Postcode na Utata wake

Postcode na Utata wake

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Wanasema shamba la bibi hauhitaji ruhusa kuvuna.

Leo nimepokea ujumbe wa SMS kuhusu postcode, ikinitaka kubonyeza *152*00# ili kuona posti kodi yangu. Ajabu ni kuwa postcode hii ni sawa na iliyotumika katika NIDA, najiuliza kwa serikali itumie pesa kufanya jambo ambalo tayari lipo katika mfumo.

Ukiangalia NIDA yako, baada ya tarehe ya kuzaliwa zinafuata namba 5 ambazo ndizi PostCode zako na zinaeleza vizuri unapatikana wapi. Suala ingekuja na namna ya street address ambayo kwa nchi yetu bado sana.

Baadhi ya Viongozi hukimbilia kutoa mifano ya nchi nyingine lakini hawaangalii usawa wa nchi masikini kama TZ na hizo nchi wanazosema. Inasikitisha sana.
 
Bado tuna changamoto sana kwenye swala la mipango miji lingekuwa linafanyika kwenye miji mipya ungepatikana utaratibu wa kutoa Postcode vizuri ila huku uswahili kipengele.
 
Hizo postikodi zilizopo TCRA, zipo muda sana... ila hazipo ktk details kama kitakacho kuja kufanyika sasa...

Tuwe watulivu ndgu zangu
 
Wanasema shamba la bibi hauhitaji ruhusa kuvuna.

Leo nimepokea ujumbe wa SMS kuhusu postcode, ikinitaka kubonyeza *152*00# ili kuona posti kodi yangu. Ajabu ni kuwa postcode hii ni sawa na iliyotumika katika NIDA, najiuliza kwa serikali itumie pesa kufanya jambo ambalo tayari lipo katika mfumo.

Ukiangalia NIDA yako, baada ya tarehe ya kuzaliwa zinafuata namba 5 ambazo ndizi PostCode zako na zinaeleza vizuri unapatikana wapi. Suala ingekuja na namna ya street address ambayo kwa nchi yetu bado sana.

Baadhi ya Viongozi hukimbilia kutoa mifano ya nchi nyingine lakini hawaangalii usawa wa nchi masikini kama TZ na hizo nchi wanazosema. Inasikitisha sana.
Hizo ni namba za utambulisho wa Kata,je mitaa mingapi ilikuwa na majina official na namba za nyumba?
 
Hizo posticode za nida ni za kata elewa. Hizi wanazogawa sahivi nizamakazi.
 
Naona wanataka kuvuruga zoezi.ilipaswa zoezi la post code liishe kwanza ndio tuanze kuupdate hizo taarifa vyenginevyo tutaharibu tu.
 
hili zoezi limeharibika kabisaaa kwa sababu limevamiwa kama nzige na matapeli...watu wameona ni fursa nyingine ya kupiga hela.
 
Huku ninakoishi nimepewa jina la mtaa! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Back
Top Bottom