Pre-primary education/chekechea imeleta impact yoyote katika elimu ya Tanzania au ni upotevu wa pesa tu?

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Watafiti tusaidieni hi miaka mitatu ya baby prep 1 prep 2 inao tumika na shule nyingi za mjini hususani private zenye gharama kubwa mpaka 1m kwa mtoto kuanzia 3- 6yrs kuanzia miaka ya 90s imeleta matokeo chanya katika makuzi na malezi ya watoto wetu ukiangalia performance ya hao watoto au ni kuongeza mzigo na umasikini kwa mzazi?

Kuanzia miaka ya 80s kurudi nyuma hayo madarasa ya prep hayakuepo mtoto alivokua na miaka 5 au sita alianza darasa la kwanza, au akianza kung"oa meno ya mbele au kushika sikio lake kwa kupitisha mkono, alianzishwa shule, kwa sasa hao wengi ndo wana siasa wetu na watumushi wa ummah walio wengi.

Suali langu je ukili nganisha utendaji wao hao ambao hawakusoma chekechea na hawa wahitimu wa miaka kuanzia 2000 kuna tofauti? Yupi ni imara zaidi?

Nisihukumiwe vibaya kwamba madarasa ya chekechea hayana umuhimu ila yanachosha wazazi kusomesha nakutumia pesa nyingi kama haina mchango bora mtoto anze darasa la kwanza moja kwa moja hizo pesa ununue kiwanja uanze maisha mdogo mdogo kuliko kipanga nyumba ya 1.2m kwa mwaka na ada ya chekechea ni 1 2m kwa mwaka wastage of resources.
 
Yamesaidia sana.
Ki vip tupe msaada wa hayo madarasa kwa jamii yetu ya Tanzania isije ikawa kwamba boda boda au madalali walio shamiri wengi wasasa ni wahitimu wa hayo madarasa na hazi yao kwa sasa ndo hiyo
 
Hapo ndipo tulipo. Kila zama na kitabu chake.

Hata tuition ya chekechea ipo.
Ndo hilo mimi naliita band wagon au mkumbo wa kutafuta social economic status, kweli mama unashida nyumbani unashindwa je kufundisha mwanao kuhesabu 1 mpaka 10, hadi ulipe 1m kwa wengine wakufundishie maneno mawili ya kiingereza ya "whats your names"
 
Yanasaidia kujua kusoma kuandika na kuhesabu katika kiingereza, ukizingatia kiingereza sio lugha ya kwanza kwenye nchi yetu, hatuna budi.

Mimi naona yalinisaidia
 
Tanzania hakujawahi kuwa na wateji Bora SI nyinyi wazee Wala vijana hata nikuuliza wastafu wa Tanzania mmelifanyia Nini taifa hutakuwa na Cha kujibu
 
Ki vip tupe msaada wa hayo madarasa kwa jamii yetu ya Tanzania isije ikawa kwamba boda boda au madalali walio shamiri wengi wasasa ni wahitimu wa hayo madarasa na hazi yao kwa sasa ndo hiyo
Bora bodoboda wanafanya kazi kuliko wazee waliokuwa ofisini miaka ya tisini na themanini hakuna kitu walifanya
 
Kwenye pre-primary education kuna kindergarten na day care. Sijui mwenzetu umelenga kipengele gani kati ya hivyo viwili maana vina malengo tofauti.

Day care kwa sasa inatumika kama sehemu ya kuacha watoto wadogo wapate sehemu ya kwenda wakati wazazi wapo busy kutafuta pesa.
Kindergarten au vidudu ndipo watoto huandaliwa kwaajiri ya primary level education. Hujifunza alphabets na wengine hutoka vidudu wakiwa vizuri wanajua kusoma na kuandika kabisa so wanaanza darasa la kwanza wakiwa vema.
 
Ndo hilo mimi naliita band wagon au mkumbo wa kutafuta social economic status, kweli mama unashida nyumbani unashindwa je kufundisha mwanao kuhesabu 1 mpaka 10, hadi ulipe 1m kwa wengine wakufundishie maneno mawili ya kiingereza ya "whats your names"
Ukiacha kujifunza "what is your name"Kama ulivyosema lkn pia mtoto anajifunza kusocialize na watoto wenzie pia michezo mbalimbali. Maana huwezi kuwa na kila kitu anachohitaji mtoto nyumbani.
Halafu walimu ni professional katika kufundisha watoto lkn sio kila mzazi ni mwalimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…