smarte_r
JF-Expert Member
- Nov 8, 2013
- 4,564
- 12,014
Nitajitahidi kutafsiri kwa kiswahili ili iwe msaada kwa ndugu zangu watanzania ambao lugha ya kingereza sio rafiki kwao.
Miguna anasema,
Jomo Kenyatta (johnston kamau ngengi) alikuwa ni mtu mbaya kimuonekano ambaye jina na sura yake vinatakiwa kuondolewa kwenye masanamu, viwanja vya ndege, barabara, majengo na fedha ya kenya kwa kutumia sulphuric acid.
Anasema hakuwa tu mbaya kimaumbile bali hata kimaadili ambapo aliuwa watu wakubwa wa kenya wa enzi hizo waliokuwa na maono mazuri kwa taifa hilo.lakini pia aliipora kenya kwa kutumia mabavu.
Anasema jomo kenyatta alirejea kenya akitokea ulaya alikokuwa anafanya kazi za bustani kwa miaka 15 nchini scotland.
Anasema alipopata tu nafasi ya kuwa waziri mkuu wa kenya mwaka 1963,hakuwa akimiliki gari, nyumba wala ardhi. lakini miaka 15 baadaye baada ya kuwa waziri mkuu, alipora ardhi yenye ukubwa sawa na eneo lote la pwani ya kenya. uporaji ulimfanya kuwa mtu mwenye utajiri mkubwa africa.
Anasema laiti kama jomo kenyatta asingewauwa watu wenye maono makubwa wa nyakati hizo kama pio pinto gama, argwings kodhek, thomas Joseph mboya na JM kariuki, taifa la kenya lingekuwa katika nafasi kubwa ya kuwa taifa la kwanza kimaendeleo toka africa ktk karne ya 20.
Anasema Jomo Kenyatta alianzisha mauaji, ukabila na uporaji katika siasa za kenya.
Anahitimisha kwa kuweka hashtag
# DespotsMustFall akiwa na maana viongozi wanaotawala kimabavu lazima wadondoke.