Povu langu nisiye na nyumba

Povu langu nisiye na nyumba

Ila wewe dogo nimnafiki sana... Ila bby wangu evelyn nimemuomba asiku'block
Hata akiniblock hainipunguzii kitu ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
Unafki wangu upo wapi hapo acha kunisingizia mkuu
 
Hata akiniblock hainipunguzii kitu ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
Unafki wangu upo wapi hapo acha kunisingizia mkuu
Mdogo wangu kesi na shem wako tumeshamaliza PM nimelia sana๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ hadi nikabubujikwa na machozi kukuombea msamaha.๐Ÿ’ช
 
Mdogo kesi tumeshamaliza PM nimelia sana๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ hadi nikabubujikwa na ma hozi kukuombea msamaha.๐Ÿ’ช
Unaniombea msamaha wa kosa gani nililofanya!!!

Nilitegemea upo pm yake kumtongoza mkuu sio kuniombea msamaha mimi
 
Kwahiyo niishi kama digidigi for 10 long years sacrificing my quality of life in the hope ya kujenga nyumba ya KAWAIDA, ambayo sitakuwa naifurahia for the rest of my life there, hivyo niendelee kuishi kama digidigi kwa miaka yangu ijayo?

Kwanini hiyo miaka kumi ambayo nina nguvu na akili inachaji nisiitumie kufocus kwenye kutengeneza mpunga mrefu huku nikipumzika mahala pazuri kufacilitate process hiyo, na kisha nitakapokuwa na uwezo nijenge nyumba ninayoweza kuifurahia?
Mimi nilipopata kazi, cha kwanza nilipanga na baadae kununua gari. Watu ee unanunua gari hata kiwanja huna. Nikawaambia ni maamuzi yangu kwani kiwanja hakitanipeleka kazini. Nikawaambia ,kama nimeweza kupanga na kununua gari kiwanja nitanunua na kujenga pia maana Mungu si Athumani.
Nimejenga tena si kwa kujibana kuishi maisha ya dhiki na kushinda njaa, mdogo mdogo.
Sipendi mambo ya kuulizwa sijui umejenga, una mtoto, umeolewa maana mimi huwa sipendi kuuliza mambo hayo.
Utamaduni mbaya sana wa kutaka kujua mambo ya watu ili kwenda kusambaza umbea.
 
Kaka ukiona tu mwanaume kafikia haya we Kua tu mpole ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 

Attachments

  • 20241216_155230.jpg
    20241216_155230.jpg
    835.7 KB · Views: 1
@evelyn salt hebu ukuje useme simu yako tofali ngapi?

Ila haya maisha jamani khaaah!!
Kuna ndugu yangu mdada alilnunuliwa silmu 2 ,iPhone na sumsung S24, jumla M7, wakwe zake wanamsema unatembea na kiwanja mkononi. Ila maskini mume kafa amebaki kulia tu mwaka unaisha sasa.
 
Aisee, kudaiwa kodi raha sana...kama vile kudaiwa bia!
Siku ya kulipa Landlord anavyochekelea pale unapomuhesabia....Acha tutembee na nyumba zetu mfukoni; leo Mbagala kesho Kigamboni...ukichoka jiji unalaza pande za Picha ya Ndege!
 
Hata siwasalimii...... hivi nyie mliofanikiwa kujenga mkoje lakini? Mbona mnajifanya kama vile mlitoka tumboni kwa mama zenu na cement mkononi, mmefika tu duniani na kuanza ujenzi, sio kudolishia huko na hapo utakuta kinyumba chenyewe cha kawaidaaa tu mxyuuu (japo mie hata nyumba isio na mlango tu sina ๐Ÿ˜‚ )

Nnaowaongelea hapa hata sio wapokea kodi wetu, ila ni wapenzi watazamaji tu ambao wapo interested na kujua wapi tunalaza vitambi vyetu, kuna vitu kabla haujaongea hebu jiulize mara mbili unaemwambia kitamgusa vipi, imagine unakutana na Mimi sasa nakuuliza mwanao anasoma shule gani unanijibu chaurembo secondary halafu nianze kukushangaa haaa unamsomeshaje huko mie siwezi asee wangu yupo st nanii huko hivo utajisikiaje?

Au mtu anakuuliza unafanya kazi gani, unawezaje kufanya hiyo kazi mie siwezi mxyuuuuuuuuuu

Hivi ushawahi kukutana na kejeli za wenye nyumba? Usiombe awe kakupa na lift jamani utatamani upenye dirishani sijui gari lina dirisha sijui mlango eeh hapo hapo. Swali linaanza kama pepa la hesabu, unapokaa umejenga, ukijibu tu nimepanga. Cha kwanza atakutolea mijicho, ndio aanze kushangaa sasa heeeee yani umepanga mi siwezi nna nyumba mbili siwezi kabisa kupanga yani kodi hapana dah siwezi pyeeeee kajambe kule bana hata Kobe na konokono wana nyumba zao tena wao wanatembea nazo kabisa na hawana hata makuu, ndio sijajenga sasa ka vipi nijengee. Mafao yenyewe tu nikistaafu nitayanywaaaa yani ntafunga bar!

Povu povu tu.๐Ÿ˜
Ile nyumba yako umeuza?
 
Masimango hayaishi, utaulizwa Tena mbona umejenga mbali hivi? Huku hata kiwanja Bure sitaki. Mbona umejenga mtindo wa kishamba? Kwa nini hukuomba ushauri?....basi tu kuhakikisha hupati amani.
 
Back
Top Bottom