Powered by Android.

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Asalaam aleykum Jamiyah, hapo awali kidogo ukinnunua simu dukani ilikuwa ni simu ambayo endapo ni Samsung, Nokia, tecno na kadhalika, wakati wa kuiwasha ilikuwa inakuja nembo halisi ya simu husika bila ya kuwa na andishi lolote linaloambatana yaani linakuja neno Samsung na mbwembwe zake kwenye screen kwa raha kabisa, lakini kwa sasa inakuwa tafrani kidogo simu nyingi mara ununuapo huja na maneno "powered by androids" pia nyingi huwa zinapatikana moto kwelikweli ambazo ndizo simu nyingi mno, Je simu hizi sio fake?
#Tujuzane wabobezi.
 
Ulitaka ziwe powered na nini?
 
Huo ni miongoni mwa ududu ambao utaukuta android,kitu kinawekwa sehemu isiyotakiwa bila sababu za msingi,mbaya zaidi logo na maandishi husika havina ubunifu kabisa kama kiraka.
 
Kwa kawaida wakati unawasha simu inatakiwa litokee neno Samsung katikati ya screen na mbwembwe zake! Kwa simu original.
Nadhani simu za android zinaonyesha powered by android mkuu, labda umezoea iPhone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…