Aisee huyu jamaa alivuma sana miaka ya 80 but sadly I never got to see him. Kulikuwepo na story kibao kuhusu uwezo wake wa nguvu za misuri, mambo kibao yaliongelewa, mfano:
-- Alikuwa anaweza kunywa kreti nzima ya soda kwa mkupuo
-- Alikuwa anaweza kutegesha kifua na tairi la nyuma la trekta kupita bila kuumia
-- Alikuwa anaweza kuvuta lorry lenye shehena kubwa kwa kutumia nywele
-- n.k.
Were these just a bunch of childish myths kutufanya tukimbie mchakamchaka na kuwahi namba shuleni or was there a grain of truth in them? Tafadhali sana naomba wale waliobahatika kuyaona maonesho ya jamaa watupatie ushuhuda hapa.
Pia naomba kuuliza, je yuko wapi siku hizi, kuna mwenye picha? Bado yupo, au..??
Akhsanteni!!
Hapana X-P hakua mtu wa msoma alikua msukuma, naskia alikuja kuokoka yeye na mwingine alikua anaitwa power Mwasekaga kitu kama hicho.Ni kweli huyo jamaa, alikuwa na nguvu kweli kweli, nasikia alikuwa ni mtu wa Musoma, Mara uko...! Hayo ni mambo ambayo kweli alikuwa anafanya, na alikuwa ana uwezo wa kunywa chupa za orange squash mpaka mbili bila ya kuzimua.
Si hivyo tu, alikuwa anauwezo wa kuzuia piki piki kwa kutumia nywele na wakati mwingine meno. Na hata kuzuiya gari kwa kutumia nywele zake. Na alikuwa akivunjiwa jiwe kubwa kifuani kwake.
Pia kulikuwa na mwingine anaitwa power Bernard, na wakaja mwishoni mwishoni kina power Bukuku, ila wengine nimewasahau.
Gonga hapa mkuu, kuna uzi kama huyo.
Power-mabula-moris-nyunyusa-na-mwinamila-tz-imewaenzi-vipi.html
Umenikumbusha enzi za mapawa na maprofesa (wanamazingaombwe). Power Mabula was one of my favourite, kulikuwa na power mwingine anaitwa Power Ngeta, huyu akija tulikuwa tunaimba "Power! Ngeta! Super! Kibongeeee!" Sijui yuko wapi naye huyu.
Kuna dogo tulikuwa tuko naye darasani alikuwa ni fundi wa kutengeneza mihuri (inayogongwa mkononi kama unatoka nje mara moja na utarudi), basi wale maprofesa wakija dogo naye anatengeza na kutugongea mikononi watu wanaotaka kuingia bila kulipia. Baadae ukitoka unampa shilingi 5 au unamnunulia vipande vya mihogo. Tulikuwa tunainjoi sana maisha yale.
The guy is alive yet; kwa sasa ana-hubiri INJILI na wakati mwingine uwa anatangaza vipindi fulanifulani KISS FM Mwanza.
Kweli huyu jamaa alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya maajabu, alikuwa ana uwezo wa kubeba kwa meno mifuko mitano yenye simenti na pia kuzuia pikipiki zisiondoke kwa kutumia kope za macho. Anayetakaya kimuona wasiliana na Kiss FM Mwanza atapata habari zake
Kulikuwa na PAWA SAVIMBI, JAFAR VURU MROMA , MBWA MWITU (RIP).......Siku hizi huu mchezo haupo tena......kila mtu sharobaro
Ahsante Mamushka kwa kusahihisha, mambo yenyewe ya siku nyingi tena, nshaanza na kusahau.Hapana X-P hakua mtu wa msoma alikua msukuma, naskia alikuja kuokoka yeye na mwingine alikua anaitwa power Mwasekaga kitu kama hicho.
Hawa jamaa walitakiwa wawekwe kwenye kipindi cha Believe it or No cha AXN.
Hao wote nilio wataja hapo juu, wameshafariki zamani, akiwemo Mzee Mwinamila. Kumbuka kuwa Mzee Moris alikuwa ni kipofu, na alikuwa ana uwezo wa kupiga ngoma mpaka kumi na sita.
Naombeni mnikumbushe mzee mwinamila alikua ni nani tana hilo jina na likumbuka.
mmenikumbusha power Mketa super Kibonge wa kule kwetu Mtwara.. Duh huyu jamaa alishatujaza uwanjwa wa Umoja pale karibu primaries zote za pale mtwara kipindi hicho kiingilio sumni