana kupitia elimu ni njia bora ya kujenga kizazi kinachotambua thamani ya huduma za Posta na matumizi yake katika maisha ya kila siku.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania