Power tillers-msaada jamani

mama dunia

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
420
Reaction score
84
Hi wanajamvi, nina maswali kadhaa kuhusiana na power tillers

1. Je kuna aina ngapi angalau za power tillers?

2.Kwa DAR zinapatikana maduka gani na bei yake ikoje

4.Je ni durable power tillers? any experience

5.Kuna mtu kaniambia zinalima heka nne kwa siku ni kweli?

6.je zinatumia mafuta/oil kiwango kizuri au zinakula sana?

Nashukuru wanajamvi, mmekuwa msaada mkubwa kwangu, ushauri wote nimekuwa nikiufanyia kazi!
 
Zilizopo na za bei nafuu ni za kichina.Kulima eka nne sio realistic kwani inategemea aina ya udongo
Ulaji wa mafuta ni mzuri mno na unaweza kufunga pump ya maji na kama una mifugo inarahisisha sana.
It is worth investing on.
 
hapa dar es salaam mimi nilikutana nazo morogoro road karibu na makutano ya morogoro road na samora kuna maduka mengi sana ya mashine mbalimbali,generator na vingine vingi tembelea uone, pale duka moja nililopita wanauza tsh. 4M
 
Asante, naanza kupata picha, ninataka kuinvest yaani nilienda kijiji kimoja huwezi amini watu wanajipanga foleni kusubirizia kulimiwa na wanagombania balaa, ndo nikaona kama pia ni fursa, maana helka moja unalimiwa kwa sh. elf 50! so am not sure ni heka ngapi kwa siku maana ndo mmoja aliniambia ni heka 4 nikaona ni big ya opportunity..
 
hapa dar es salaam mimi nilikutana nazo morogoro road karibu na makutano ya morogoro road na samora kuna maduka mengi sana ya mashine mbalimbali,generator na vingine vingi tembelea uone, pale duka moja nililopita wanauza tsh. 4M

ohhh ok, najua yale Maeneo, kwahiyo nafkr zinatofautiana labda ukubwa/uwezo nk, nasikia kuna za milion 6 , asante sana ngoja nitaenda kucheck
 
Suala la kulima eka nne usilitilie maanani sana kwani inategemea sana ardhi kwa mfano ardhi ya kilosa kutokana na kuvamiwa na ngombe wengi power tiler hata eka moja hailipi.Kama umeona kwa macho yako ikilima then that is fine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…