Kwenye raga timu ya Kenya 7s inatajwa kati ya mabingwa duniani, hapa Afrika mpinzani ni SA tu. Timu ya raga 7s kwa kina dada, Kenya Lionesses, ndio mabingwa hapa barani Afrika, hivyo hivyo kwa Malkia Strikers kwenye mpira wa wavu. Harambee Starlets kwenye soka ndio wanawika ukanda huu wa Afrika Mashariki na ya Kati. Mpira wa Magongo tupo, Kriketi na Kabaddi pia hadi na Tong Il Mo Doo! 😀 Kwenye dondi wakenya wanashikilia belt kadhaa za kimataifa wakiongozwa na Fatuma Zarika. Hata kwenye soka Harambee Stars inawaongoza kwenye rank za FIFA. Kama kuna nchi ambayo ni 'Sports Powerhouse' ukanda huu ni Kenya, sio nyie vibwengo wengine na miguu yenu miwili miwili ya kushoto. 😎