Marehemu Mzee Mwinamila (Mzee Saleh Ramadhan Mwinamila), alikuwa ni kiongozi wa kikundi cha ngoma, kilichojulikana kwa jina la 'Hiari ya Moyo'. Iki kikundi kilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1950, nazani mwaka 1957 kama nakumbuka historia vizuri. Na ni ngoma za kabila la watu wa Tabora (Wanyamwezi). Iki kikundi kilikuwa kama kikundi cha kitaifa, serikali ndio walikuwa wakiwapa pesa na kikitumbuiza kwenye dhifa mbali mbali za kitaifa.Naombeni mnikukmbushe, hivi mzee mwinamila alikua nani vilee, hilo jina nalikumbuka.
Duh! umenikumbusha mbali kweli enzi za shule ya msingi.
Pia kulikuwa na profesa mmoja wa kihindi anakupa ndizi waila halafu anapasua tumbo live na kutoa ndizi iliyoliwa sijui walikuwa wanatudanganyaje? mazingaombwe ya zawadi za biskuts, chupi na vitu kibao watoto mnapewa duh kazi kweli
Umenikumbusha enzi za mapawa na maprofesa (wanamazingaombwe). Power Mabula was one of my favourite, kulikuwa na power mwingine anaitwa Power Ngeta, huyu akija tulikuwa tunaimba "Power! Ngeta! Super! Kibongeeee!" Sijui yuko wapi naye huyu.
Kuna dogo tulikuwa tuko naye darasani alikuwa ni fundi wa kutengeneza mihuri (inayogongwa mkononi kama unatoka nje mara moja na utarudi), basi wale maprofesa wakija dogo naye anatengeza na kutugongea mikononi watu wanaotaka kuingia bila kulipia. Baadae ukitoka unampa shilingi 5 au unamnunulia vipande vya mihogo. Tulikuwa tunainjoi sana maisha yale.