Mkuu tuache unafki..
Diamond kashuka sana kimuziki,kwa sasa anatamba na skendo za insta za kula mademu wakali..
Hivi Diamond anatoa wimbo na Rick Ross alafu unabuma.??huyu sio Diaomond tuliyemzoea..
Tatizo linalomuangusha ni huyu Sallam kazidi sana uswahili hadi anakera,.
Kuna siku aliwahi kuropoka eti "Alipofikia Diamond kwa sasa hawezi tena kufanya shoo za ndani ya nchi"..
Umeona ushamba huo sasa.! Akina Wizkid hawafanyi shoo Nigeria kwani.??????
Dogo anajipalilia kaburi lake mwenyewe..
Infact kwa sasa mimi sitamuunga mkono msanii yeyote atakayepamba na Clouds media kwasbabu wakina Sugu walijitahidi sana na Jaydee alafu hawa wakina Diamond walikuwa upande wa Clouds leo hii wanajifanya ndiyo wanaelewa kwamba Sugu na Jide waliona mbali..