Power tiller special thread

Jembe la power tiller ya mikono mifupi ni zito sana pawatila za mikono mirefu haziwezi kulivuta. Mashine huwa zinaelemewa sana na unaweza kusababisha matatizo mengine.

Kinachofanyika watu huwa wanachukua disc za majembe mazito na kuzifunga kwenye majembe ya power tiller za mikono morefu. Hii huongeza ufanisi na kufanya kazi kwa uhakika kwani disc nzito huhimili visiki na maeneo magumu. Disc za mashine za mikono mirefu ni nyepesi ikikutana na kisiki au jiwe huwa zinapinda au kuchanika, vile vile huwa zinaisha faster.

Kuhusu planter za kuendeshwa na power tiller hizo sijaziona.
 
Kama ni mahindi na watu wakawa wanapokezana ni wastani wa heka 8-10. Kwenye mpunga kukatua ni heka 5 - 7.5 hiyo rate ni kwa powertiler za mikono mirefu.

Kwa powertiler za mikono mifupi; kulima mahindi ni heka 2-4. Mpunga kukatua ni heka 2.5 -3.
Powertiller inaweza kupiga heka ngapi kwa siku bila kusumbua?
 
Nashukru, swali lingine nilikuwa nimeuliza hivi jembe la power tiller ya mikono mirefu ambalo linadisc nyingi ambalo power tiller ya mikono mirefu inaweza ikalivuta pasipo kuteteleka la mwisho kabisa linakuwa na disc ngapi? .
 
Vipi kuna sehemu watu wanakodisha hizo power tiler ama mtu anaweza kupata used?
Used labda mitaani Kubota full umapata kwa 7-8 million. Kukodisha hapana, hazikodishwi labda kama utampata mtu mkaingia mkataba nae.
 
Nashukru, swali lingine nilikuwa nimeuliza hivi jembe la power tiller ya mikono mirefu ambalo linadisc nyingi ambalo power tiller ya mikono mirefu inaweza ikalivuta pasipo kuteteleka la mwisho kabisa linakuwa na disc ngapi? .
Power tiller inavuta jembe la disc mbili tu! Kuna vidisc mfumo wa harrow vipo vinne lakini havifai kwa matumizi yetu waafrica.

Ukichongea mwamba na kuongeza disc ziwe tatu nayo nzuri lakini utaongeza risk ya operator kuumia kwa kukatwa na kisu au kujigonga kwenye kisu. Idadi ya disc imezingatia usalama wa mwendeshaji wakati wa kazi.
 
je kwa upande wa trailer ni vipi?kwani kuna baadhi ya power tiller unakuta watumiaji wameondoa trailer original na kuweka za kuchongwa kienyeji wakati mwingine unakuta trailer hizo ni kubwa zaidi kupita zile ambazo power tiller inatoka nazo kiwandani na kuzifanya power tiller zibebe mzigo mwingi na mzito zaidi,hiyo haiwezi ikaiathiri Power tiller?.

Kwa Power tiller za mikono mirefu ambayo ni nyepesi, kwa upande wa trailer la kutengeneza kienyeji trailer lake linatakiwa liwe na upana wa ft ngapi ili power tiller isiweze kuathirika?.
 
Power tiller ambayo inaweza kuhimili kubeba mzigo wa trailer za kuchonga ni zile za mikono mifupi (16-20 HP). Ingawa watu wanafunga kwenye Power tiller za mikono mirefu.

Faida za matela hayo ni kuwa utabeba mzigo mkubwa lakini hasara ni kuua mashine ndani ya muda mfupi. Tela za kuchonga kwenye power tiller za mikono mirefu hufanya machine kutoa moshi mzito muda wote, hii ni ishara ya kuelemewa. Hivyo kwa usalama wa chombo chako sikushauri uchongee tera kubwa kwani tela tu huwa na uzito mkubwa.

Kawaida power tiller za mikono mirefu (14 HP ) mzigo uwe 1-1.5 tone. Lakini watu hubebesha mpaka tani 2. Kwa zile za mikono mifupi unaweza kupakia hata tani 2 na mashine isiathirike labda tela liteteleke.

Tela la kawaida lina futi 3 upana na futi 6.5-7 uredu na futi 1-2 kimo. Inashauriwa kununua tela original na kulifanyia maboresho.
 
Mkuu mimi nina powertiller ya mikono mifupa naomba ushauri, je naweza kubadilisha tairi ndogo na kuweka za siam kubota upande wa injini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lengo likiwa ni nini? Jibu ni ndio unaweza kubadili tairi lakini utatakiwa kuchongea matundu mengine maana matundu ya stadi za kubota hayaingiliani.

Kama lengo ni kuongeza speed basi weka puli ya mashine za kusaga za diesel na pawatila itakimbia kama kubota bila kubadili tairi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je power tiller inaponunuliwa inakuja na water pump au water pump inanunuliwa kivyake?.
 
Puli nmeshabadilisha nataka kuongeza spidi na kusave mafuta, kingine injini ya powertila mikono mifupi ni nzito na inamaliza tairi mapema so nikiweka zile za kubota nahisi hazitaisha mapema.
Pia ushauri kwa wenye powertiller za mikono mifupi wanunue tairi za india za mchina hazina ubora zinaisha mapema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba pia kujua kuhusu Mintractors kama itawezekana
 
Mkuu kuna rejeter za aluminium huwa zinanisumbua sana chini zina rubber,huwa inaisha mapema na kuruhusu maji kuvuja naomba ushauri ufundi wa kureplace hiyo ruber.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni tiller gani inafaa kwenye kupalilia Mkonge?
 
Power tiller zinafaa eneo la lindi? Kuna eneo limekatwa miti hivyo kuna visiki ila vipo mbalimbali? Je ninaweza kuingiza power tiller nikawa ninakwepa visiki? Kuna majani sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…