Wale wanaohitaji kuzielewa power tiller karibuni.
Uzi huu utatumika kujibu maswali na majibu ya wadau ambao wamekua wakiniuliza mara kwa mara.
Kuna aina kuu mbili za power tiller yaani Long hand power tiller na Short hand power tiller.
LONG HAND POWER TILLER
Long hand power tiller ni zile zenye mikono mirefu ya kuendeshea kama ville Siam Kubota, Boar, Toyo, Myanmar(hazipo nchini), Swami, N.k
Power tiller hizi zote huwa ni 14 HP, 4 gear na magurudumu ya mbele makubwa kiasi. Powetiller hutoka ikiwa na cage wheel, disc plough na leki kwaajiri ya kupigia level na kuokota.
Bei zake nchini ni million 5 au pungufu kwa aina nyingine zote( India and chinese) bila tera na 7.5 million ikiwa complete. Hazidumu sana kwani huanza kusumbua gear box na engine ndani ya mwaka mmoja au miwili toka kununuliwa. Zinadumu kwa miaka 7 - 10 zikitunzwa vizuri.
Zinafaa kwenye kilimo cha mahindi na kilimo kingine kinachofanana na hicho.
Bei ni 9.5- 10 Million kwa Siam Kubota (Japan) bila tera na 12-14 million complete. Hudumu kwa muda mrefu up to 15 years na inaweza kufanya kazi miaka 3 bila serious service ya engine wala gear box. Shida ya hizi mashine ni ghalama kubwa zaa spea.
Hizi hukimbia sana na hufanya kazi kwa uharaka zaidi. Vile vile ni nyepesi kuopoa kama zikikwama kwenye tope wakati wa kuvuruga. Zinafaa kwa matumizi yoyote ya kilimo na katika mazingira yoyoye isipokuwa Yale yenye visiki kwani jembe lake si imara sana.
Picha hizi hapa.
View attachment 1275195View attachment 1275196View attachment 1275197View attachment 1275201View attachment 1275202
SHORT HAND POWER TILLER
Short hand power tiller ni zile zenye mikono mifupi ya kuendeshea kama vile Amec, Kubota(ndogo), Toyo, Greeves, Jiang Dong (JD), Zhong Hou (ZH) n.k.
Power tiller hizi huwa na 13 HP mpaka 20 HP kutegemeana na uhitaji wa mteja. Bei zake huanzia million 3.5 bila tera mpaka million 7 ikiwa full.
Power tiller hizi hutoka ikiwa na disc plough,Rotavator na cage wheel za kwenye maji.
Machine hizi huwa na gia 8 na hazikimbii sana lakini zinanguvu kubwa. Zinafaa kwenye kilimo cha aina yoyote. Tatizo kubwa la hizi machine ni kufa haraka yaani hazikai zaidi ya miaka 7 kama zinafanya kazi kweli kweli.
picha hapa chini
View attachment 1275204View attachment 1275205
MASOKO
power tiller hizi zinapatikana nchini sehemu Mbali mbali kama vile
Iringa - Auto sokoni ( aina zote), Kishen Inter prices( Toyo tu) na maduka mengine ya spear na power tiller
Dar es salaam - kishen pia wapo, na ofisi nyingine sizijui( watanisaidia wenyeji).
Agricom wanaopatikana morogoro na Mbeya na mikoa mingine.
Kwa Mbeya zinapatikana sehemu kubwa zenye kilimo cha mpunga.
Mikoa mingine zipo kwenye maduka mbali mbali ambayo yanapatikana huko.
Kama unauza utanitajia jina na mkoa ili nipandishe hapa.
Karibuni kwa maswali, maoni na nyongeza.