Power tiller special thread

Power tiller special thread

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,292
Reaction score
7,867
Wale wanaohitaji kuzielewa power tiller karibuni.

Uzi huu utatumika kujibu maswali na majibu ya wadau ambao wamekua wakiniuliza mara kwa mara.

Kuna aina kuu mbili za power tiller yaani Long hand power tiller na Short hand power tiller.

LONG HAND POWER TILLER

Long hand power tiller ni zile zenye mikono mirefu ya kuendeshea kama ville Siam Kubota, Boar, Toyo, yanmar, Swami, N.k

Power tiller hizi zote huwa ni 14 HP, 4 gear na magurudumu ya mbele makubwa kiasi. Powetiller hutoka ikiwa na cage wheel, disc plough na leki kwaajiri ya kupigia level na kuokota.

Bei zake nchini ni million 5 au pungufu kwa aina nyingine zote( India and chinese) bila tera na 7.5 million ikiwa complete. Hazidumu sana kwani huanza kusumbua gear box na engine ndani ya mwaka mmoja au miwili toka kununuliwa. Zinadumu kwa miaka 7 - 10 zikitunzwa vizuri.

Zinafaa kwenye kilimo cha mahindi na kilimo kingine kinachofanana na hicho.

Bei ni 9.5- 10 Million kwa Siam Kubota (Japan) bila tera na 12-14 million complete. Hudumu kwa muda mrefu up to 15 years na inaweza kufanya kazi miaka 3 bila serious service ya engine wala gear box. Shida ya hizi mashine ni ghalama kubwa zaa spea.

Hizi hukimbia sana na hufanya kazi kwa uharaka zaidi. Vile vile ni nyepesi kuopoa kama zikikwama kwenye tope wakati wa kuvuruga. Zinafaa kwa matumizi yoyote ya kilimo na katika mazingira yoyoye isipokuwa Yale yenye visiki kwani jembe lake si imara sana.

Picha hizi hapa.

images%20(4).jpeg
images%20(2).jpeg
images%20(5).jpeg
images%20(8).jpeg
images%20(6).jpeg

SHORT HAND POWER TILLER

Short hand power tiller ni zile zenye mikono mifupi ya kuendeshea kama vile Amec, Kubota(ndogo), Toyo, Greeves, Jiang Dong (JD), Zhong Hou (ZH) n.k.

Power tiller hizi huwa na 13 HP mpaka 20 HP kutegemeana na uhitaji wa mteja. Bei zake huanzia million 3.5 bila tera mpaka million 7 ikiwa full.

Power tiller hizi hutoka ikiwa na disc plough,Rotavator na cage wheel za kwenye maji.

Machine hizi huwa na gia 8 na hazikimbii sana lakini zinanguvu kubwa. Zinafaa kwenye kilimo cha aina yoyote. Tatizo kubwa la hizi machine ni kufa haraka yaani hazikai zaidi ya miaka 7 kama zinafanya kazi kweli kweli.

picha hapa chini

images%20(1).jpeg
images%20(3).jpeg

MASOKO

power tiller hizi zinapatikana nchini sehemu Mbali mbali kama vile

Iringa - Auto sokoni ( aina zote), Kishen Inter prices( Toyo tu) na maduka mengine ya spear na power tiller

Dar es salaam - kishen pia wapo, na ofisi nyingine sizijui( watanisaidia wenyeji).

Agricom wanaopatikana morogoro na Mbeya na mikoa mingine.

Kwa Mbeya zinapatikana sehemu kubwa zenye kilimo cha mpunga.

Mikoa mingine zipo kwenye maduka mbali mbali ambayo yanapatikana huko.

Kama unauza utanitajia jina na mkoa ili nipandishe hapa.

Karibuni kwa maswali, maoni na nyongeza.

images%20(2).jpeg

images%20(7).jpeg
 
Je spea za kubota zinaingiliana na powertiller za mchina
 
Kwa hiyo kuna uwezekano wa kuibadilisha kabisa powertiller ya kichina ikawa original kwa kuweka spea za Kubota kwenye engine na gear box?
Ndio, zinaingiliana kwa kiwango kikubwa, hata dukani spea zilizopo ni za kubota ingawa zipo za kichina na kijapani.
 
Kwa kilimo cha mpunga na mahindi power killer ipi inafaa na yenye hp ngapi?
 
Kwa kilimo cha mpunga na mahindi power killer ipi inafaa na yenye hp ngapi?
Kama una pesa ya kutosha powertiller nzuri ni Siam kubota ina 14 HP. Kama una mtaji mdogo nunua za kichina ambazo nazo ni long hand na zina 14 HP.

Hizi za mikono mifupi ni zina majembe mazito pia ni nzito mno hata utumiaji lazima kuwa watu zaidi ya mmoja wakati wa ufungaji wa majembe.

Wakati hizi za mikono mirefu ni nyepesi hata majembe yake ni mepesi, mtu mmoja tu anaoperate. Vile vile hizi za mikono mirefu hufanya kazi kwa uharaka zaidi.
 
Ni ngumu sana, kwasababu mashine za kichina zikichoka huanza na kufumuka/ kupasua jumba la gear box,kusumbua engine, kukata chassis, clutch kuungua, steering cable kukatika Mara kwa Mara, ukisema ubadili kila kitu utajikuta kwenye bei ya original.
Kwa hiyo kuna uwezekano wa kuibadilisha kabisa powertiller ya kichina ikawa original kwa kuweka spea za Kubota kwenye engine na gear box?
 
Sawa kabisa
Ni ngumu sana, kwasababu mashine za kichina zikichoka huanza na kufumuka/ kupasua jumba la gear box,kusumbua engine, kukata chassis, clutch kuungua, steering cable kukatika Mara kwa Mara, ukisema ubadili kila kitu utajikuta kwenye bei ya original.
 
Wapi naweza kupata spea za jumla za Kubota powertiller Dar es salaam
 
Kama una pesa ya kutosha powertiller nzuri ni Siam kubota ina 14 HP. Kama una mtaji mdogo nunua za kichina ambazo nazo ni long hand na zina 14 HP.

Hizi za mikono mifupi ni zina majembe mazito pia ni nzito mno hata utumiaji lazima kuwa watu zaidi ya mmoja wakati wa ufungaji wa majembe.

Wakati hizi za mikono mirefu ni nyepesi hata majembe yake ni mepesi, mtu mmoja tu anaoperate. Vile vile hizi za mikono mirefu hufanya kazi kwa uharaka zaidi.
Ok, kwahiyo naweza kwenda dukani nitachukua yoyote mradi ina mikono mirefu mkuu kutegemea na budget yangu
 
Kama una pesa ya kutosha powertiller nzuri ni Siam kubota ina 14 HP. Kama una mtaji mdogo nunua za kichina ambazo nazo ni long hand na zina 14 HP.

Hizi za mikono mifupi ni zina majembe mazito pia ni nzito mno hata utumiaji lazima kuwa watu zaidi ya mmoja wakati wa ufungaji wa majembe.

Wakati hizi za mikono mirefu ni nyepesi hata majembe yake ni mepesi, mtu mmoja tu anaoperate. Vile vile hizi za mikono mirefu hufanya kazi kwa uharaka zaidi.
Hizo za mikono mirefu za kichina ni bei gani?
 
Kama una pesa ya kutosha powertiller nzuri ni Siam kubota ina 14 HP. Kama una mtaji mdogo nunua za kichina ambazo nazo ni long hand na zina 14 HP.

Hizi za mikono mifupi ni zina majembe mazito pia ni nzito mno hata utumiaji lazima kuwa watu zaidi ya mmoja wakati wa ufungaji wa majembe.

Wakati hizi za mikono mirefu ni nyepesi hata majembe yake ni mepesi, mtu mmoja tu anaoperate. Vile vile hizi za mikono mirefu hufanya kazi kwa uharaka zaidi.
Je majembe ya Power tiller ya mikono mifupi ambayo umeeleza kuwa ni mazito yanaweza yakafungwa kwenye Power tiller ya mikono mirefu na Power tiller ikafanya kazi kwa ufanisi uleule au itazidiwa na uzito wa jembe na kupunguza ufanisi?.

Je jembe kubwa kabisa ambalo linaweza kufungwa kwenye Power tiller ya mikono mirefu na power tiller ikaendelea kufanya kazi ya kulima kwa ufanisi uleule lina disc ngapi?.

planter za kupandia nafaka kwa kutumia Power tiller nazo zipo? na zinapatikana wapi na kwa kiasi gani?.
 
Back
Top Bottom