PPPTZ: Sasa ruksa wanaotaka kusambaza Umeme wa TANESCO kwa Wateja

PPPTZ: Sasa ruksa wanaotaka kusambaza Umeme wa TANESCO kwa Wateja

YAY

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
879
Reaction score
873
IMG-20260407-WA0082.jpg

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Oxford umeonesha kuwa katika nchi 13 tajiri zaidi duniani, takribani asilimia 25 ya nguvu ya uchumi hutokana na ufanisi wa kitaasisi. Hii ina maana kuwa taasisi zenye mifumo thabiti na uwajibikaji huongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kuliko hata rasilimali pekee.

Akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Nishati, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha PPP (PPPC), Bwana David Kafulila, alifafanua kuwa ucheleweshaji wa maandalizi ya miradi ina gharama kubwa ya kiuchumi ambayo mara nyingi haionekani. Alitoa mfano wa jambo linaloweza kuandaliwa kwa siku saba lakini likachukua miaka saba, kwani ni hasara kubwa kwa taifa na huathiri kasi ya maendeleo.

Akijibu hoja ya Profesa Semboja kuhusu sekta binafsi kupewa jukumu la kusafirisha umeme, Kafulila alikiri kuwa mjadala huo umekuwa mkali lakini ni kweli sekta binafsi inaweza kusafirisha umeme, japokuwa hofu imekuwa kubwa kama ilivyokuwa kwenye bandari na viwanja vya ndege.

Alibainisha kuwa tayari nchi chache duniani zimeanza, ikiwemo India na Brazili, na barani Afrika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ziko mbioni.

Kafulila alisisitiza kuwa hofu za kiusalama hazipaswi kuwa kikwazo cha moja kwa moja kwa miradi ya PPP badala ya kuikataa, serikali inapokuwa na masuala ya kiusalama inapaswa kutoa mapendekezo ya aina ya makubaliano na mikataba inayohitajika ili kulinda maslahi ya taifa, huku ikiruhusu miradi kusonga mbele na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.

Kafulila alihitimisha kwa kusisitiza kuwa Mikataba ya PPP ni structured na yenye uwezo wa kuleta uwiano wa nguvu kati ya sekta binafsi na sekta ya umma. Kwa mtazamo wa kiuchumi,

Aidha PPP ni chombo cha kuharakisha maendeleo, kuongeza ushindani, na kuimarisha uwajibikaji, huku ikihakikisha wananchi wanapata huduma bora na taifa linapiga hatua mbele kisiasa, kijamii na Kiuchumi.


View: https://www.instagram.com/reel/DW0z4UFgExU/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
 
Sijui miaka mingapi itapita kabla hatujaona vitendo!
 
Wana mzaha sana hawa watu.

TANESCO kwa kipindi cha miaka zaidi ya 30 muda pekee ambao wametengeneza 2019-2021.

Tofauti na hiyo miaka miwili kipindi cha Magufuli shirika la biashara lina operate kama ‘cost centre’ ya serikali kila siku wao ni kupewa ruzuku na kutengeneza hasara.

Leo tena wanatafuta uwekezaji wenye masharti ya malipo fixed + variable; historical TANESCO hawajawai meet such obligations in any contract which requires schedule payment. Mara zote serikali uishia kuwa mlipaji wa contrac zao.

TANESCO wanachojua ni kutengeneza hasara and it’s not rocket science huyo mwekezaji atataka government guarantee ya malipo, maintance costs zake zitakuwa kubwa, RoI kubwa and so are the charges kwa TANESCO.

Ni kutengeneza mgogoro kabla uwekezaji wenyewe aujaanza. Haka katumbili kanatumika vibaya sana kuharibu nchi, kenyewe kazi kuropoka ujinga tu kwa mambo ambayo anauelewa nao mdogo mno.

Mimi nawasifu wabongo sehemu moja tu confidence, yaani taahira mmoja anaweza toka hadharani na kuongea upuuzi wa mambo ambayo hana uelewa nayo kabisa and it’s OK.
 
Back
Top Bottom