Kampuni ya Ndege ya Precision Air ina wanyanyasa abiria wa wanaokwenda mkoa wa Mtwara. Hii nimeishuhudia mwenyewe leo abiria hao ambao walikuwa waondoke saa tatu (3) asubuhi matokeo yake wakaambiwa wataondoka saa 9 mchana mara saa 10:30 na matokeo yake wakaambiwa hakuna usafiri na kupewa vyumba katika Hoteli ya TANSOMA. Ukiacha abiria wa leo hata jana hali ilikuwa hivyohivyo ingawa abiria wa jana waliondoka jioni badala ya asubuhi. Kama route ya Mtwara hailipi ifuteni ili abiria watafute usafiri mbadala.