PP kutotaja vielelezo wakati wa PH

abagabo

Senior Member
Joined
Jun 4, 2014
Posts
155
Reaction score
168
Heshima kwenu wanajamvi,

Hivi ni sahihi siku ya PH Jamuhuri kutotaja vielelezo walivyonanyo au watakavyotumia wakati wa ushahidi? Nimeshuhudia kwenye kesi ya ya jamaa yangu PP akisema vielelezo watavielezea siku ya ushahidi.

Je, ni sahihi? Je, kielelezo ambacho akikutajwa wakati wa PH kinaruhusiwa kupokelewa kwenye ushahidi? Je, kuna rejea yoyote ya high Court au CA inayohusu suala kama ili?

Msaada.
 
huku uwaoni wapo bize na siasa, ila Kwa uelewa wangu sidhani kama ni muhimu kutaja vielelezo ila wakihamua is okay,, hata muda mwingine inatokea wanataja na idadi ya mashahidi ambao watakuwa nao siku wanakusomea PH,
so hata kama hawajataja vielelezo ambavyo watavileta kesi itakapoanzwa kusikilizwa,bado uyo jamaa yako sidhani kama kuna haja ya yeye kuwa na hofu,, maana kama walimkamata na jembe wakaleta shoka, bado kutaitajika watoe ushahidi kuwa walimkamata na shoka sio jembe
 
Samahani.. kwa kudandia ..PH ndio Nini?
Sio mtaalamu wa sheria lakini kwa ninavojua PH ni kifupi cha Preliminary Hearing. Katika kesi za jinai baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa anasomewa maelezo ya awali ya kesi inayomkabil.

Hapa atasomewa taarfa binafsi zinazomhusu, tuhuma zinazomkabili n.k.
Mtuhumiwa ataombwa kusema ndio kwa taarifa za kwel na hapana kwa taarifa/maelezo anayoona ni ya uongo kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Lengo/dhumuni la PH ni kumsaidia prosecutor aweze kuandaa mashahidi wakuja kuthibitisha tuhuma zinazomkabili mtuhumiwa na kumtia hatiani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…